Sababu sita kuu na za msingi zinazojibu swali la kwanini siku hizi wanaume wengi hawapendi kuoa?,,,,,,

 
Kumekuwa na maswali yasiyo na majibu miongoni mwa jamii kwamba imekuaje vijana wa kiume wamekuwa ni waongo sana hasa linapokuja swala la kuoa? Kwa kadiri siku zinavyozidi kwenda ndivyo ambavyo idadi ya wanaume wanaoogopa kuoa inazidi kuongezeka. Utakuta wapenzi wanaambiana kwamba wanapendana na kuahidiana kuwa wataoana, lakini kitakachotokea baada ya hapo ni mwanaume kuanza kupiga chenga kwa visingizio lukuki.

Kwa nini hali hiyo hutokea?

Ukweli ni kwamba hakuna jibu la moja kwa moja juu ya tatizo hilo, lakini yapo mambo ambayo yanaweza kutupa angalau tafakuri. Nitajaribu kudadavua baadhi ya sababu zinazowafanya wanaume siku hizi kukwepa kuingia katika taasisi ya ndoa:

1 Ukosefu wa mtu wa kumchukulia kama mfano: Hapa nawazungumzia wale watoto wa kiume waliolelewa malezi ya upande mmoja yaani walilelewa na mama peke yao. Sina maana ya kudharau au kutweza malezi ya mama, la hasha, lakini ni vyema mkafahamu kwamba kuwa na baba asiye na malezi mazuri si sawa na kutokuwa na baba. Na ndio maana nikasema ukosefu wa mtu wa kumchukulia kama mfano. Achilia mbali aina ya malezi atakayoyapata kwa familia yawe mazuri au mabaya lakini lazima kutakuwa na tabia za kiume zitakazoakisi malezi ya mtoto wa kiume katika familia husika. Watoto waliolelewa na mama peke yao kuna kitu huwa wanakosa, kwani wanakuwa hawana mtu wa kumchukulia kama mfano kwa upande wa jinsia ya kiume na hapo ndipo hujikuta wakijifunza wenyewe namna ya kuongea na kutenda kama wanaume kwa sababu katika makuzi yao hawakupata fursa ya kuwa karibu na baba zao. Kwa kuwa siku hizi kuna kundi kubwa la kina mama ambao wamejikuta wakiachiwa mzigo wa malezi ya watoto, baada ya aidha kuachwa na waume zao au kuzalishwa na kutelekezwa (Single mothers), na hapo ndipo tunaposhuhudia mtoto wa kiume anapokua kwa umri na kimo huku akiwa hana mtu wa kumuangalia kama mfano wa mume anavyotakiwa kuwa katika familia zaidi ya kujifunza mambo hayo kupitia katika TV, senema au miziki. Wanaume waliopitia malezi ya aina hii huchelewa sana kuoa kwani huyaangalia maisha ya ndoa kwa namna ya kujaribu na ndipo hapo wengi huishia kuishi kinyumba na wanawake kwa ajili ya kutaka kujifunza namna ya maisha ya ndoa yanavyotakiwa kuwa na ndio sababu huchukua muda mrefu kufanya maamuzi. Na mara nyingi huishia kubadilisha wanawake kutokana na kutokuwa na uhakika wa kile wanachokitafuta.

2 Mgogoro wa kiuchumi: Kuna kundi kubwa la vijana siku hizi hawana ajira au hawana uhakika na kipato. Ukweli ni kwamba hakuna mwanaume atakayependa kujiingiza kwenye ndoa wakati hana kazi au hana uhakika na kipato chake. Na hiyo ni kutokana na wanawake wengi siku hizi kuonekana kujali zaidi wanaume wenye uhakika na kipato. Hii misemo ya wanawake ya kebehi dhidi ya wanaume wasio na ajira au kipato, kama vile “mwanaume suruale” ina mchango mkubwa sana katika kuwafanya wanaume kukwepa kuoa iwapo hawana ajira au hawana uhakika na kipato chao.


3 Wanawake wengi kuwa na kiwango cha elimu ya juu: Siku hizi wanawake wengi wameibuka katika kutafuta elimu ya juu kwa juhudi kubwa. Idadi ya wanawake wanaojiunga na vyuo vikuu ni wengi tofauti na ilivyokuwa zamani. Na hiyo ni kutokana na wazazi wengi kubadili mtazamo wao juu ya mtoto wa kike. Zamani mtoto wa kike alichukuliwa kama kitega uchumi. Kwa maeneo ya vijijini na katika familia masikini, watoto wa kike walikuwa wanatazamwa kama, ‘biashara ya kesho’ ambapo watauzwa kwa njia ya mahari. Kwa hiyo thamani yao ilikuwa ni kuolewa, ni ile ya kibidhaa na sio kibinadamu. Lakini tofauti na zamani siku hizi hata kule vijijini kumekuwa na mwamko mkubwa sana wa kumsomesha mtoto wa kike hadi elimu ya juu. Kutokana na mwamko huo wanawake wengi wamejikuta wakiona elimu kama kimbilio pekee la kuepukana na mfumo dume. Mwanamke gani atakubali kunyanyaswa na mwanaume akiwa na elimu yake na labda pia akiwa na kazi yake yenye mshahara na marupurupu ya kutosha, naamini watakuwa ni wachache sana ambao hawajiamini au waliathiriwa na malezi. Kwa upande wa wanaume nao, wamejikuta wakiwaogopa wanawake hawa wenye elimu ya juu kwa hofu ya kuzidiwa kipato na labda kukosa sauti kama mwanaume na hiyo inatokana na ego tu. 

4 Wanaume huwaona wanawake kama tishio wanapokuwa na mafanikio makubwa kifedha: Inaweza kutokea mwanaume anaweza kuwa na uhusiano na mwanamke ambaye labda tu nisema ni mbangaizaji. Wakati huo anaweza kuahidi kufunga ndoa na mwanamke huyo, lakini iwapo itatokea mwanamke huyo akapata mafanikio kibiashara na kuinuka kifedha. Kama mwanamke asipokuwa makini anaweza kusababisha mwanaume huyo akaingia mitini. Sababu kubwa hapo inaweza kuwa ni hofu ya kuogopa kuongozwa na mwanamke. Kumbuka kwamba mfumo dume bado umetawala vichwani mwa wanaume wengi kutokana na malezi. Mwanaume asiyejiamini ni vigumu sana kwake kuoa mwanamke aliyemzidi kipato. Kwa sababu akifanyiwa jambo dogo tu, inakuwa kama ametoneshwa. Atahisi kutaka kutawaliwa na mwanamke huyo. Jambo ambalo wanawake wanatakiwa kulifahamu ni kwamba kila mwanaume anataka kutambuliwa na kuheshimiwa kama shujaa kabla ya kumfuata msichana. Iwapo utakuwa umesimama iwe ni kifedha au kielimu pale unapotafuta kupata mwenza, inabidi ujishushe sana la sivyo utadoda.


5 Wanaume wengi siku hizi wana hofu ya majukumu, hasa ya kulea watoto: Kutokana na malezi yao au kile wanachokijua kuhusu watoto, baadhi ya vijana huamini kwamba, kulea watoto ni jambo gumu sana. Lakini wengine wanaamini kwamba, hata mke anapaswa kulelewa kama ilivyo kwa mtoto. Hivyo wanaamua kutafuta kwanza uwezo ambao haupatikani kiurahisi. Kuna wengine, ambao wamefundishwa au kuelekezwa na mila na desturi zao kwamba, kabla hawajaoa, ni lazima wawe na nyumba kwanza, tena kwao. Kwa hiyo, hawa hadi waje wapate uwezo wa fedha wanakuwa wameshachelewa.

6 Kuna baadhi ya wanaume, maisha bila ya ndoa wanayaona kuwa ndiyo bora kuliko yale ya ndoa: Kuna baadhi ya wanawake hujirahisisha sana kwa wanaume. Siku hizi ni jambo la kawaida sana kukuta mwanaume anaishi na mwanamke bila ndoa, wenyewe wanaita Trial Marriage. Na hapo ndipo unapokuta wanaume hawaoni tena umuhimu wa kuoa. Sasa kama mwanamke anaweza tu kuishi na mwanaume bila ya ndoa na mwanaume huyo akapata huduma zote kutoka kwa mwanamke huyo, unadhani ni kitu gani kitamvuta kufunga ndoa. Jambo lingine ni ile dhana kwamba maana ya ndoa ni tendo la ndoa. Siku hizi wanaume wengi wamejikuta wakiwa hawahitaji tena kuoa kwa sababu tendo hilo linapatikana kiurahisi tofauti na zamani. Siku hizi inawezekana kabisa kumtongoza binti leo na kupata tendo siku hiyo hiyo….. Na hapa siwazungumzii makahaba. Nawazungumzia mabinti zetu ambao wengine ukiwaona ni watu wa kuheshimiwa ukiwaangalia kwa nje lakini kwa ndani hawana lolote, vijana wa siku hizi wenyewe huwaita maharage ya Mbeya.

