Home » » HAYA TENAAA,,, MCHINA AUKATA UUME WAKE BAADA YA KUKATALIWA NA DEMU WAKE......

HAYA TENAAA,,, MCHINA AUKATA UUME WAKE BAADA YA KUKATALIWA NA DEMU WAKE......

tangazo

Mwanaume mmoja wa Jiaxing, China amejikuta akichukua uamuzi mgumu wa kujikata uume wake baada ya nyota yake ya bahati katika mapenzi kushindwa kung’aa katika anga la maisha yake, kiasi cha kumfanya akate tamaa na kuamua kuchukua uamuzi huo.
  
 
Baada ya kujikata kiungo hicho muhimu katika mwili wa mwanaume, mchina huyo Yang Hu mwenye miaka 26 aligundua kwamba haikuwa ndoto ni kweli ameukataa uume wake, ndipo alipochukua baiskeli yake na kukimbia hospitali kwa matarajio ya kwenda kuunganishiwa kiungo chake alichokikata mwenyewe. 
 
Sipati picha aliwezaje kunyonga ‘pedal’ za baiskeli yake mpaka hospitali ilihali maumivu makali aliyokuwa nayo, lakini mbaya zaidi kutokana na kuchanganyikiwa kwa alichokifanya, baada ya kufika hospitali ndipo ndoto zake zikazidi kufifia baada ya madakrati kumueleza kuwa amesahau kuja na kiungo hicho ili kirudishiwe sehemu yake.
 
Hu alinyonga baiskeli yake tena kwa haraka kurudi nyumbani kuuchukua uume wake aliousahau na kurejea tena hospitali, lakini madaktari wakampa taarifa mbaya kuwa kutokana na kiungo hicho kutenganishwa na mwili na kukaa muda mrefu bila kuwa na damu haitawezekana tena kukiunganisha na mwili.

Tupe Maoni yako!

KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DODOSO - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger