
Ustadhi Yahya Michael, mkazi wa Dar, hivi karibuni amejitokeza na kudai
kuwa yeye ndiye mganga aliyempaisha mwanamuziki Nasibu Abdu ‘Diamond
Platnumz’ ambaye kwa sasa ni kinara wa Bongo Fleva.....
Akizungumza na Risasi katika mahojiano maalum maeneo ya Magomeni, Dar, mganga huyo
alidai kuwa pamoja na jitihada kubwa alizofanya kumpaisha Diamond
lakini anamshangaa kwa kuwa amesahau alikotoka na anajifanya supastaa.
Alidai kuwa siku hizi akimpigia simu, Diamond huwa hapokei, tofauti na zamani alipokuwa akihangaika kuchomoka kisanii.
Mganga
huyo alifunguka kuwa sababu ya kufanya hivyo ni baada ya kuchukuliwa na
watu waliompeleka...