Kuna sababu nyingi zinazotajwa kusababisha wanaume siku hizi kujivuta sana katika kufanya maamuzi ya kutafuta mwenza. Lakini hizo chache nilizozitaja zina mchango mkubwa.

EWE MWANAMKE UJUE UKWELI LEO....... SIO KILA DALILI YA MWANAMKE KUPENDA NI YA KWELI

 

Siyo kila dalili ya mwanaume kupenda ni ya kweli…!


Kuna wakati ambapo, wanawake wanajikuta wakikabiliwa na swali la, je, mwanaume huyu ananipenda kweli? Hii hutokea pale anapokutana na mwanaume ambaye, huenda amevutiwa naye. Pengine mwanaume naye anaweza kuonesha kuvutiwa na mwanamke huyo.

Kwa hiyo, mwanamke hujiuliza kama akubali ombi la mwanaume huyo na kukubali kuzungumza naye au kuanzisha naye uhusiano, kama mwanaume atakuwa amezungumza naye kuhusu jambo hilo. ni kweli kwamba, kuna ugumu kwa mwanamke kujua hasa ni kwa namna gani anaweza kujua kwamba, huyo mwanaume amempenda kweli au hapana.

Kuna vitu vingi ambavyo vinaweza kuwa ni dalili ya kumpenda mwanamke, lakini wakati huo huo vinaweza visiwe.

1. Hebu tuchukulie kwamba, mwanaume ameonesha kuwa na tabia tunazoziita nzuri. Labda amekumbuka kirahisi jina la mwanamke, ameonesha kuwa msikilizaji mzuri, ameonesha kuwa anajali kuhusu kinachosemwa na mwanamke, na amekuwa anamuuliza maswali kwa dhati na utulivu. Hapa mwanamke anaweza kuamini kwamba, huyu mwanaume anampenda. Lakini ukweli huenda ukawa ni kinyume chake. Inawezekana huyo mwanaume ni muungwana tu, na anaonesha tabia hizo kutokana na uungwana wake na siyo kutokana na kumpenda kimapenzi mwanamke.

2. Kuna watu ambao wana upendo, wamekomaa kihisia na wanajua kuhusiana vizuri na watu. Hii haina maana kwamba, kumwonesha mtu tabia hizo, kuna maana ya kumpenda au kumpenda sana mwanamke. Dalili hizi ni nzuri na inawezekana zikawa zinaonesha mwanaume kumpenda mwanamke, lakini mwanamke asilichukulie jambo hilo kwa namna hiyo.

3. Mwanaume anaweza kuonesha kuwa na udadisi kuhusu mwanamke kwa maana kwamba, kutaka kujua mambo yake, kumfuatilia au kuulizauliza kuhusu habari za mwanamke. Hii haina maana kwamba mwanaume amempenda kimapenzi. Inawezekana mwanaume akawa amevutiwa kimapenzi na mwanamke ndiyo maana akaonesha tabia hizo, lakini siyo lazima iwe hivyo. Kumbuka kwamba, mwanaume anaweza kuvutiwa na mazungumzo ya mwanamke, akavutiwa hata na namna alivyo usoni, hivyo akapenda kuzungumza naye lakini siyo kwa sababu anampenda.

4. Kuna wanaume ambao wana wake au wapenzi, lakini wanajisikia vizuri kusikiliza wanawake wengine au kujua tu habari za wanawake wengine, bila kuwa na haja ya kuanzisha uhusiano nao. Mwanaume anapompa mwanamke ‘ofa’ hasa ya chakula cha mchana au usiku, ni dalili ya wazi ya kuvutiwa naye. Hapa kuna uhakika mkubwa zaidi, labda tu kama mazungumzo yanayotajwa kufanywa wakati huo wa chakula yanafahamika, na ni ya shughuli maalum. Kwa hiyo ‘ofa’ ya chakula ni dalili nzuri na yenye uhakika. Lakini kuna jambo ambalo ni muhimu kwa mwanamke kulifahamu katika hali kama hii. Kuna wakati mwanaume kumpa ‘ofa’ mwanamke kwa chakula cha mchana au jioni, kunaweza kusiwe na maana ya moja kwa moja kwamba, uhusiano utaundwa. Inawezekana katika kutoka outing huko, mwanaume akaghairi. Kwa wengine huchukua muda hadi kuamua kuhusu kuunda uhusiano au hapana.

5. Hata mwanaume kuamua kumpeleka mwanamke kwa familia yao na kumtambulisha kama rafiki yake, ni hatua yenye kuonesha kwamba, mwanaume ameamua kumpenda mwanamke huyo. Lakini wakati mwingine hii inaweza ikawa ni janja yake kutaka tu kumthibitishia mwanamke ili amhadae vizuri, na wala hakuna maana ya uhusiano wa kudumu.

6. Kuzungumza kwa pamoja kuhusu masuala ya baadaye ya kiuhusiano, kama vile, idadi ya watoto na mambo mengine ambayo mara nyingi huzungumzwa na watu ambao tayari wako kwenye uhusiano ni dalili ya mwanaume kuvutiwa mwanamke. Lakini tatizo la jambo hili ni kwamba, kuzungumza masuala ya baadaye inaweza kuwa ni njia ya mwanaume kutaka kujisikia au kujua jinsi inavyokuwa katika mambo hayo. Inaweza kuwa pia ni njia yake ya kutaka kupima wanawake wanavyosema kuhusu masuala hayo. Lakini inaweza ikawa mwanaume huyo anatafuta kujua misimamo ya mwanamke huyo ili hatimaye afanye uamuzi. Kwa hiyo, bado haioneshi kuwa amevutiwa na kuamua tayari.

Mara nyingi wanawake hudanganywa na dalili fulani zinazooneshwa na wanaume wakati wanapoanza kuzoeana nao. Dalili hizi huwafanya kuamini kwamba, wanaume hao wamewapenda tayari, wakati siyo kweli. Kwa kuangalia baadhi ya dalili hizo kama nilivyozitaja, mwanamke anaweza kuwa makini wakati anapoanzisha uhusiano, ili asikurupuke na kujikuta amedanganyika. Ni kweli, kuna wakati ni dalili zinasema kweli, lakini kuna wakai zinadanganya kuhusu kupenda au kupendwa.

TANGAZO LA KIFO BUNGENI DODOMA

Marehemu Anselm L. Mrema enzi za uhai wake.
Katibu wa Bunge, anasikitika kuwataarifu wananchi kuhusu kifo cha mtumishi wa Ofisi ya Bunge katika idara ya shughuli za Bunge, Mkurugenzi Msaidizi Ndg. Anselm L. Mrema kilichotokea jana usiku tarehe 10.11.2013 katika Hospitali ya Mkoa, Dodoma.
Ofisi inaendelea na taratibu za mazishi kwa kushirikiana na familia ya marehemu, tutaendelea kuwapa taarifa zaidi kutokana na msiba huo. Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe. Amen!
 Chanzo: Michuzi…

Msaniii wa taarabu Nyawana Fundikira afariki dunia.

Msanii wa taarab nchini anayejulikana kwa jina la Nyawana Fundikira aliyetamba na wimbo wa 'Nipo Kamili Nimejipanga', amefariki dunia mchana huu kwa ugonjwa wa malaria.
Nyawana amefariki akiwa kwake maeneo ya Mwananyamala B na mwili wake sasa umepelekwa kuhifadhiwa Hospitali ya Mwananyamala, Dar.

daaah..... MAUTI IPO NJIANI INAMVIZIA MTU HUYU..... KWA MUJIBU WA DACTARI


Doctor Amesema kijana Huyu Atafariki Baada Ya 

muda mfupi Kwa Sababu damu imevujia ndani ya 

Ubongo Wake Na Amesema Hawana Uwakika Kama 

Wataweza Kumnusuru.


Lakini Mungu Pekee ndio anauwezo Wa Kuongea 


Juu Ya Huyu kijana Na Anaweza Kumponyesha, 

Eeeh Mungu Twaomba Umponyeshe Huyu kijana 

Na 

 Uweze Kushinda Maneno Ya Doctor. 
 

 Kama Unaamini Mungu Anaweza Kumponyesha 
 
Huyu kijana Comment "Amen" Kwa Huyu kijana 

james Na "Share" Kwa Maombi Zaidi ya watanzania 

wenzake

HAYA SASAAA,,, VIASHIRIA VINAVYOMUONYESHA MPENZI MPYA KUWA WEWE NI KIN'GAN'GANIZA KWAKE....

Mwanamke: Dalili zitakazomfanya mpenzi mpya akuone wewe ni king’ang’anizi…!

Hizi ni miongoni mwa sababu ambazo wanaume wengi huchomoa mapema kwa wapenzi wao wapya kabla uhusiano haujashika kasi. Kuna wakati wanawake hukosea na kuvuka mipaka mwanzoni tu mwa uhusiano. Anamganda mwanaume haraka sana au anaonesha dalili zote za kujipendekeza kupita kiasi. Lakini jambo ambalo wanawake wengi hawalijui ni kwamba, wanaume wako makini sana kuwakwepa wanawake ving’ang’anizi……..

Nitadadavua baadhi ya vijitabia vya wanawake vinavyowafanya wanaume wawaone kama ni ving’ang’anizi…..
1. Unataka kuwa naye muda mwingi kuliko kawaida… Ni vizuri kwa wapenzi wapya kupata fursa ya kuwa pamoja peke yao, lakini kama unakataa kuwa na mtoko, kuhudhuria sherehe au kukutana na marafiki na kulazimisha kuwa pamoja peke yenu mahali fulani pa faragha, basi hapo ni lazima mwanaume atadhani kwamba unataka akupe umuhimu wa pekee muda wote. Unaweza kukuta mwanamke anakuwa king’ang’anizi kiasi kwamba hana muda na marafiki zake au watu wengine isipokuwa mpenzi wake. Anakuwa kama mzigo, muda wote yuko nyuma ya mwanaume kila anapokwenda…. Hapa ni lazima mwanaume atatemana na wewe kungali mapema. Hakuna mwanaume anayeweza kujenga mahusiano na mwanamke wa aina hii, watakukimbia kila siku.

2. Unampangia mwanaume kila kitu… Unampangia aina ya mavazi ya kuvaa, unaanza kuboresha mazingira ya nyumbani kwake haraka sana kwa kununua vitu mbalimbali vya nyumbani kwake bila kushauriana naye. Hiyo ni dalili kwamba una matarajio makubwa kwake, jambo ambalo kwake yeye bado halijamuingia akilini. Hapa mwanaume ambaye huyachukulia mambo kwa tahadhari, hukuona kuwa wewe ni king’ang’anizi na unataka kukita mizizi kwake wakati bado anachunguza uhusiano wenu ili kujua iwapo utakuwa kama vile anavyotarajia yeye… Kumbuka kwamba kila mtu ana sifa azitakazo pale anapochagua mwenza, na ni vigumu kumjua mtu kwa muda mfupi. Kunahitajika muda wa kutosha mtu kumjua mwenzake vizuri linapokuja swala la mahusianao. 


3. Unatumia muda mwingi zaidi kukaa kwake…. Unalala kwa mpenzi wako, na asubuhi mwanaume huyo anaondoka kwenda kwenye shughuli zake, na wewe unabaki labda ukidai unamsaidia usafi kidogo. Lakini anaporudi jioni anakukuta bado uko hapo nyumbani kwake ukiwa umejipumzisha. Inawezekana ukawa umeandaa chakula cha usiku tayari na pia huenda ukawa umebeba nguo za kubadilisha kwenye mkoba wako pamoja na vipodozi ukiwa umejiandaa kulala tena hapo kwake. Huonyeshi dalili za kuondoka hapo kwake zaidi ya kwenda kwako au kwenu na kubadilisha nguo na kuchukua viti vichache utakavyovihitaji utakapokuwa hapo kwake, lakini unapanga hayo yote bila kumshirikisha zaidi ya kukuona tu ukimganda kama luba. Huonyeshi kuwa na maisha yako kama wewe, zaidi ya kujipachika kwake……


4. Unajenga urafiki na mama yake haraka sana…… Baada ya kukutambulisha kwa mama yake na kubadilishana namba za simu au labda na email, unaanza kujenga ukaribu na mama yake kupita kiasi. Wanawake wengi hudhani kwamba, iwapo watajenga urafiki na mama wakwe watarajiwa, basi itakuwa rahisi kwao kumnasa mwanaume huyo, maana huamini kwamba watoto wa kiume hawawezi kwenda kinyume na mama zao linapokuja swala la kuchagua mwenza. Kwa kawaida wanaume humuona mwanamke anayejipendekeza kwa mama yake kama vile anataka kulazimisha uhusiano au ndoa, hivyo humchukulia kama ni king’ang’anizi.




5. Unampigia simu na kumuuliza kama yuko wapi….. Unapompigia simu badala ya kumjulia hali unakuwa na maswali ya kipolisi.. ‘Uko wapi?’ ‘Unafanya nini? Maswali ya aina hiyo mwanaume huyachukulia kama ya kimtego na hawafurahishwi nayo. Wanawake wengi huamini kwamba wanaume huwa hawasemi ukweli kuhusu mahali walipo pale wanapoulizwa na wenzi wao. Jambo hilo linaweza kuwa kweli au lisiwe kweli. Inawezekana kuwa kweli kwa sababu labda ya wanaume kukwepa maswali mengi. Mara nyingi wanawake hawaridhiki na jibu moja. Mfano ni jioni ndio ametoka kazini, lakini nakapitia mahali fulani kukutana na rafiki yake, inawezekana ikawa ni kwenye mghahawa au kwenye baa. Kama mwanamke akipiga simu na mwanaume akamwambai yuko kwenye baa na rafiki yake, yatafuata maswali lukuki. Hakuna mwanaume anayependa kuulizwa maswali mengi kama vile anatuhumiwa. Na ndio sababu wanaume wengi wanakwepe kusema mahali walipo. Kwa hiyo ili kuepuka maswali anaweza kujibu kwa kifupi tu kwamba yuko kwenye kikao kazini na hatakuwa hewani, ili apate nafasi ya kuzima simu japo kwa muda. Mwanaume humuona mwanamke mwenye udadisi wa aina hiyo kama king’ang’anizi. 


6. Unakuwa na chuki na wanawake wenzako… Pale ambapo mwenzi wako anapomtaja mwanamke fulani, inaweza kuwa ni mfanyakazi mwenzake, mke wa kaka yake au mtu wanayeshirikiana kibiashara, unaonyesha kisirani cha waziwazi kwamba unakerwa na ukaribu wake na wanawake wengine. Tabia hii inaashiria kwamba wewe unapenda kumiliki na wanaume wengi huwa hawapendi wanawake wenye vijitabia vya kupenda kumiliki. Hapo ni lazima utaonekana kuwa wewe ni king’ang’anizi na uhusiano wenu utavunjika mapema…..

7. Unakubali kila analosema au kila anachokifanya….Kuna kitu kinaitwa ‘uhusiano wa kinyonga.’ Hapa mwanamke anajibadili kupita kiasi ili afanane na mwenzi wake. Unakuta mwanamke anakubali kila kitu anachokiamini mwenzi wake bila kuhoji. Anapoteza utambulisho wake na kujipachika utambulisho wa mwenzi wake. Mwanaume akikuona uko hivyo, atakukimbia, atajua wewe ni king’ang’anizi
8. Unawazungumzia mabwana ulioachana nao kila wakati…Kama una kawaida ya kumzungumzia mwanaume uliyeachana naye mara kwa mara uwapo na mpenzi wako mpya, ina maana kwamba bado hujaachana na jakamoyo la kuachwa. Hakuna mwanaume anayependa kusikia kuhusu mahusiano yako ya nyuma, kwa sababu hayamuhusu. Kama ukiwa unapenda kumzungumzia mpenzi wako wa zamani kila uwapo na mpenzi wako mpya, jua kwamba na yeye pia utampoteza kwa sababu atakuona kuwa wewe ni dhaifu na king’ang’anizi na ndio maana umeshindwa kusimama kama wewe, na badala yake unawaza kuhusu mtu uliyeachana naye pamoja na kwamba uko naye. Sio kwamba ni vibaya kumzungumzia mpenzi mliyeachana, lakini ni vyema kama utamzungumzia pale ambapo kuna ulazima sana wa kufanya hivyo, labda kuna jambo ambalo limamhusu ambalo mnajadili, na ikakulazimu kumtaja…..

EXTRA BOGO YAWAPA UTAMU MASHABIKI WAKE DAR LIVE.....

    Wanenguaji wa Extra Bongo wakiwa kazini ndani ya Dar Live.
  Kiongozi wa bendi hiyo, Ally Choki, akiimba.
    
…Ally choki…
    Wanenguaji wa Extra Bongo wakiwa kazini ndani ya Dar Live.
  Kiongozi wa bendi hiyo, Ally Choki, akiimba.
   
 …Ally choki akimpiga tafu ya kunengua mnenguaji wake.
  Kiongozi wa wanenguaji, Super Nyamwela (katikati) akinengua.  
   Rapa wa bendi hiyo, Saigon, akionyesha umahiri wake wa kurap.
BENDI ya muziki wa dansi ya Extra Bongo ya jijini Dar es Salaam jana iliwapagawisha mashabiki waliofurika katika Uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar es Salaam

UCHAFU,,,, MCHUMBA WA MTU AFUMANIWA NA MSANII MAKABURINI

Na Issa Mnally

MREMBO aliyetajwa kwa jina moja la Ema aliyedai kuwa ni mchumba wa jamaa aliyemtaja kwa jina la Amri au Mdudu amefumaniwa laivu akisaliti penzi na mwanaume mwingine.
Mchumba wa mtu akipewa kichapo baada ya kufumaniwa.
Tukio hilo la aina yake lilijiri kwenye Makaburi ya Buguruni, Dar, mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya kuwekewa mtego.
TAARIFA KWA OFM

Wakati makachero wa Oparesheni Fichua Maovu wakiwa kwenye ‘patroo’ walipokea taarifa kutoka kwa chanzo chake…


MREMBO aliyetajwa kwa jina moja la Ema aliyedai kuwa ni mchumba wa jamaa aliyemtaja kwa jina la Amri au Mdudu amefumaniwa laivu akisaliti penzi na mwanaume mwingine.
Mchumba wa mtu akipewa kichapo baada ya kufumaniwa.
Tukio hilo la aina yake lilijiri kwenye Makaburi ya Buguruni, Dar, mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya kuwekewa mtego.

TAARIFA KWA OFM
Wakati makachero wa Oparesheni Fichua Maovu wakiwa kwenye ‘patroo’ walipokea taarifa kutoka kwa chanzo chake ambacho kiliomba wafike katika makaburi hayo ambapo kulikuwa na fumanizi.
OFM: Fumanizi la aina gani? Isije ikawa ni wanandoa tukaingia chaka.
Watuhumiwa baada ya kutolewa kwenye teksi walimokuwa wanafanya yao.
Chanzo: Hawa bado ni wachumba tu. Jamaa alikuwa anamfuatilia mchumba’ke amemnasa na jamaa kwenye gari wakifanya mapenzi sasa kuna timbwili zito.
 
OFM: Una uhakika na unachokisema?
Chanzo: Kama hamtaki acheni (akakata simu).

OFM KAZINI
Kwa kuwa OFM haipuuzii habari, ilimteua ‘kamanda’ wake mmoja ambaye aliwasha bodaboda na kuwahi eneo la tukio.
 
Huku sekeseke likiendelea makaburini hapo, Mdudu ambaye alikuwa na jazba ya kuibiwa ‘mali’ zake alisema kuwa alitonywa na rafiki zake kwamba mchumba’ke huyo yupo katika Baa ya Kimboka, Buguruni akijirusha na jamaa huyo.
...Mchumba wa mtu akizidi kupokea kipondo.
Mdudu alisema aliamua kwenda katika baa hiyo na kubana sehemu huku akishuhudia kila kitu.
 
“Unajua nimekuwa nikiambiwa tu kuwa Ema ananisaliti lakini nilikuwa napuuzia.
 
“Sasa nimeamini baada ya kumshuhudia mwenyewe akisaliti penzi letu,” alisema Mdudu.

VIKAO VYA HARUSI
Alisema kuwa Ema ni mchumba’ke na anaishi na wazazi wake Buguruni-Malapa, Dar na ameshamtolea mahari.
 
“Ndiyo tumeanza kupanga vikao vya harusi vifanyike katika Baa ya Wazee iliyopo Ilala-Amana (Dar),” alisema.
...Kipigo kikiendelea kwa mchumba wa mtu.
Alisema baada ya kuwasubiri hadi usiku wa manane, aliwaona wakiinuka na kuingia kwenye teksi ndipo na washikaji zake nao wakachukua bodaboda na kuifuata ile teksi kwa nyuma bila wahusika kushtuka.

WAKUTWA LAIVU
Alisema walishangaa kuona gari lile likipaki maeneo ya Makaburi ya Buguruni kisha dereva akatoka na kwenda kusimama mbali kidogo akivuta sigara.

“Machale yakanicheza nikawatonya wanangu kuwa tusubiri kama dakika kumi halafu tukaivamie teksi.
Watuhumiwa wakiwekwa sawa kabla ya kupelekwa kituo cha polisi.
“Baadaye uzalendo ulinishinda ikabidi nikavamie. Ndipo tukawakuta laivu wanavua nguo wakiwa kimahaba,” alisema Mdudu.

Alisema roho ilimuuma alipomkuta mchumba’ke huyo ambaye anampenda kwa dhati akiwa katika hali ile, nusura apoteze fahamu na mara baada ya kuwavamia waliwatoa nje ndipo sekeseke likaanza.

KUMBE NI MSANII!
Wakati mtiti ukiendelea, yule mwanaume mwingine aligundulika kuwa kumbe ni msanii wa Bongo Fleva aliyejitambulisha kwa jina la Spince Seseme.
 
Mchumba wa mtu akitoka nduki baada ya kuchoropoka mikononi mwa jamaa waliokuwa wakimpa kipigo.

Akihojiwa na Ijumaa Wikienda kulikoni kufumaniwa na mke wa mtu, Spince alisema hakufahamu kama Ema ni mchumba wa mtu kwani kama angefahamu asingetoka naye kimapenzi.

ANATUMIA UMAARUFU WAKE?
Jamaa huyo aliyeimba Wimbo wa Ayaya akimshirikisha Ali Kiba alidai alifahamiana na Ema siku nyingi na hawakuwahi kuvunja amri ya sita.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wanaomjua jamaa huyo, eti amekuwa akitumia umaarufu wake kupindua uhusiano wa watu na kuapa kumkomesha.“Kama polisi wakishindwa tutamwendea kwa babu ili ajue cha mtu mali,” alisikika brazameni mmoja.

POLISI
Hata hivyo, tukio hilo lilimalizika kwa kila mmoja kukimbilia Kituo cha Polisi cha Buguruni akidai kupigwa ambapo hadi OFM inaondoka walikuwa wakichukuliwa maelezo.

AIBUUUU..... PICHA CHAFU ZA UCHI ZA MSANII MANAKI SANGA NA DEMU WAKE ZANASWA


xdjay  imefanikiwa kunasa picha mbalimbali za aibu za msanii chipukizi na mwanamuziki Manaiki Sanga akifanya ufuska wa kutisha na wanawake tofauti tofauti hali inayoonesha ameazimia kujitoa muhanga juu ya gonjwa hatari la ukimwi linalotishia dunia nzima.


 Habari za uhakika toka kwa chanzo chetu kilichotushushia shehena za  picha hizo kilisema msanii huyo ambae pia ni anaigiza pamoja na kundi  la Ze Komedi la East Afrika Tv tangu apate jina amekuwa akijihusisha  na vitendo viovu vya unyanyasaji wa kijinsia kwa kuwarubuni mabinti  kupiga nao picha za aibu kwa lengo la kutafuta jina na amekuwa 
akitumia kiasi kikubwa cha pesa kufanikisha suala hilo. 


Aidha katika hali nyingine msanii huyo aliyetamba sana kwenye filamu  ya Love Position, Tikisa na nyinginezo amekuwa akitumia gari yake  kufanyia ufusika  hadharani....


























Mtandao wa  xdjay  umefanikiwa kunasa picha mbalimbali za aibu za msanii chipukizi na mwanamuziki Manaiki Sanga akifanya ufuska wa kutisha na wanawake tofauti tofauti hali inayoonesha ameazimia kujitoa muhanga juu ya gonjwa hatari la ukimwi linalotishia dunia nzima.

Habari za uhakika toka kwa chanzo chetu kilichotushushia shehena za  picha hizo kilisema msanii huyo ambae pia ni anaigiza pamoja na kundi  la Ze Komedi la East Afrika Tv tangu apate jina amekuwa akijihusisha  na vitendo viovu vya unyanyasaji wa kijinsia kwa kuwarubuni mabinti  kupiga nao picha za aibu kwa lengo la kutafuta jina na amekuwa
akitumia kiasi kikubwa cha pesa kufanikisha suala hilo.
 
Aidha katika hali nyingine msanii huyo aliyetamba sana kwenye filamu  ya Love Position, Tikisa na nyinginezo amekuwa akitumia gari yake  kufanyia ufusika

" Kwa kweli hali ni mbaya ile gari yake ameigeuza kama  gesti ambapo ukiiona gari hiyo imepaki sehemu kwa muda uje kuna  shughuri inafanyika ndani hivyo tunaliomba jeshi la polisi Kanda ya  Dar es  Salaam kulifanyia kazi suala hilo kisha kumtia mikononi huenda  wasichana wa watu wakasalimika jamani" Alisema muhudumu wa baa ya Coco  Beach ambako msanii huyo huwa anapenda kukaa.

Gari ya msanii huyo imekuwa maarufu sana huku nyuma ya gari hiyo  kukiwa na maneno haya " Nina Fanya Mambo" Money is Paper na inadaiwa  msanii huyo ni mtoto wa kigogo mmoja maarufu ambae anamiki hotel  kadhaa hapa mjini ikiwemo Itumbi iliyopo Magomeni.
 
Picha hizi zinawaonesha mamisi mbalimbali Kama Irine Kanka ambae  alikuwa Miss Temeke namba 2 mwaka juzi. Miss Utalii Fathiya Alfan"  Mrembo wa Facebook" Dida ambae ni mwanamuziki huko Zanziba. na  wengineo.

Hata hivyo watu wamemuonya msanii nyota wa kike nchini
Wastara kutompa nafasi msanii huyo kwani akifanya hivyo atakuja kujuta  kwani imeonekana siku za hivi karibuni amekuwa na ukaribu sana kiasi  cha kwenda nyumbani kupata chakula.
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DODOSO - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger