Showing posts with label MISS TANZANIA. Show all posts
Showing posts with label MISS TANZANIA. Show all posts

JOKATE MWEGELO ATOKA NA "KIDOTI LOVING"

Mrembo, mtangazaji na mjasiriamali wa nchi Tanzania Jokate Mwegelo leo ameizundua rasmi kampuni yake ya Kidoti Loving katika hafla iliyofanyika Serena Hotel jijini Dar es Salaam.

Bidhaa za kwanza za Kidoti zilizoingia sokoni ni Nywele (weaving) ambazo amesema tayari zinapatikana katika soko la Kariakoo na maeneo mengine jijini Dar es Salaam ambapo baada ya muda mfupi zitaanza kupatikana mikoani.

Amesema kwa kuanzia kampuni yake imeanza kwa kutengeneza nywele za aina nane ambazo zinapatikama kwa bei ya kawaida ili kuwawezesha watanzania wengi kupendeza kwa gharama nafuu.

“Hizi nywele mabibi na mabwana zimefanyiwa utafiti kwa takriban mwaka mzima,” alisema Jokate.

“Ni nywele safi zenye ubora wa hali ya juu, hazifungamani, zipo katika mawimbi, rangi na style za kisasa, ni nyepesi, rahisi kusukia, laini, zinadumu kwa muda mrefu na muhimu kuliko yote zipatikana kwa bei nafuu sana.”

“Ni bidhaa ambazo naweza kusema confidently zinamfaa mwanamke wa kisasa.”

Jokate amesema utengenezaji wa nywele hizo ameusimamia mwenyewe na kwa msaada wa timu yake ya Kidoti.


Hizi ni baadhi ya picha za tukio hilo.
DSC_7943 (800x537) DSC_7944 (800x537) DSC_7945 (800x537) DSC_7946 (800x537)

 DSC_7942 (800x537)

 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DODOSO - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger