HAYA TENAAAA....... BINTI HUYU WA KIAFRIKA ANA LA KUSEMA .... SOMA ZAIDI......











DUH,,, IRENE UWOYA APOROMOSHA MATUS YA NGUONI,,, KISA,,,SOMA ZAIDI.....

 
“...Wale ma-(Tusi linalohusisha kiungo cha mwili) wanao post (Tusi kama la hapo mwanzo) humu...waaandike watakavyo...sio (Tusi- vitendo vibaya kwenye jamii) tuuu yan na vza yakuzunguka dunia nzima....siitaj watu ma-(Tusi kali sana)...kama na kuboa kafe mbele....eti range nimehongwa mtasubiri sanaaaa....sina mdaa huo sinaaa...wakukaa pemben na kumsmanga mtuuuu...wote mnao ni disss ma-(Tusi la kumalizia sentensi)...
  Hayo ni maneno ya mwadada Irene Uwoya aliyoaandika usiku wa leo hii kupitia ukurasa wake wa mtandao mmoja wa kijamii. Tulipoyasoma tuu, tulishtushwa sana kwani si kawaida kwa mwanadada huyu kuandika maneno mzito kama haya na ndipo tulipoamua kufanya utafiti yakinifu ili tujue why??? Na haya ndo majibu ya uchunguzi wetu huu…
Tujikumbushe Historia fupi Hivi majuzi mwadada Irene Uwoya alipost kwenye mtandao picha za gari yake mpya aina ya Range Rover na ndipo watu wengi walianza ku-comment na “kumponda” mwanadada huyu kuwa sio yake bali kahongwa na wanaume “wanaomuweka mjini”
Irene akajibu Siku si nyingi baadae Irene aliwajibu kwa kusema kuwa gari hiyo ni yake na wote wanaosema kahongwa watasubiri sana maana hiyo ni matokeo ya jasho lake
Msiba wa baba yake wema wahusishwa Kwa bahati mbaya mwanadada Wema Sepetu alipata matatizo ya kufiwa na baba yake hivi majuzi na ndipo zikatoka tetesi kuwa ETI mwanadada Irene pamoja na kundi jingine la mastaa Fulani wamesusa kuhudhuria msiba huo kwa madai kuwa Wema huwa hashiriki misiba ya wengine
Mashabiki wa wema wamjia juu Baada ya mambo hayo yote hapo juu ndipo kundi la mashabiki wa wema walipoanza kuandika kwenye ukurasa wa mwanadada huyo, wakimutukana na kumponda sana eti hilo gari sio lake bali kahongwa na jamaa mmoja hivi (Jina tunalihifadhi kwa sababu za kiusalama) na hivyo asiwadanganye wananchi mambo ambayo si kweli
Uvumilivu ukawa mchache kwa Irene Baada ya matusi na maneno mengi ya kejeli toka kwa mashabiki hao kumzidi Irene hatimaye ndio ameamua kuandika hayo hapo unayoyaona juu. Daah, hatari sana mjini hapa ukiwa staa.A

HAYA TENAAA,,, MCHINA AUKATA UUME WAKE BAADA YA KUKATALIWA NA DEMU WAKE......



Mwanaume mmoja wa Jiaxing, China amejikuta akichukua uamuzi mgumu wa kujikata uume wake baada ya nyota yake ya bahati katika mapenzi kushindwa kung’aa katika anga la maisha yake, kiasi cha kumfanya akate tamaa na kuamua kuchukua uamuzi huo.
  
 
Baada ya kujikata kiungo hicho muhimu katika mwili wa mwanaume, mchina huyo Yang Hu mwenye miaka 26 aligundua kwamba haikuwa ndoto ni kweli ameukataa uume wake, ndipo alipochukua baiskeli yake na kukimbia hospitali kwa matarajio ya kwenda kuunganishiwa kiungo chake alichokikata mwenyewe. 
 
Sipati picha aliwezaje kunyonga ‘pedal’ za baiskeli yake mpaka hospitali ilihali maumivu makali aliyokuwa nayo, lakini mbaya zaidi kutokana na kuchanganyikiwa kwa alichokifanya, baada ya kufika hospitali ndipo ndoto zake zikazidi kufifia baada ya madakrati kumueleza kuwa amesahau kuja na kiungo hicho ili kirudishiwe sehemu yake.
 
Hu alinyonga baiskeli yake tena kwa haraka kurudi nyumbani kuuchukua uume wake aliousahau na kurejea tena hospitali, lakini madaktari wakampa taarifa mbaya kuwa kutokana na kiungo hicho kutenganishwa na mwili na kukaa muda mrefu bila kuwa na damu haitawezekana tena kukiunganisha na mwili.

DAH,,,,,HABARI KUHUSU WALEMAVU WALIOPELEKWA MOMBASA NA MWANAMKE MMOJA KUFANAYA BIASHARA YA OMBAOMBA,,,,,SOMA ZAIDI


Citizen TV Kenya wanaripoti kwamba huko Mombasa wamekamatwa watu 26 wenye ulemavu ambao walichukuliwa kutoka Tanzania na Mwanamke Mtanzania ili kwenda kufanya biashara ya kuomba pesa na baadae jioni Mwanamke huyo anapitia mahesabu huku akiwa amewaweka walemavu hawa kuishi kwenye nyumba moja huko Mwembe tayari.
 
Mwanamke huyu nadaiwa kuwa na mtindo wa kuagiza Walemavu kuchukuliwa Tanzania na kuingizwa Kenya kupitia Taveta na Lungalunga ambapo anawatumia kibiashara yeye na washirika wake ambapo mpaka sasa washukiwa saba wametiwa mbaroni kutokana na hii ishu.

Taarifa inasema ombaomba hawa ambao wanatoka Shinyanga, Mwanza, Musoma na Bukoba wakiwa mitaani kuomba, wakipata shilingi mia tano ya Kenya tajiri anachukua shilingi 300 na anamuachia shilingi 200.

Mmoja wa Walemavu hao anasema ‘kabla ya kuletwa Kenya tunapewa ahadi nzuri za kuvutia kwenda, mimi niliahidiwa kupewa Baiskeli lakini kinachotokea sasa hivi ni kwamba nikipata hiyo pesa ya kuombaomba, Mwanamke huyu ndio anapanga bajeti zake wala hamna anachofanya’

MAJANGA..... KILA MSICHANA NINAEJARIBU KUMTONGOZA,,,,,,ANANIOMBA HELA,,,,JAMANI NISAIDIENI...HIKI NI NINI?????????

Mimi ni Kijana wa miaka 25 ninafanya kazi bank moja hapa Mjini ..nimefikia umri wa kutafuta mchumba wa kuoa ila hawa mabinti sijui wakoje kila ninaye mtongoza haipiti siku ananiomba hela kwa visingizio mbali mbali na mimi demu akishaniomba hela design hii hapo hapo naona sio namuona kimeo ndio wale wale ....Kwani Mapenzi siku hizi lazima usambaze Hela kwanza ndio upendwe ama? Naomba ushauri

INATIA HIZUNI.. MTU MMOJA AFARIKI MAHAKAMANI AKISUBIRI KUMTOLEA DHAMANA MWANAE


MTU mmoja aliyefahamika kwa jina la Tiger Mwaigomole (70) Mkazi wa kata ya Masukulu wilayani Rungwe amefariki dunia ghafla akiwa katika chumba cha Mahakama ya Wilaya ya Rungwe akifuatilia mwenendo wa kesi inayomkabili mtoto wake wakati Mahakama ikiendelea.

Tukio hilo la aina yake lilitokea hivi karibuni majira ya saa 9 alasiri ndani ya Mahakama hiyo ambapo Marehemu alifika mahakamani hapo akiwa na mwanaye aliyejulikana kwa jina la Lusajo Tiger (40) wakiwa na lengo la kumwekea dhamana ndugu yao Gwakisa Tiger ambaye alifikishwa mahakamani hapo akituhumiwa kwa kosa la kupigana na kujeruhi katika ugomvi uliotokea kijijini kwao.

Kwa mujibu wa mtoto wa Marehemu aliyekuwa ameongozana nae Mahakamani hapo Lusajo Tiger alisema wakati kesi ikiendelea chini ya Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Rungwe, Kingwele, ndugu yao alipandishwa kizimbani kusomewa mashtaka yanayomkabili ndipo marehemu alipoanza kutetemeka kwa madai kuwa anajisikia baridi kali sana.

Alisema kutokana na marehemu kulalamikia baridi aliamua kumnunulia chai ya moto ili anywe na kupunguza baridi ambapo baada ya kufanya hivyo marehemu alikata roho muda mfupi baada ya kumaliza kunywa chai aliyokuwa amepelekewa huku akiwa amekaa ndani ya chumba cha mahakama hiyo.

Kutokana na tukio hilo Askari polisi waliokuwepo mahakamani hapo waliuchukua mwili wa marehemu na kuukimbiza katika Hospitali ya Wilaya ya Rungwe Makandana kwa ajili ya vipimo lakini hata hivyo mwili ulikabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya taratibu za mazishi ingawa ripoti ya kifo chake haikutolewa mapema.

Wakati huo huo Hukumu ya kesi ya mauaji dhidi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Rungwe, John Mwankenja inayowakabili Hakimu Mwakalinga na wenzie watatu huenda ikatolewa Novemba 11 mwaka huu baada ya Mahakama kuu kanda ya Mbeya chini ya Jaji Samwel Karua kumaliza kusikiliza ushahidi wa upande wa mashtaka pamoja na utetezi kwa upande wa watuhumiwa.

Kwa mujibu wa Jaji Karua alisema baada ya kumaliza kusikiliza pande zote mbili atatumia muda wa siku mbili kwa ajili ya kuandika hukumu ambayo itaitoa Novemba 11, Mwaka huu, kesi ambayo inasimamiwa na Mwanasheria wa Serikali Archiles Mulisa huku watuhumiwa wakitetewa na Mawakili wawili wa kujitegemea ambao ni Simon Mwakolo na Victor Mkumbe.

INATIA UCHUNGU....WANANDOA HAWA WAKOSA MSIMAMIZI KATIKA NDOA YAO.....KISA.... SOMA ZAIDI,,,,,

Irene Malecela na mume wake, Sixmond Mdeka ‘Ras Six’ wakikata keki.
 
- WALIKOSA WASIMAMIZI WA NDOA
- MKE HAWEZI KWENDA CHOONI MWENYEWE


Irene Malecela na Sixmond Mdeka ‘Ras Six’ katika pozi.
 
WANAMUZIKI  wa kizazi kipya ambao ni wanandoa, Irene Malecela na mume wake, Sixmond Mdeka ‘Ras Six’, wamelieleza Dodoso  habari ya kusikitisha


Wanamuziki hao ambao kwa sasa ni wazazi wa mtoto mmoja anayeitwa Jason,  wamelieleza paparazi kuwa ulemavu walionao uliwafanya wakose wasimamizi kwenye ndoa yao.
Wawili hao mara baada ya kukosa wasimamizi kwa kila waliyekuwa wanakwenda kumwambia kuhusu suala hilo kukataa, walijitokeza Wazungu raia wa Italia ambao walikubali kuwasimamia.
 
Wakiongea kwa furaha nyumbani kwao Mbagala Maji-Matitu, wanandoa hao walisema wanafurahia sana maisha ya ndoa na wanawahimiza watu wengine wenye hali kama yao kutokata tamaa ya maisha na kama wana wapenzi wafunge ndoa kwani ni jambo lenye baraka na  wasiogope vikwazo.

 
Walikutana vipi na kuanzisha uhusiano?
Six na Irene walikutana Kinondoni kwenye bendi  inayoitwa Tunaweza  ambapo walikuwa wakifahamiana kutokana na wote kuwa wasanii na kuanzisha rasmi uhusiano. Irene alikuwa miongoni mwa wanachama waanzilishi na Six akiwa  meneja wa bendi hiyo.

 
Wawili hawa walianzisha uhusiano, yaani uchumba mwaka 2009 na 2011 mwishoni  walifanikiwa kufunga ndoa yao na sherehe kufanyika kwenye Ukumbi wa Msasani Beach ambapo ilihudhuriwa  na watu mbalimbali.
 
Kilichowanyong’onyesha kwenye ndoa
Wakati wakiandaa ndoa yao walijaribu kupita kwa kila mtu kutafuta wasimamizi  lakini walikataliwa kwa kunyanyapaliwa huku kila mmoja akiwa na sababu yake. 

 

 Walipokata tamaa, waliwaomba Wazungu ambao ni mke na mume ambao walikubali kuwasimamia ndoa yao.
 
“Ukweli tunawaheshimu sana Mr na Mrs Fundi waliokuwa hapa nchini kwani baada ya kuwaambia tu walikubali bila hata kuuliza swali la aina yoyote na walituunga mkono kwa hali na mali na kuifanya siku yetu kuwa ya kifahari,” alisema Sixmond.
 
Kinachowafurahisha ndani ya ndoa yao
“Tukiwa ndani ya ndoa tulifurahi sana siku tuliyofanikiwa kupata mtoto wetu wa kwanza, Jason, na mpaka leo tunamshukuru Mungu kwani amekua na anaendelea vema.

 
Matatizo wanayokutana nayo
Matatizo wanayokumbana nayo ni sehemu ya kuishi, kwani wanaishi mbali na mji na wamekuwa wakifanya kazi zao za muziki ambapo mwanamke anaimba na kundi lake la Survivor Sisters linaloundwa na wasichana walemavu watatu.  

 
 Mume anaimba kama ‘solo artist’   akiwa kwenye bendi ya muziki ya Tunaweza.  Hivyo kutokana na umbali, wakati mwingine wamekuwa wakifika nyumbani usiku sana kutokana na kutembea kwa shida.

Sisi yote tunaweza kuvumilia ila tatizo kubwa ni nyumba ya kuishi ambayo huwa ni lazima kuwe na mazingira yanayoendana na mke wangu, kwa sababu hali aliyonayo si ya kushea choo hasa sehemu zile ambapo huwa kinajengwa juu kwani kama hana mtu wa kumsaidia kumpadisha inakuwa ni tatizo.

“Kwa ujumla kwa yule aliye na nyumba ambaye anaweza kutupa tukaishi tutamshukuru sana na tutafanikiwa kufanya mambo makubwa ya maendeleo kwani mimi ninao uwezo wa kufanya kazi na mke wangu.  Kupitia muziki tunaweza kuendesha maisha yetu,” alisema Six.

Aliendelea kueleza kuwa mkewe na kundi lake wametoa wimbo wao unaoitwa Binuka-Binuka ambao uko mtaani na wanaomba watu waupokee na kuwapa kipaumbele.

Video ya mganga aliyekamatwa na kiganja cha binadamu kikivuja damu huko Mwanza

 
Watu watatu wakiwemo waganga wawili wa jadi wamekamatwa na polisi katika eneo la Igombe Tx, jijini Mwanza wakiwa na kiganja cha mkono wa kulia unaoaminika kuwa wa binadamu.
Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza, kamishna msaidizi wa polisi Joseph Konyo amesema tukio hilo limetokea eneo la kati ya ziwani na nyuma ya uwanja wa ndege wa Mwanza baada ya raia wema kuwapa taarifa za siri.

Mtoto wa miaka 8 alazimishwa kuwa housegeli....Mwajiri wake amchoma kisu


UKATILI! Katika hali ya kusikitisha, mtoto mwenye umri wa miaka 8 aliyejitambulisha kwa jina la Loveness na mwenzake aitwaye Anna, wanadaiwa kulazimishwa kufanya kazi za ndani huku wakipata vipigo vikali kutoka kwa waajiri wao.  

Loveness alikuwa akifanyishwa kazi Ubungo-Maziwa na Anna alikuwa Kimara jijini Dar. Watoto hao wameeleza kazi nzito wanazofanyishwa katika mazingira magumu wakiwa na umri mdogo, wanaohitaji kwenda shule.

“Mama (mwajiri wake) alikuwa akinipiga na wakati mwingine kunichanja na kisu,” alisema Loveness.
Majirani ambao hawakupendezwa na matukio hayo, walitutonya  ili kufuatilia suala hilo. Jirani mmoja ambaye hakutaka kutajwa, alidai kwamba alikuwa akiumizwa na mwajiri wa Anna ambaye alikuwa akimpa vipigo vikali mtoto huyo ambaye alikuwa akimlea mtoto wa mama huyo kila siku.
 

“Hakuna kitu kilichokuwa kikituumiza majirani kama mtoto Anna ambaye alikuwa akipata vipigo vikali kila siku iendayo kwa Mungu kutoka kwa mwajiri wake, heri arudi kwao,” alisema. Mtangazaji wa kipindi cha Wanawake Live kinachotetea haki za watoto na wanawake kupitia EATV, Joyce Kiria ambaye alitinga nyumbani kwa waajiri hao na kumkamata mmoja wao kisha  kumpeleka katika Kituo cha Polisi cha Kimara, Dar kwa ajili ya kujibu mashitaka ya kukaa na mtoto mdogo kama mfanyakazi.

  Hata hivyo, mtangazaji huyo aliamua kuwachukua watoto hao na kwenda kuishi nao nyumbani kwake Changanyikeni, Dar, kwa ajili ya kufanya utaratibu wa kuwasafirisha vijijini kwao ambapo Loveness anatokea Morogoro na Anna ametokea Singida.

  Joyce amekuwa akifanya mawasiliano na familia za watoto hao ili kuwarejesha kwao huku Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Sophia Simba na Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka wakiombwa kuangalia suala hilo la unyanyasaji kwa watoto kwa umakini mkubwa.

picha za mwili wa marehemu baba wema sepetu alipoagwa jijini dar, es salaam


BABA mzazi wa staa wa sinema za Kibongo ambaye pia ni Miss Tanzania 2006/2007 Wema Sepetu, Balozi Abraham Isaac Sepetu ameagwa jana  jioni  nyumbani kwake Sinza - Mori jijini Dar es Salaam.
 
Tukio hilo lilihudhuria na viongozi mbalimbali wa kiserikali akiwemo Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Warioba, Getrude Mongela pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Benard Membe na wengine wengi waliofika kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu aliyefariki dunia Jumapili ya wiki iliyopita.
 
Waziri Membe kwa niaba ya serikali ametoa salamu za rambirambi na kuchangia kiasi cha shilingi milioni  1, “Kwa niaba ya serikali tumechangia kiasi cha shilingi milioni 1. Hata mimi pia nilimfahamu marehemu kwa muda mrefu na alikuwa kiongozi makini, Mungu alilaze roho ya marehemu mahali pema peponi amen,” alisema Waziri Membe.
 
Mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa leo asubuhi kuelekea Zanzibar tayari kwa mazishi.
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 

HAYA TENA...... UCHOVU KITANDANI WAMFANYA MSANII HUYU WA KIKE WA BONGO MOVIE KUWACHUKIA WANAUME WA KIBONGO

Msanii  wa kike wa filamu bongo  maarufu kwa jina  la Husna Chobis ‘Avana’ amedai kuwa yeye hataki kuwa  na mwanaume wa kibongo kwa sababu wengi  wao ni waongo  na  hawayajui  mapenzi...
 
Akiongea  na  mwandishi  wetu, mrembo  huyo  alidai  kuwa  umaarufu  wake  humpa  wakati  mgumu  sana  wa  kumtambua  mwanaume  mkweli  maana  wengi  humtamani  kimapenzi  kutokana  na  jina  lake ( ustaa  wake )

  “Sitaki kuzalishwa   wala  kuwa  na  uhusiano wa  kudumu  na mwanaume  toka  Tanzania  maana  wengi  wao ni tapeli  na  hata  ukiwakubali   huwa hawajui  kitu . ALIFUNGUKA.....
 
"Bora kwa nchi za wenzetu kuna  ndoa za mikataba  kiasi  kwamba  mtu  unakuwa  unajua kabisa nitakuwa na huyu   kaka  kwa muda fulani , ntazaa  naye au ni wa raha tu.
 
"Hiyo  inasaidia  sana  kwa  sababu   kama huyo  kaka  ni   MSHAMBA inakuwa  ni  rahisi  kwako  kumpiga  chini  na  kuangalia  ustaarabu  mwingine”..alisema Avana

MTOTO WA DARASA LA SITA ACHAPWA NA MWALIMU WAKE HADI KUPOOZA MIGUU.... KISA ALIKUNYWA MAJI YA SHULE BILA RUHUSA...

MWANAFUNZI wa darasa la sita, Ismail Godfrey (13) anayesoma katika Shule ya Msingi Maendeleo  Sinuka iliyopo mkoani Kigoma amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya kudai  kutandikwa viboko  na Mwalimu Muige Joseph na kupooza miguu.

 Mtoto huyo ambaye kwa sasa anapata matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar baada ya kukosa matibabu ya kina mkoani Kigoma alipokutana na mwandishi wetu alikuwa na haya ya kusema:  
“Awali sikuwa na matatizo yoyote ya kiafya hususan katika viungo vya mwili, isipokuwa haya yalinipata baada ya kuchapwa fimbo na mwalimu wangu ndipo nikapooza ghafla.
Miguu ya mtoto Ismail iliyopooza.
 
Tukio hili lilitokea mwezi wa tano nilipokuwa shuleni, nilipofika nilifungua bomba nikawa nakunywa maji kwa kuwa nilikuwa na kiu, ghafla mwalimu huyo alikuja na kuniambia kwa nini nachezea boma,  ndipo akaanza kunitandika viboko. 
 
 Hapo hapo nikahisi viungo vyote vya mwili vimepoa na miguu ikapata ganzi, nikaanguka chini baada ya kukosa nguvu,” alisema Ismail.
 
Kutokana na tukio hilo baba wa mtoto huyo,  Godfrey Lucas aliitwa  na baada ya kuona Ismail yupo katika  hali hiyo ya kupooza miguu aliamua kumpeleka katika Hospitali ya Mkoa, Maweni, kupatiwa matibabu, huku akifanya juhudi za kumtafuta mtuhumiwa ambaye alikuwa amekimbia makazi  yake.

Ismail Godfrey.
 
Hata hivyo , kutokana na juhudi za kumtafuta kwa kushirikiana na wananchi walifanikiwa kumkamata mwalimu huyo katikati ya mji wa Kigoma na kumfikisha polisi ambapo alifunguliwa kesi kwa jalada namba  KIGO/RB/2269/013 17/3/2013 SHAMBULIO LA MWILI.
 
Mtoto alianza kutokwa na vidonda miguuni ndipo nikaamua tuje hapa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na tukapokelewa na mtoto amelazwa wodi ya wagonjwa ya Kibasila, alisema. 
 
 Hata hivyo, amesikitika kuachiwa mtuhumiwa kwa dhamana wakati  mwanaye bado kalazwa na anakosa masomo kwa sababu yake.

AJABU......KIGANJA CHA MKONO WA BINADAMU CHAKUTWA KWA MGANGA AKIMUUZIA MTEJA WAKE KWA KIASI CHA MILIONI 100 JIJINI MWANZA


Mtu mmoja jijini Mwanza anadaiwa kukamatwa na kiganja cha mtu akiwa anajiandaa kumuuzia mteja kwa sh million 100.

Washukiwa walikamatwa  jana  karibia na uwanja wa ndege wa Mwanza  wakifanya  biashara  hiyo  haramu....
 

 Baada  ya  upekuzi  wa  kina, mteja  alikuwa  ana  milioni  100  na mganga alikutwa  na   kiganja cha  binadamu  ambacho kilikuwa  kibichi kikitoa damu.

Kiganja  hicho  kilikuwa  kimevishwa  tunguri  na nywele za binadamu.

MAMBO YA LADY GAGA JUKWAANI LAIV BILA NGUO.....AKITUMBUIZA



         
       
Huyu  ni  msanii Lady Gaga  aliyeamua  kutoa  burudani   akiwa  uchi  wa  mnyama  katika show ya G-A-Y huko London, Uingereza Ijumaa iliyopita.

Gaga (27) alipanda jukwaani akiwa amevalia vazi linalomfunika hadi miguu lakini wakati akiendelea kuperform ghafla alianza kusaula taratibu kutokea juu hatimaye kulishusha vazi lote na kubaki uchi..

DAH... NGUMI ZAPIGWA KATI YA WADADA BARABARANI ETI KISA BWANA WANAEMGOMBANIA


Wadada wawili Warembo wa Mitaa ya kawe waliamua kuzichapa kavu kavu bila maglovsi mbele za watu kwa eti mmoja akimtuhumu mwenzie kuwa anatoka na Boyfriend wake...Inasemekana hawa madada ni marafiki sana lakini leo yamewashinda baada ya kuchangia bwana mmoja ...

UKATILI.. PANGA NA RUNGU VYATUMIWA NA BABA MZAZI WA MTOTO KUMWADHIBU KWA KOSA LA KUTOKWENDA SHULE HUKO MKOANI MBEYA

 
        
Victoria Mukama (10) baada ya matibabu
 
       Kabla ya matibabu
 
      
Mwalimu wa zamu wa Shule ya Msingi Airport, Damali Obadia alisema tukio hilo la ajabu lilitokea  majira ya saa mbili na nusu asubuhi ambapo akiwa ofisini alimuona mzazi huyo akiwa na mtoto huku akiendelea kumpiga wakielekea ofisini.
 
 
 
 Mama mzazi wa binti huyo Teodora Paulo alisema yeye na mume wake hawakuwepo nyumbani ambapo baada ya kurejea kutoka Msibani majira ya asubuhi walimkuta binti yao hajaenda shule na walivyomuuliza sababu ya kutoenda shule alijibu alikuwa havioni viatu vyake.
 
 
 
 majirani wa mtuhumiwa huyo walidai kuwa tabia ya Mwanaume huyo kufanya unyanyasaji inafichwa na mkewe ambaye anaonekana kuwa muoga wa kupigwa na mumewe na kuongeza kuwa anatabia ya kuandika makosa anayotendewa na mkewe
 
 
KATIKA hali isiyokuwa ya Kawaida, Baba mmoja aliyejulikana kwa jina la Oscar Mukama  mkazi wa Isengo Airport Jijini Mbeya amemjeruhi vibaya binti yake Victoria Mukama (10) kwa kumpiga sehemu mbali mbali za mwili wake akitumia vifaa vyake vya ulinzi likiwemo Lungu.

Kwa mujibu wa Mwalimu wa zamu wa Shule ya Msingi Airport, Damali Obadia alisema tukio hilo la ajabu lilitokea  majira ya saa mbili na nusu asubuhi ambapo akiwa ofisini alimuona mzazi huyo akiwa na mtoto huku akiendelea kumpiga wakielekea ofisini.

Alisema mzazi huyo baada ya kufika walimu walimpokea na kumuuliza kwa nini anampiga kiasi hicho mtoto wake alijibu mtoto ni wa kwake mwenyewe na alizaa kwa manufaa yake hivyo haoni sababu ya kuulizwa kuhusu kipigo kwa mwanaye.

Aliongeza kuwa baada ya walimu kumweleza kuwa kitendo alichokifanya ni cha kinyama na hakipaswi kutendeka Mzazi huyo alitoa kisu na kuwatishia walimu ikiwa ni pamoja na kutoa matusi makali dhidi yao ambapo walimu walifanikiwa kumtuliza na kumuomba amwache mtoto ili walimu wamwadhibu.

Alisema baada ya mzee huyo kuondoka na kumwacha mtoto walimpigia simu mama wa mtoto ambaye baada ya kufika shule alizimia kutokana na hali aliyomkuta nayo mtoto wake ambapo Walimu walitoa taarifa kwa Mwenyekiti wa Mtaa kasha kwenda Polisi kuchukua Fomu namba tatu (PF3) kwa ajili ya matibabu.

Mama mzazi wa binti huyo Teodora Paulo alisema yeye na mume wake hawakuwepo nyumbani ambapo baada ya kurejea kutoka Msibani majira ya asubuhi walimkuta binti yao hajaenda shule na walivyomuuliza sababu ya kutoenda shule alijibu alikuwa havioni viatu vyake.

Alisema baada ya kumsaidia kutafuta na kutofanikiwa kuviona baba yake ambaye nayeb alikuwa amejiandaa kwa ajili ya kwenda kazini kwake anakofanya kazi ya Ulinzi alimwamuru mwanaye kuvaa sare za shule na kwenda naye hivyo hivyo kwa kile alichodai anampeleka shule.

Alisema alishikwa na butwaa hadi kupoteza fahamu baada ya kumkuta mtoto amejeruhiwa huku akiwa amepigiwa simu na mumewe kwamba aende shule kumchukua mtoto wake lakini hakujua kama amepigwa kiasi cha kumjeruhi mtoto sehemu mbali mbali za mwili wake.

Akizungumzia kisa cha kupigwa kwake baada ya kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya katika Chumba cha dharula, Victoria Mukama (10) ambaye ni mwanafunzi wa darasa la nne katika Shule ya Msingi Airport alisema wakiwa njiani kuelekea shuleni alishangaa akianza kupigwa bila kuelezwa sababu ni nini.

Alisema alianza kupigwa tangu wanatoka nyumbani hadi wanafika shule iliyoumbali wa Mita 250 kutoka Nyumbani hadi Shuleni akitumia Virungu na fimbo huku akiwa ameshika kisu mkononi kwa ajili ya kuwatishia wanataka kumuokoa.

Kutokana na tukio hilo Jeshi la Polisi linaendelea kumtafuta Mtuhumiwa huyo wa unyanyasaji wa watoto baada ya kufunguliwa kwa jarada lenye namba MB/IR/9563/2013 katika kituo cha kati cha Polisi Mbeya.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa wa Pambogo Esia Edward ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa kamati ya Shule hiyo alisema kitendo kilichofanywa na mtuhumiwa huyo hitendo hakipaswi kufumbiwa macho hivyo ni lazima sheria ichukue mkondo wake kwa kuhakikisha vitendo hivyo vinakomeshwa ndani ya jamii.

Aliongeza kuwa hajawahi kusikia mtuhumiwa huyo kama amewahi kujihusisha na ukatili wa namna hiyo na kuongeza kuwa huwa anatoa ushirikiano vizuri katika ngazi ya mtaa na kuhudhuria vikao mbali mbali vinavyoitishwa pamoja na kuchangia mada.

Nao majirani wa mtuhumiwa huyo walidai kuwa tabia ya Mwanaume huyo kufanya unyanyasaji inafichwa na mkewe ambaye anaonekana kuwa muoga wa kupigwa na mumewe na kuongeza kuwa anatabia ya kuandika makosa anayotendewa na mkewe.

Walisema awali amewahi kuoa mke na kuzaa nae watoto watatu lakini mkewe huyo alikimbia baada ya kuona tabia ya unyanyasaji imezidi kutoka kwa Mwanaume huyo aliyetajwa kuwa ni jamii ya watu wa Mosoma Mkoani Mara ambako tabia kandamizi dhidi ya wanawake na watoto bado zinafanyika.

AJABU....MWIZI WA KUKU AVULIWA NGUO BAADA YA KUKAMATWA......AFUNGIWA NDANI YA TENGA NA WANANCHI TAYARI KWA KUCHOMWA MOTO



Huyu  ni  mkenya   aliyekuwa  ameiba  kuku.Wananchi  walipomnasa walimpa  kichapo  kikali  na  kisha  kumfungia  ndani  ya  tenga  la  kuku  kwa  ajili  ya  kumchoma  moto….

Wangali  katika  maandalizi  ya  kutafuta  petrol, polisi  waliwasili  eneo  la  tukio  na  kumuokoa  kwa  kumpeleka  kituoni

LESENI ZA MAFUTA NA GESI ZAPINGWA NA MNYIKA


WAZIRI Kivuli wa Nishati na Madini, John Mnyika, amemtaka Rais Jakaya Kikwete kusitisha mzunguko wa nne wa utoaji wa leseni za utafutaji wa gesi asili na mafuta hadi sera na sheria ya gesi asili zikamilike, na marekebisho ya sera ya nishati na sheria za mafuta yafanyike. 

Mnyika ambaye pia ni mbunge wa Ubungo (CHADEMA), alisema hatua hiyo ni kurejea maoni na mapendekezo aliyoyawasilisha bungeni kwa niaba ya Kambi Rasmi ya Upinzani Mei 22 mwaka huu.
 
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, alisema rais anapaswa kuchukua hatua hiyo kwa kuzingatia kwamba Mei 25 mwaka huu, badala ya kushughulikia mapendekezo hayo, Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo alitoa majibu ya uongo na upotoshaji bungeni kuhusu masuala mbalimbali.
 
Aidha Ikulu inapaswa kueleza iwapo Baraza la Mawaziri chini ya Rais Kikwete ndilo lililofanya uamuzi wa kuendelea na mchakato wa kutoa leseni za vitalu vya utafutaji wa gesi asili bila ya kuwepo kwa sera ya gesi asili na sheria ya gesi asili, na sera ya nishati na sheria zinazohusu mafuta au ni maamuzi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) na Wizara ya Nishati na Madini,” alisema.
 
Mnyika aliongeza kuwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda anapaswa kueleza iwapo kauli ya kejeli, dharau na uongo ya hivi karibuni iliyotolewa na Waziri Muhongo, kwamba uwezo wa wafanyabiashara wa Tanzania ni kuwekeza kwenye soda na juisi, si kwenye sekta ya gesi, ni msimamo wa serikali au maoni ya waziri binafsi.
 
“Izingatiwe kwamba Wizara ya Nishati na Madini, kupitia Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC), imetangaza mzunguko wa nne wa utoaji leseni za utafiti wa gesi asili na mafuta katika vitalu nane ndani na nje ya maji ya Ziwa Tanganyika vyenye ukubwa wa kilomita za mraba elfu tatu kila kimoja utakaofanyika Oktoba 2013.
  
Serikali pia imetenga mipaka ya vitalu viwili kwenye bahari kuu, na kuingia ubia wa utafiti na kampuni inayoitwa mbia wa kimkakati (Strategic Partner) ambae serikali haijamtaja,” alisema.
 
Alisema mchakato huu unafanyika wakati taifa likiwa halina sera (mchakato wa kuiandika bado unaendelea) na hatimaye yaanze maandalizi ya kupata sheria mahususi za kusimamia sekta ndogo ya gesi, hatua ambayo inapaswa kuambatana na marekebisho ya kisera na kisheria ya sekta.
 
Aliongeza kuwa tayari Tanzania imeshafanya ugunduzi wa futi za ujazo zaidi ya trilioni 32 za gesi katika maeneo kadhaa nchini, hivyo kuifanya kuwa kati ya nchi vinara wa gesi nyingi Afrika na duniani.
 
Utajiri huu wa gesi hadi sasa hauna sera wala sheria zinazotoa mwongozo wa usimamizi na udhibiti wake, ili kuhakikisha unawanufaisha Watanzania, kuepuka makosa yaliyofanyika katika uwekezaji mwingine wa gesi asili na rasilimali nyingine uliofanyika bila mifumo thabiti,” alisema.

MKE WA MTU ANASWA AKIJIUZA HUKO BUGURUNI

 
Mchumba huyo wa mtu aliyejitambulisha kwa jina moja la Diva alitoa kali ya mwaka baada ya kuzimia ghafla huku akitokwa na mapovu kinywani baada ya kunaswa  akijiuza.
  
Tukio hilo lilitokea wiki iliyopita maeneo ya Kimboka, Buguruni, Dar ambapo msichana huyo pamoja na ‘madadapoa’ wenzake walikuwa wakifanya biashara hiyo haramu bila kificho.
 
Mara baada ya kuona wenzake wakiwa mikononi mwa nguvu za dola katika kamatakamata ya polisi, mrembo huyo ambaye baadaye alijitambulisha kama mchumba wa mtu, alianguka ghafla na kuzimia kiasi cha kuzua hofu miongoni mwa machangu wenzake walioangua kilio wakidhani mwenzao amekata ringi (kufa).
 
Baada ya muda msichana huyo alirejewa na fahamu akiwa mikononi mwa polisi na kuanza kuangua kilio akiomba asikamatwe kwa kuwa yeye ni mchumba wa mtu na atakuwa kwenye wakati mgumu kama mchumba’ke atajua anajiuza.


Naomba msinikamate. Mimi ni mchumba wa mtu afande. Mtaniweka kwenye wakati mgumu kama akijua nilikuwa nikijiuza. Jamani nitamkosa mchumba wangu Luka,” alisema mrembo huyo huku akiomba maji ya kunywa.
 
Hata hivyo, kilio chake hakikuwazuia  waandishi  kufanya kazi yake ndani ya Kituo cha Polisi
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DODOSO - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger