Showing posts with label UDAKU. Show all posts
Showing posts with label UDAKU. Show all posts

HAYA SASAAA,,, VIASHIRIA VINAVYOMUONYESHA MPENZI MPYA KUWA WEWE NI KIN'GAN'GANIZA KWAKE....

Mwanamke: Dalili zitakazomfanya mpenzi mpya akuone wewe ni king’ang’anizi…!

Hizi ni miongoni mwa sababu ambazo wanaume wengi huchomoa mapema kwa wapenzi wao wapya kabla uhusiano haujashika kasi. Kuna wakati wanawake hukosea na kuvuka mipaka mwanzoni tu mwa uhusiano. Anamganda mwanaume haraka sana au anaonesha dalili zote za kujipendekeza kupita kiasi. Lakini jambo ambalo wanawake wengi hawalijui ni kwamba, wanaume wako makini sana kuwakwepa wanawake ving’ang’anizi……..

Nitadadavua baadhi ya vijitabia vya wanawake vinavyowafanya wanaume wawaone kama ni ving’ang’anizi…..
1. Unataka kuwa naye muda mwingi kuliko kawaida… Ni vizuri kwa wapenzi wapya kupata fursa ya kuwa pamoja peke yao, lakini kama unakataa kuwa na mtoko, kuhudhuria sherehe au kukutana na marafiki na kulazimisha kuwa pamoja peke yenu mahali fulani pa faragha, basi hapo ni lazima mwanaume atadhani kwamba unataka akupe umuhimu wa pekee muda wote. Unaweza kukuta mwanamke anakuwa king’ang’anizi kiasi kwamba hana muda na marafiki zake au watu wengine isipokuwa mpenzi wake. Anakuwa kama mzigo, muda wote yuko nyuma ya mwanaume kila anapokwenda…. Hapa ni lazima mwanaume atatemana na wewe kungali mapema. Hakuna mwanaume anayeweza kujenga mahusiano na mwanamke wa aina hii, watakukimbia kila siku.

2. Unampangia mwanaume kila kitu… Unampangia aina ya mavazi ya kuvaa, unaanza kuboresha mazingira ya nyumbani kwake haraka sana kwa kununua vitu mbalimbali vya nyumbani kwake bila kushauriana naye. Hiyo ni dalili kwamba una matarajio makubwa kwake, jambo ambalo kwake yeye bado halijamuingia akilini. Hapa mwanaume ambaye huyachukulia mambo kwa tahadhari, hukuona kuwa wewe ni king’ang’anizi na unataka kukita mizizi kwake wakati bado anachunguza uhusiano wenu ili kujua iwapo utakuwa kama vile anavyotarajia yeye… Kumbuka kwamba kila mtu ana sifa azitakazo pale anapochagua mwenza, na ni vigumu kumjua mtu kwa muda mfupi. Kunahitajika muda wa kutosha mtu kumjua mwenzake vizuri linapokuja swala la mahusianao. 


3. Unatumia muda mwingi zaidi kukaa kwake…. Unalala kwa mpenzi wako, na asubuhi mwanaume huyo anaondoka kwenda kwenye shughuli zake, na wewe unabaki labda ukidai unamsaidia usafi kidogo. Lakini anaporudi jioni anakukuta bado uko hapo nyumbani kwake ukiwa umejipumzisha. Inawezekana ukawa umeandaa chakula cha usiku tayari na pia huenda ukawa umebeba nguo za kubadilisha kwenye mkoba wako pamoja na vipodozi ukiwa umejiandaa kulala tena hapo kwake. Huonyeshi dalili za kuondoka hapo kwake zaidi ya kwenda kwako au kwenu na kubadilisha nguo na kuchukua viti vichache utakavyovihitaji utakapokuwa hapo kwake, lakini unapanga hayo yote bila kumshirikisha zaidi ya kukuona tu ukimganda kama luba. Huonyeshi kuwa na maisha yako kama wewe, zaidi ya kujipachika kwake……


4. Unajenga urafiki na mama yake haraka sana…… Baada ya kukutambulisha kwa mama yake na kubadilishana namba za simu au labda na email, unaanza kujenga ukaribu na mama yake kupita kiasi. Wanawake wengi hudhani kwamba, iwapo watajenga urafiki na mama wakwe watarajiwa, basi itakuwa rahisi kwao kumnasa mwanaume huyo, maana huamini kwamba watoto wa kiume hawawezi kwenda kinyume na mama zao linapokuja swala la kuchagua mwenza. Kwa kawaida wanaume humuona mwanamke anayejipendekeza kwa mama yake kama vile anataka kulazimisha uhusiano au ndoa, hivyo humchukulia kama ni king’ang’anizi.




5. Unampigia simu na kumuuliza kama yuko wapi….. Unapompigia simu badala ya kumjulia hali unakuwa na maswali ya kipolisi.. ‘Uko wapi?’ ‘Unafanya nini? Maswali ya aina hiyo mwanaume huyachukulia kama ya kimtego na hawafurahishwi nayo. Wanawake wengi huamini kwamba wanaume huwa hawasemi ukweli kuhusu mahali walipo pale wanapoulizwa na wenzi wao. Jambo hilo linaweza kuwa kweli au lisiwe kweli. Inawezekana kuwa kweli kwa sababu labda ya wanaume kukwepa maswali mengi. Mara nyingi wanawake hawaridhiki na jibu moja. Mfano ni jioni ndio ametoka kazini, lakini nakapitia mahali fulani kukutana na rafiki yake, inawezekana ikawa ni kwenye mghahawa au kwenye baa. Kama mwanamke akipiga simu na mwanaume akamwambai yuko kwenye baa na rafiki yake, yatafuata maswali lukuki. Hakuna mwanaume anayependa kuulizwa maswali mengi kama vile anatuhumiwa. Na ndio sababu wanaume wengi wanakwepe kusema mahali walipo. Kwa hiyo ili kuepuka maswali anaweza kujibu kwa kifupi tu kwamba yuko kwenye kikao kazini na hatakuwa hewani, ili apate nafasi ya kuzima simu japo kwa muda. Mwanaume humuona mwanamke mwenye udadisi wa aina hiyo kama king’ang’anizi. 


6. Unakuwa na chuki na wanawake wenzako… Pale ambapo mwenzi wako anapomtaja mwanamke fulani, inaweza kuwa ni mfanyakazi mwenzake, mke wa kaka yake au mtu wanayeshirikiana kibiashara, unaonyesha kisirani cha waziwazi kwamba unakerwa na ukaribu wake na wanawake wengine. Tabia hii inaashiria kwamba wewe unapenda kumiliki na wanaume wengi huwa hawapendi wanawake wenye vijitabia vya kupenda kumiliki. Hapo ni lazima utaonekana kuwa wewe ni king’ang’anizi na uhusiano wenu utavunjika mapema…..

7. Unakubali kila analosema au kila anachokifanya….Kuna kitu kinaitwa ‘uhusiano wa kinyonga.’ Hapa mwanamke anajibadili kupita kiasi ili afanane na mwenzi wake. Unakuta mwanamke anakubali kila kitu anachokiamini mwenzi wake bila kuhoji. Anapoteza utambulisho wake na kujipachika utambulisho wa mwenzi wake. Mwanaume akikuona uko hivyo, atakukimbia, atajua wewe ni king’ang’anizi
8. Unawazungumzia mabwana ulioachana nao kila wakati…Kama una kawaida ya kumzungumzia mwanaume uliyeachana naye mara kwa mara uwapo na mpenzi wako mpya, ina maana kwamba bado hujaachana na jakamoyo la kuachwa. Hakuna mwanaume anayependa kusikia kuhusu mahusiano yako ya nyuma, kwa sababu hayamuhusu. Kama ukiwa unapenda kumzungumzia mpenzi wako wa zamani kila uwapo na mpenzi wako mpya, jua kwamba na yeye pia utampoteza kwa sababu atakuona kuwa wewe ni dhaifu na king’ang’anizi na ndio maana umeshindwa kusimama kama wewe, na badala yake unawaza kuhusu mtu uliyeachana naye pamoja na kwamba uko naye. Sio kwamba ni vibaya kumzungumzia mpenzi mliyeachana, lakini ni vyema kama utamzungumzia pale ambapo kuna ulazima sana wa kufanya hivyo, labda kuna jambo ambalo limamhusu ambalo mnajadili, na ikakulazimu kumtaja…..

UCHAFU,,,, MCHUMBA WA MTU AFUMANIWA NA MSANII MAKABURINI

Na Issa Mnally

MREMBO aliyetajwa kwa jina moja la Ema aliyedai kuwa ni mchumba wa jamaa aliyemtaja kwa jina la Amri au Mdudu amefumaniwa laivu akisaliti penzi na mwanaume mwingine.
Mchumba wa mtu akipewa kichapo baada ya kufumaniwa.
Tukio hilo la aina yake lilijiri kwenye Makaburi ya Buguruni, Dar, mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya kuwekewa mtego.
TAARIFA KWA OFM

Wakati makachero wa Oparesheni Fichua Maovu wakiwa kwenye ‘patroo’ walipokea taarifa kutoka kwa chanzo chake…


MREMBO aliyetajwa kwa jina moja la Ema aliyedai kuwa ni mchumba wa jamaa aliyemtaja kwa jina la Amri au Mdudu amefumaniwa laivu akisaliti penzi na mwanaume mwingine.
Mchumba wa mtu akipewa kichapo baada ya kufumaniwa.
Tukio hilo la aina yake lilijiri kwenye Makaburi ya Buguruni, Dar, mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya kuwekewa mtego.

TAARIFA KWA OFM
Wakati makachero wa Oparesheni Fichua Maovu wakiwa kwenye ‘patroo’ walipokea taarifa kutoka kwa chanzo chake ambacho kiliomba wafike katika makaburi hayo ambapo kulikuwa na fumanizi.
OFM: Fumanizi la aina gani? Isije ikawa ni wanandoa tukaingia chaka.
Watuhumiwa baada ya kutolewa kwenye teksi walimokuwa wanafanya yao.
Chanzo: Hawa bado ni wachumba tu. Jamaa alikuwa anamfuatilia mchumba’ke amemnasa na jamaa kwenye gari wakifanya mapenzi sasa kuna timbwili zito.
 
OFM: Una uhakika na unachokisema?
Chanzo: Kama hamtaki acheni (akakata simu).

OFM KAZINI
Kwa kuwa OFM haipuuzii habari, ilimteua ‘kamanda’ wake mmoja ambaye aliwasha bodaboda na kuwahi eneo la tukio.
 
Huku sekeseke likiendelea makaburini hapo, Mdudu ambaye alikuwa na jazba ya kuibiwa ‘mali’ zake alisema kuwa alitonywa na rafiki zake kwamba mchumba’ke huyo yupo katika Baa ya Kimboka, Buguruni akijirusha na jamaa huyo.
...Mchumba wa mtu akizidi kupokea kipondo.
Mdudu alisema aliamua kwenda katika baa hiyo na kubana sehemu huku akishuhudia kila kitu.
 
“Unajua nimekuwa nikiambiwa tu kuwa Ema ananisaliti lakini nilikuwa napuuzia.
 
“Sasa nimeamini baada ya kumshuhudia mwenyewe akisaliti penzi letu,” alisema Mdudu.

VIKAO VYA HARUSI
Alisema kuwa Ema ni mchumba’ke na anaishi na wazazi wake Buguruni-Malapa, Dar na ameshamtolea mahari.
 
“Ndiyo tumeanza kupanga vikao vya harusi vifanyike katika Baa ya Wazee iliyopo Ilala-Amana (Dar),” alisema.
...Kipigo kikiendelea kwa mchumba wa mtu.
Alisema baada ya kuwasubiri hadi usiku wa manane, aliwaona wakiinuka na kuingia kwenye teksi ndipo na washikaji zake nao wakachukua bodaboda na kuifuata ile teksi kwa nyuma bila wahusika kushtuka.

WAKUTWA LAIVU
Alisema walishangaa kuona gari lile likipaki maeneo ya Makaburi ya Buguruni kisha dereva akatoka na kwenda kusimama mbali kidogo akivuta sigara.

“Machale yakanicheza nikawatonya wanangu kuwa tusubiri kama dakika kumi halafu tukaivamie teksi.
Watuhumiwa wakiwekwa sawa kabla ya kupelekwa kituo cha polisi.
“Baadaye uzalendo ulinishinda ikabidi nikavamie. Ndipo tukawakuta laivu wanavua nguo wakiwa kimahaba,” alisema Mdudu.

Alisema roho ilimuuma alipomkuta mchumba’ke huyo ambaye anampenda kwa dhati akiwa katika hali ile, nusura apoteze fahamu na mara baada ya kuwavamia waliwatoa nje ndipo sekeseke likaanza.

KUMBE NI MSANII!
Wakati mtiti ukiendelea, yule mwanaume mwingine aligundulika kuwa kumbe ni msanii wa Bongo Fleva aliyejitambulisha kwa jina la Spince Seseme.
 
Mchumba wa mtu akitoka nduki baada ya kuchoropoka mikononi mwa jamaa waliokuwa wakimpa kipigo.

Akihojiwa na Ijumaa Wikienda kulikoni kufumaniwa na mke wa mtu, Spince alisema hakufahamu kama Ema ni mchumba wa mtu kwani kama angefahamu asingetoka naye kimapenzi.

ANATUMIA UMAARUFU WAKE?
Jamaa huyo aliyeimba Wimbo wa Ayaya akimshirikisha Ali Kiba alidai alifahamiana na Ema siku nyingi na hawakuwahi kuvunja amri ya sita.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wanaomjua jamaa huyo, eti amekuwa akitumia umaarufu wake kupindua uhusiano wa watu na kuapa kumkomesha.“Kama polisi wakishindwa tutamwendea kwa babu ili ajue cha mtu mali,” alisikika brazameni mmoja.

POLISI
Hata hivyo, tukio hilo lilimalizika kwa kila mmoja kukimbilia Kituo cha Polisi cha Buguruni akidai kupigwa ambapo hadi OFM inaondoka walikuwa wakichukuliwa maelezo.

HAYA TENAAAA....... BINTI HUYU WA KIAFRIKA ANA LA KUSEMA .... SOMA ZAIDI......











DUH,,, IRENE UWOYA APOROMOSHA MATUS YA NGUONI,,, KISA,,,SOMA ZAIDI.....

 
“...Wale ma-(Tusi linalohusisha kiungo cha mwili) wanao post (Tusi kama la hapo mwanzo) humu...waaandike watakavyo...sio (Tusi- vitendo vibaya kwenye jamii) tuuu yan na vza yakuzunguka dunia nzima....siitaj watu ma-(Tusi kali sana)...kama na kuboa kafe mbele....eti range nimehongwa mtasubiri sanaaaa....sina mdaa huo sinaaa...wakukaa pemben na kumsmanga mtuuuu...wote mnao ni disss ma-(Tusi la kumalizia sentensi)...”
  Hayo ni maneno ya mwadada Irene Uwoya aliyoaandika usiku wa leo hii kupitia ukurasa wake wa mtandao mmoja wa kijamii. Tulipoyasoma tuu, tulishtushwa sana kwani si kawaida kwa mwanadada huyu kuandika maneno mzito kama haya na ndipo tulipoamua kufanya utafiti yakinifu ili tujue why??? Na haya ndo majibu ya uchunguzi wetu huu…
Tujikumbushe Historia fupi Hivi majuzi mwadada Irene Uwoya alipost kwenye mtandao picha za gari yake mpya aina ya Range Rover na ndipo watu wengi walianza ku-comment na “kumponda” mwanadada huyu kuwa sio yake bali kahongwa na wanaume “wanaomuweka mjini”
Irene akajibu Siku si nyingi baadae Irene aliwajibu kwa kusema kuwa gari hiyo ni yake na wote wanaosema kahongwa watasubiri sana maana hiyo ni matokeo ya jasho lake
Msiba wa baba yake wema wahusishwa Kwa bahati mbaya mwanadada Wema Sepetu alipata matatizo ya kufiwa na baba yake hivi majuzi na ndipo zikatoka tetesi kuwa ETI mwanadada Irene pamoja na kundi jingine la mastaa Fulani wamesusa kuhudhuria msiba huo kwa madai kuwa Wema huwa hashiriki misiba ya wengine
Mashabiki wa wema wamjia juu Baada ya mambo hayo yote hapo juu ndipo kundi la mashabiki wa wema walipoanza kuandika kwenye ukurasa wa mwanadada huyo, wakimutukana na kumponda sana eti hilo gari sio lake bali kahongwa na jamaa mmoja hivi (Jina tunalihifadhi kwa sababu za kiusalama) na hivyo asiwadanganye wananchi mambo ambayo si kweli
Uvumilivu ukawa mchache kwa Irene Baada ya matusi na maneno mengi ya kejeli toka kwa mashabiki hao kumzidi Irene hatimaye ndio ameamua kuandika hayo hapo unayoyaona juu. Daah, hatari sana mjini hapa ukiwa staa.A

HAYA TENAAA,,, MCHINA AUKATA UUME WAKE BAADA YA KUKATALIWA NA DEMU WAKE......



Mwanaume mmoja wa Jiaxing, China amejikuta akichukua uamuzi mgumu wa kujikata uume wake baada ya nyota yake ya bahati katika mapenzi kushindwa kung’aa katika anga la maisha yake, kiasi cha kumfanya akate tamaa na kuamua kuchukua uamuzi huo.
  
 
Baada ya kujikata kiungo hicho muhimu katika mwili wa mwanaume, mchina huyo Yang Hu mwenye miaka 26 aligundua kwamba haikuwa ndoto ni kweli ameukataa uume wake, ndipo alipochukua baiskeli yake na kukimbia hospitali kwa matarajio ya kwenda kuunganishiwa kiungo chake alichokikata mwenyewe. 
 
Sipati picha aliwezaje kunyonga ‘pedal’ za baiskeli yake mpaka hospitali ilihali maumivu makali aliyokuwa nayo, lakini mbaya zaidi kutokana na kuchanganyikiwa kwa alichokifanya, baada ya kufika hospitali ndipo ndoto zake zikazidi kufifia baada ya madakrati kumueleza kuwa amesahau kuja na kiungo hicho ili kirudishiwe sehemu yake.
 
Hu alinyonga baiskeli yake tena kwa haraka kurudi nyumbani kuuchukua uume wake aliousahau na kurejea tena hospitali, lakini madaktari wakampa taarifa mbaya kuwa kutokana na kiungo hicho kutenganishwa na mwili na kukaa muda mrefu bila kuwa na damu haitawezekana tena kukiunganisha na mwili.

MAJANGA..... KILA MSICHANA NINAEJARIBU KUMTONGOZA,,,,,,ANANIOMBA HELA,,,,JAMANI NISAIDIENI...HIKI NI NINI?????????

Mimi ni Kijana wa miaka 25 ninafanya kazi bank moja hapa Mjini ..nimefikia umri wa kutafuta mchumba wa kuoa ila hawa mabinti sijui wakoje kila ninaye mtongoza haipiti siku ananiomba hela kwa visingizio mbali mbali na mimi demu akishaniomba hela design hii hapo hapo naona sio namuona kimeo ndio wale wale ....Kwani Mapenzi siku hizi lazima usambaze Hela kwanza ndio upendwe ama? Naomba ushauri

HAYA TENA...... UCHOVU KITANDANI WAMFANYA MSANII HUYU WA KIKE WA BONGO MOVIE KUWACHUKIA WANAUME WA KIBONGO

Msanii  wa kike wa filamu bongo  maarufu kwa jina  la Husna Chobis ‘Avana’ amedai kuwa yeye hataki kuwa  na mwanaume wa kibongo kwa sababu wengi  wao ni waongo  na  hawayajui  mapenzi...
 
Akiongea  na  mwandishi  wetu, mrembo  huyo  alidai  kuwa  umaarufu  wake  humpa  wakati  mgumu  sana  wa  kumtambua  mwanaume  mkweli  maana  wengi  humtamani  kimapenzi  kutokana  na  jina  lake ( ustaa  wake )

  “Sitaki kuzalishwa   wala  kuwa  na  uhusiano wa  kudumu  na mwanaume  toka  Tanzania  maana  wengi  wao ni tapeli  na  hata  ukiwakubali   huwa hawajui  kitu . ALIFUNGUKA.....
 
"Bora kwa nchi za wenzetu kuna  ndoa za mikataba  kiasi  kwamba  mtu  unakuwa  unajua kabisa nitakuwa na huyu   kaka  kwa muda fulani , ntazaa  naye au ni wa raha tu.
 
"Hiyo  inasaidia  sana  kwa  sababu   kama huyo  kaka  ni   MSHAMBA inakuwa  ni  rahisi  kwako  kumpiga  chini  na  kuangalia  ustaarabu  mwingine”..alisema Avana

MAMBO YA LADY GAGA JUKWAANI LAIV BILA NGUO.....AKITUMBUIZA



         
       
Huyu  ni  msanii Lady Gaga  aliyeamua  kutoa  burudani   akiwa  uchi  wa  mnyama  katika show ya G-A-Y huko London, Uingereza Ijumaa iliyopita.

Gaga (27) alipanda jukwaani akiwa amevalia vazi linalomfunika hadi miguu lakini wakati akiendelea kuperform ghafla alianza kusaula taratibu kutokea juu hatimaye kulishusha vazi lote na kubaki uchi..

DAH... NGUMI ZAPIGWA KATI YA WADADA BARABARANI ETI KISA BWANA WANAEMGOMBANIA


Wadada wawili Warembo wa Mitaa ya kawe waliamua kuzichapa kavu kavu bila maglovsi mbele za watu kwa eti mmoja akimtuhumu mwenzie kuwa anatoka na Boyfriend wake...Inasemekana hawa madada ni marafiki sana lakini leo yamewashinda baada ya kuchangia bwana mmoja ...

AJABU....MWIZI WA KUKU AVULIWA NGUO BAADA YA KUKAMATWA......AFUNGIWA NDANI YA TENGA NA WANANCHI TAYARI KWA KUCHOMWA MOTO



Huyu  ni  mkenya   aliyekuwa  ameiba  kuku.Wananchi  walipomnasa walimpa  kichapo  kikali  na  kisha  kumfungia  ndani  ya  tenga  la  kuku  kwa  ajili  ya  kumchoma  moto….

Wangali  katika  maandalizi  ya  kutafuta  petrol, polisi  waliwasili  eneo  la  tukio  na  kumuokoa  kwa  kumpeleka  kituoni
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DODOSO - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger