Watu watatu wakiwemo waganga wawili wa jadi wamekamatwa na polisi katika
eneo la Igombe Tx, jijini Mwanza wakiwa na kiganja cha mkono wa kulia
unaoaminika kuwa wa binadamu.
Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza,
kamishna msaidizi wa polisi Joseph Konyo amesema tukio hilo limetokea
eneo la kati ya ziwani na nyuma ya uwanja wa ndege wa Mwanza baada ya
raia wema kuwapa taarifa za siri.
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.