Home » » FUKWE ZAFUNGWA AFRIKA KUSINI KUFUATIA KUVAMIWA NA PAPA WEUPE WALIOKUWA WAKINYATIA MZOGA WA NYANGUMI.

FUKWE ZAFUNGWA AFRIKA KUSINI KUFUATIA KUVAMIWA NA PAPA WEUPE WALIOKUWA WAKINYATIA MZOGA WA NYANGUMI.

tangazo

 Wafanyakazi wa mamlaka ya Usalama wa baharini nchini Afrika Kusini wakiwa katika harakati za kusogeza mzoga wa Nyangumi nchi kavu kwa ajili ya kwenda kuzika.
Sehemu kubwa ya pwani ya Afrika Kusini imefungwa kufuatia mzoga wa nyangumi mwenye ukubwa wa mita 30 kusukumwa na maji pembezoni mwa fukwe na kuanza kushambuliwa na jamii ya papa weupe.
Mzoga wa nyangumi huyo umelazimika kuondolewa haraka ufukweni ulikokuwa ukielea, kwa kuwa ulikuwa ukifukuziwa na papa weupe kadhaa walio ugeuza kitoweo na kuhatarisha maisha ya watu.
Mamlaka husika zimechukua hatua ya kuuondoa mzoga huo lakini pia imefunga mtandao wa fukwe hizo kuanzia Muizenberg hadi Monwabisi kwa tahadhari.
Mzoga wa Nyangumi ukipimwa urefu.
 Mashine Maalum ya kubebea vitu vizito kama Makontena ikifanya kazi ya kusomba mzoga huo.
Jitihada za kumbeba Nyangumi huyo kwa kutumia mashine maalum za kubebea makontena zikiendelea.
Nyangumi akiwa tayari amepakiwa kwenye Lori.
Safari imeanza ya kumsafirisha Nyangumi huyo sehemu kunakohusika.

Tupe Maoni yako!

KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DODOSO - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger