Showing posts with label BONGO FLEVA. Show all posts
Showing posts with label BONGO FLEVA. Show all posts

"BONGO FLEVA IMEFULIA"....MAD ICE



Msanii wa kimataifa kutoka Tanzania aishiye nchini Finland, Mad Ice amesema ladha ya Bongo Flava imebadilika kwa kiasi kikubwa kutokana na wasanii kutaka kucopy style za wasanii wa nchi zingine husasan Nigeria na Afrika Kusini.


“Jana nilikuwa na mtu mmoja anaitwa Man Razor tulikuwa kwenye interview radio, Dj Tass alipiga kwanja za nyuma ile miaka yetu tunaanza 2002/03 akapiga track zile zote, nikasema kweli muziki umebadilika sana, ladha imepotea, ile ladha ya Bongo Flava ya mwanzo ile, na nikajiuliza ni kwanini. 

Jamaa akaniambia ‘sikiliza vizuri kazi zinazofuata’, kuna flava ya kinaijeria, sijui South Africa sijui wapi, akaniambia ‘unajua tatizo ni kwamba vijana wakisikia wamehit P-Square naye anakambilia anakwenda kwa producer nitengenezee track kama ile,” Mad Ice

Amesema tatizo hilo linachangiwa pia na mashabiki ambao huzipenda nyimbo za wasanii wa Nigeria na hivyo kuwafanya wasanii wengi hasa wanaotegemea muziki kuiga style hizo ili kupata shows zaidi.

“Ni wachache walio na msimamo kwamba mimi natengeteza kazi mimi kama mimi, I don’t care mtu mwingine anafanya kitu gani.”

Mad Ice yupo nchini kwa siku kadhaa sasa na Jumamosi anatarajiwa kuwa na show visiwani Zanzibar.

TOP FLAVA WAJA NA REMIX YA BEAUTIFUL ONYINYE


Kundi la muziki la kizazi kipya lijulikanalo kama Top Flava lenye makazi yake Kigamboni jijini Dar es Salaam, limeachia video ya wimbo wake ambao ni remix ya hit ya P-Square waliomshirikisha Rick Rozay, ‘Beautiful Onyinye’.

Msemaji mkuu wa kundi hilo Tony Torch ameiambia Dodoso kuwa huo ni mwanzo tu na wanawaomba mashabiki wawwpokee kazi zao pamoja na hii ya wimbo walioupa jina la Rudi Home.

‘Pia kuna nyimbo tumeifanya na Chege ‘Uchumi Unayumba’ ikiwa tayari mtaipata hapa hapa ,”alisema.

JOKATE MWEGELO ATOKA NA "KIDOTI LOVING"

Mrembo, mtangazaji na mjasiriamali wa nchi Tanzania Jokate Mwegelo leo ameizundua rasmi kampuni yake ya Kidoti Loving katika hafla iliyofanyika Serena Hotel jijini Dar es Salaam.

Bidhaa za kwanza za Kidoti zilizoingia sokoni ni Nywele (weaving) ambazo amesema tayari zinapatikana katika soko la Kariakoo na maeneo mengine jijini Dar es Salaam ambapo baada ya muda mfupi zitaanza kupatikana mikoani.

Amesema kwa kuanzia kampuni yake imeanza kwa kutengeneza nywele za aina nane ambazo zinapatikama kwa bei ya kawaida ili kuwawezesha watanzania wengi kupendeza kwa gharama nafuu.

“Hizi nywele mabibi na mabwana zimefanyiwa utafiti kwa takriban mwaka mzima,” alisema Jokate.

“Ni nywele safi zenye ubora wa hali ya juu, hazifungamani, zipo katika mawimbi, rangi na style za kisasa, ni nyepesi, rahisi kusukia, laini, zinadumu kwa muda mrefu na muhimu kuliko yote zipatikana kwa bei nafuu sana.”

“Ni bidhaa ambazo naweza kusema confidently zinamfaa mwanamke wa kisasa.”

Jokate amesema utengenezaji wa nywele hizo ameusimamia mwenyewe na kwa msaada wa timu yake ya Kidoti.


Hizi ni baadhi ya picha za tukio hilo.
DSC_7943 (800x537) DSC_7944 (800x537) DSC_7945 (800x537) DSC_7946 (800x537)

 DSC_7942 (800x537)

MAUNO YA SHILOLE YAWADATISHA ASKARI

WAKATI SHILOLE ANAPERFORM FIESTA 2012, ALIWADATISHA MPAKA ASKARI NA MABAUNSA......






 Nilichokigundua ni kwamba askari pamoja na kikosi cha mabaunsa waliokua mbele kabisa kuhakikisha usalama unakuepo, wote waligeuka kuangalia stage baada ya Shilole na dancers wake kudatisha kwa jinsi walivyokua wanacheza, yani jamaa walijiachia kabisa.

 

JANETH AMSHITAKI LINEX KWA KUMTANDIKA KOFI


Hiki kinaweza kuwa kituko cha mwaka kwenye muziki wa Bongo Flava. Mrembo aliyeigiza kwenye video ya Linex Aifola, ameamua kumfungulia RB msanii huyo baada ya kumpiga kibao cha kweli kwenye video hiyo.

Katika video hiyo Linex anaonekana akiwa amekaa kwenye kochi na kuanza kukagua simu ya mchumba wake Aifola ambaye humo ameigiza Janeth Bundala na ndipo alipogundua kuna meseji za kimapenzi anazotumiwa na mwanaume mwingine kiasi cha kuchukia na kumpiga kofi kali la shavuni.


“hahhahahahhahaha frm no where eti janeti aka aifola kanipigia leo kaniambia kanichukulia R B kwa kofi nililompiga wakati tunaigiza hahah kama kachelewa hv,” aliandika Linex jana kupitia Facebook.

“Sijajua alikua anatania but ndo kitu alichoniambia muda si mrefu nimekia nacheka tu. Nimemsikia live radion anataka kulipwa aseeee kumbe anamaanisha. Nimeshaongea nae na kesho ndo nakutana nae rasmi ntajua anatakaje na ntamalizana nae.”

Unahisi Janeth yuko sahihi kumshtaki Linex kwa kumpiga kibao cha kweli kwenye uigizaji wa video? Na je amechelewa kama Linex anavyosema?

“WATU WALITAKA KUUA MUZIKI WA HIP HOP ILI KUWAPA NAFASI WAIMBA MAPENZI” – AFANDE SELE


WAKATI muziki Hip Hop ukizidi kushika kasi, msanii kutoka mji kasoro bahari Morogoro, Afande Sele au unaweza kumuita King of Rhymes, amesema kuwa kuna baadhi ya watu ambao wanajiita wadau wa muziki walitaka kuua muziki wa Hip Hop ili kuwapa nafasi wabana pua lakini walishindwa kutokana na halikati zao na hakuna kilichofanyika.

Msanii huyo aliwafumbua macho mashabiki wao kuwa muziki huo unaozungumza maisha halisi ya mwanadamu kunanbaadhi ya watangazaji na wadau ambao lengo lao lilikuwa ni kuuzimisha muziki huo baada ya kuona ujumbe unaopatikana una lengo la kuelemisha zaidi jamii na si wale wanaoimba ujumbe wa mapenzi tu.


Alidai kuwa muziki wa Hip Hop haujapewa nafasi kama ilivyo kwa wabana pua na ndiyo maana hata vijana wengi wanashindwa kujua nchi inakwenda wapi kutokana na nyimbo za mapenzi kushika kasi kila siku.


“Unajua kuna watu wanajifanya wadau wa muziki wakati lengo lao ni kuua muziki wa Hip Hop na kuwapa nafasi waimba mapenzi lakini hata hivyo bado muziki wetu utazidi kuwa juu kutokana na ujumbe unatolea ndani ni ule wa kudumu miaka mia lakini mapenzi leo na kesho wimbo hauna tena maana,”
alisema Afande.

RECHO AWAPONDA WASANII WA BONGO FLEVA NA KUDAI KUWA NI WEZI


STAA wa filamu Bongo, Recho Haule ‘Recho’ amebwatuka na kuwaita wezi wasanii wa Bongo Fleva akidai wanawaibia mashabiki kwa kucheza CD katika shoo zao.


Akizungumza na Mdodosaji wetu juzikati jijini Dar, Recho anayeng’ara kupitia Bongo Movies, amesema kuwapigia CD mashabiki ni sawa na mwizi anayeiba bidhaa za watu.


“Yaani hawa wasanii nathubutu kuwaita wezi kwa sababu kupitia muziki wanaoufanya wanajiingizia pesa bila kuwa hata na kipaji cha uimbaji na upigaji ala zaidi ya kufuatisha CD jukwaani,”
alisema Recho.

AIBU: DIAMOND AAMUA KUYAANIKA MAKALIO YAKE


Kwa wale walioondoka mapema kwenye show ya Fiesta usiku wa kuamkia Jumapili baada tu ya Rick Ross kumaliza performance yake, walikosa kujionea kituko kilichofanywa na Diamond Platnumz. Ama wengine wamekuja tu kuona picha zilizosambaa kwenye internet.

 Akiwa stage na madancer wake wakati show imepamba moto, Diamond aliamua kuvua na kuonesha boxer yake nyeupe kama ishara kuwa yeye na madansa wake ni ‘wasafi’ kiasi cha kutoogopa kuionesha hadharani.

Bahati mbaya watanzania wamemuelewa tofauti. Kitendo hicho kimewakera wengi. 

Kwa mujibu wa maoni tuliyoyapata kupitia ukurasa wetu wa Facebook baada ya jana kuweka picha hiyo, wengi wameitafsiri picha hiyo kama ishara ya ‘ushoga’ na huku wengine wakienda mbali zaidi na kuibua tena mada ya ufreemason. Haya ni baadhi ya maoni.

“Wanaonyesha kuwa na mapepo hao maana walianza na kuvua magoti hadi mashati wakabakiza suruali , sasa wamebakiza boxer unadhani wakishatoa boxer watabakiza nini, huo ni ushirikina na muda si mrefu watahumbuka hao maana naona ule mwisho wao umeshafika; hizo ni akili ama matope…wana akili ama matahairaaaaa1.”

“Ndio maana wazee wetu hawaupend kuusikiliza huu muzk munaoita bongo flava. Uchafu kama huu mnafanya mbele za watu au umaarufu unatafutwa kwa kila njia,basi huyo tanzanite awe john elton wa bongo.”

“Lbd alielewa tofauti,alpockia MUONEKANO MPYA BURUDAN ILEILE ndani ya fiesta!!nd mana akafanya hcho k2ko lkn pia mayb woz search and luking fo huzband! nadhan co rdhk nyota uyu.teh teh teh shame upon hiz unimpressive kboxa.”

LADY JAYDEE AJIPANGA KUTOKA NA KIPINDI CHA TV MWEZI HUU



Baada ya kufanya vizuri kwenye biashara zake hasa ile inayoendelea Nyumbani Lounge, mwanadada Judith Mbibo aka Lady Jaydee, amesema katikati ya mwezi huu ataanza kuonekana kwenye kipindi chake cha TV.

Hata hivyo mwanamuziki huyo hajasema jina la kipindi hicho na wapi kitakuwa kikionekana na amewataka mashabiki wake wabashiri.


“Habarini za Leo, Nimerudi tena. Kutoa jibu la Project yangu mpya… NI KIPINDI CHA TV, ila nahitaji washindi zadi, Unaweza kubahatisha ni Kituo gani cha TV kitakachorusha kipindi hicho na Kipindi kitaitwaje????? washindi 5 watashirikishwa katika hafla ya ufunguzi wa kipindi hicho October 2012… Kazi ni kwenu,”ameandika leo kupitia ukurasa wake wa Facebook.

Amesema washindi watatu watakaopatia watapata CD ALBUM YA.5, Complimentary za kuingia MACHOZI BAND miezi 3 pamoja na kula lunch au dinner pamoja na yeye siku ya utambulisho wa project hiyo.
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DODOSO - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger