Home » » MTOTO WA DARASA LA SITA ACHAPWA NA MWALIMU WAKE HADI KUPOOZA MIGUU.... KISA ALIKUNYWA MAJI YA SHULE BILA RUHUSA...

MTOTO WA DARASA LA SITA ACHAPWA NA MWALIMU WAKE HADI KUPOOZA MIGUU.... KISA ALIKUNYWA MAJI YA SHULE BILA RUHUSA...

tangazo
MWANAFUNZI wa darasa la sita, Ismail Godfrey (13) anayesoma katika Shule ya Msingi Maendeleo  Sinuka iliyopo mkoani Kigoma amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya kudai  kutandikwa viboko  na Mwalimu Muige Joseph na kupooza miguu.

 Mtoto huyo ambaye kwa sasa anapata matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar baada ya kukosa matibabu ya kina mkoani Kigoma alipokutana na mwandishi wetu alikuwa na haya ya kusema:  
“Awali sikuwa na matatizo yoyote ya kiafya hususan katika viungo vya mwili, isipokuwa haya yalinipata baada ya kuchapwa fimbo na mwalimu wangu ndipo nikapooza ghafla.
Miguu ya mtoto Ismail iliyopooza.
 
Tukio hili lilitokea mwezi wa tano nilipokuwa shuleni, nilipofika nilifungua bomba nikawa nakunywa maji kwa kuwa nilikuwa na kiu, ghafla mwalimu huyo alikuja na kuniambia kwa nini nachezea boma,  ndipo akaanza kunitandika viboko. 
 
 Hapo hapo nikahisi viungo vyote vya mwili vimepoa na miguu ikapata ganzi, nikaanguka chini baada ya kukosa nguvu,” alisema Ismail.
 
Kutokana na tukio hilo baba wa mtoto huyo,  Godfrey Lucas aliitwa  na baada ya kuona Ismail yupo katika  hali hiyo ya kupooza miguu aliamua kumpeleka katika Hospitali ya Mkoa, Maweni, kupatiwa matibabu, huku akifanya juhudi za kumtafuta mtuhumiwa ambaye alikuwa amekimbia makazi  yake.

Ismail Godfrey.
 
Hata hivyo , kutokana na juhudi za kumtafuta kwa kushirikiana na wananchi walifanikiwa kumkamata mwalimu huyo katikati ya mji wa Kigoma na kumfikisha polisi ambapo alifunguliwa kesi kwa jalada namba  KIGO/RB/2269/013 17/3/2013 SHAMBULIO LA MWILI.
 
Mtoto alianza kutokwa na vidonda miguuni ndipo nikaamua tuje hapa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na tukapokelewa na mtoto amelazwa wodi ya wagonjwa ya Kibasila, alisema. 
 
 Hata hivyo, amesikitika kuachiwa mtuhumiwa kwa dhamana wakati  mwanaye bado kalazwa na anakosa masomo kwa sababu yake.

Tupe Maoni yako!

KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DODOSO - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger