ETIIII,,,, KUMBE WANAWAKE KUTEMBEA NUSU UCHI WANA LAO JAMBO????.....

 
Kuna wakati wanaume hudhani kwamba, wanawake wanaovaa nusu uchi huwa wanafanya hivyo kwa sababu ya kutafuta soko kwa wanaume. Inawezekana kukawa na wale ambao wana sababu hizo, lakini wapo wale ambao wanalipa fidia kutokana na kuamini kwao kwamba, sura zao zimewaangusha, hivyo miguu yao mizuri inabidi kuziba pengo au udhaifu huo.

Wakati mwingine hata wanawake wanaodhani au kudhaniwa kuwa ni wazuri, wamekuwa wakivaa nguo fupi zinazoonyesha maungo yao. Hawa nao ni lazima wanalipa fidia ya kasoro fulani waliyo nayo. Inawezekana wameshindwa kulinda ndoa zao, au inawezekana hawajaolewa na sasa wanataka kuonyesha kwamba, pamoja na kutoolewa kwao, bado wao wana sura na miguu au miili mizuri.

Udhaifu wowote ambao unamkera mwanamke iwe ni wa moja kwa moja au kupitia nyuma ya ubongo wake, unaweza kuonyeshwa kwa mwanamke huyo kuyatangaza yale maeneo ya mwili wake ambayo anaamini ni mazuri. Kuyatangaza huko humpa ahueni kwa kuamini kwamba bado anayo thamani, kwani ataangaliwa sana na wanaume, kusifiwa na pengine kutongozwa.

Hebu angalia wanawake ambao wanavaa nguo za kubana huku wakiwa na makalio makubwa. Hawa mara nyingi wana sura ambazo wao au wengi huamini kwamba ni mbaya. Huvaa nguo hizi ili kuonyesha kwamba, pamoja na ubaya wa sura zao, bado wao ni wazuri sana katika maeneo mengine ya mwili ambayo wanaume na hata wanawake wengi huyapenda au kutamani kuwa nayo.

Wengi hawavai tu nguo hizi za kubana kwa sababu ni fasheni, la hasha, wengi hili ni kimbilio la udhaifu wao.

WANAWAKE WANAVYOIVAA MKENGE WANAPOAMUA KUOLEWA........./////

 
Ngoja leo niyadadavue makosa yanayofanywa na wanawake wengi pale wanapoamua ni nani wa kuoana naye:

1. Kosa la kwanza, unaolewa na mtu ambaye unajua kabisa ni dhaifu na mkorofi, ukitarajia kwamba ataondoa kasoro zake akiwa ndani ya ndoa. Hili ni kosa kubwa. Kama huna furaha sasa na mtu kabla hujaoana naye, usikubali kuingia huo mkenge. Huwezi kutegemea mtu kuadilika aiwa ndani ya ndoa.

2. Kosa la pili, unaolewa na mtu asiye sahihi kwa sababu ya msisimko wa mwili kimapenzi lakini si kwa sababu ya tabia zake. Kuwa mwangalifu na neno “Nakupenda” neno hili mara nyingi maana yake ni “Nina uchu nawe.” Ndiyo amevutiwa nawekimaumbile, lakini undani wa tabia yake unaujua? Hapa kuna mambo manne… Kwanza, Je anapenda kutomfanyia binadamu mwenzie mabaya kama mabavyo yeye hataki kufanyiwa? Pili, anaishi vipi na watu wengine? Anaishi vipi na watu ambao ana uadui nao, Anawasamehe au analipiza visasi? Je anatoa misaada kwa masikini? Tatu, je ni mkweli, anachokisema ndicho anachokifanya? Je anaaminika? Majukumu anayoahidi kuyafanya anayatimiza? Nne, je anajipenda? Je ni mtu ambaye yuko imara kimapenzi au ni mtu wa kuyumbayumba na asiye na msimamo? Sio mtu akishauriwa na marafiki zake au ndugu zake huko, anakuja na maamuzi yasiyo na kichwa wala miguu

3. Kosa la tatu, unaolewa na mtu ambaye hamna malengo na vipaumbele vya aina moja vya maisha. Je mna utashi wa aina moja? Kwa mfano ni vyema mwanamuziki akaolewa na mwanamuziki mwenzie kwa kuwa anajua mzingira ya kazi ya mwenzie ili kupunguza wivu wa kupindukia usio wa lazima

4. Kosa la nne, unaolewa na mtu asiye sahihi kwa sababu mnakutana kimwili mapema mno. Kukutana kimwili kabla ya ndoa kunaweza kuleta matatizo makubwa mno. Tendo la ndoa kabla ya ndoa hufunika uwezo wa mtu kufikiri. Mtu anabaki kufaidi na kubaki kujali mapenzi ya kimwili na kusahau kukuna ubongo juu ya mambo mengine. Ni lazima mwanamke akune ubongo ili kujua kama huyo mpenzi anakidhi vigezo vyote vya mume mtarajiwa.

5. Kosa la tano, unaolewa na mtu ambaye huna msisimko wa kimwili umwonapo. Kuna uwezekano mkubwa mwanamke akavutiwa na mwanaume kwa sababu ya aina ya gari analomiliki. Hapa hakuna msisimko wa kimwili bali mwanamke kavutwa na gari au rasilimali alizo nazo mwanaume huyo.

6. Kosa la sita, unaolewa na mwanaume anayependa kudhibiti. kuwa na tabia ya kudhibiti wenzako ni ya dalili za mtu jeuri na mwenye kujisikia na mfujaji. Naomba kutofautisha kati ya “kudhibiti” na “kutoa mawazo.” Mtu anayekupa mawazo ni kwa faida yako, lakini anayekudhibiti ni kwa faida yake.

7. Kosa la saba, unaolewa na mtu asiye sahihi kwa sababu unakimbia matatizo uliyo nayo. Unaweza kuwa hujaolewa na huna raha wala amani na ukataka kuolewa. Ndo haiwezi kukutatulia matatizo yako binafsi ya kisaikolojia nay a kimapenzi. Badala a kuyapunguza matatizo hayo, ndoa itayaoneza. Kama huna amani na huyafuahii maisha, chukua jukumu la kurekebisha matatizo hayo sasa kabla hujaolewa. Itakuwa ni faida kwako na kwa mmeo mtarajiwa.

8. Kosa la nane, unaolewa na mtu asiya sahihi kwa kuwa yuko ndani ya pembe tatu. Mtu ambaye anaishi na wazazi wake ni moja ya mfano wa mtu anayeishi katika pembe tatu. Watu wengine wanaoweza wakawa wanaishi ndani ya pembe tatu ni kama wanaofanya kazi saa 24! Huyu mtu halali? Watu wengine walio katika pembe tatu ni watu wanaotumia madawa ya kulevya, mtu anayetawaliwa na “hobbie” zake, anapenda sana michezo (Mpira), kuperuzi mitandao ya kijamii na anapenda sana fedha. Hakikisha kwamba wewe na mpenzi wako , nyote hamtawaliwi na pembe tatu. Mtu ambaye anatawaliwa na pembe tatu hawezi kumtimizia mpenzi wake haja ya upendo atakapokuwa anahitaji. Kama mpenzi wako anatawaliwa na pembe tatu kwa kiasi kikubwa, wewe huwezi kuwa kipaumbele chake.

NI KWELI......... MZAHA NA KUCHEKA KWA WANANDOA HUDUMISHA MAPENZI?........

 
Kucheka mara kwa mara kutakuondolea msongo wa mawazo na mifadhaiko; pia kutakufanya kulala usingizi mnono na kufurahia maisha yako. Uchekeshaji ni kitu muhimu sana na ndio maana viongozi wakuu, waalimu na washauri nasaha wengi ni wachekeshaji katika mazungumzo yao.

Mara nyingi ninapozungumzia au kujadili kuhusu kucheka, huwa najiuliza, hivi ni ndoa ngapi ambapo wanandoa wake hucheka na vicheko hivyo hutoka kwa wenzao? Nalijua jibu, lakini silipendi, ingawa siwezi kuubadili ukweli. Kama kuna ndoa kumi, basi ni ndoa mbili tu ambapo wanandoa wake hupeana afya kupitia kuchekeshana.
Kwenye ndoa nyingi, utakuta mke au mume amenuna muda wote. Hata mwenzake anapojaribu kumchekesha ili kufanya hali iwe na mwelekeo wa amani na upendo, ni kazi bure. Mke au mume huyu anapokuwa nje na nyumbani kwake, ni mchekaji mzuri sana tena wa vichekesho vya kawaida mno!
Nimebaini kwamba, ndoa inapokuwa na vichekesho yaani mzaha na utani usioumiza, humfanya kila mwanandoa kutamani kuwa nyumbani kwake, humfanya kila mwanandoa kuhisi haja ya ukaribu wa mwenzake. Lakini kubwa zaidi ni kwamba, mwanandoa hujenga afya yake ya akili, mwili na hisia kupitia kicheko.
Mara nyingi nikitazama zile sinema za dhati zilizobuniwa na wataalamu wanaojua Nyanja nyingi za kimaisha, huwa ninaona kicheko kikitumiwa sana kuelezea au kuonesha kama ndoa ni ya amani au vurugu. Kama ndoa ni ya amani, ni wazi utaona wanandoa wakitaniana na kufurahia sana utani. Huu siyo ukweli wa kisinema, bali ndio ukweli halisi.
Ndoa bora huweza kupimwa kwa kiwango cha utani kati ya wanandoa. Hebu jaribu kufikiri kwa hatua, halafu ujiulize, ni ndoa ngapi ngumu unazifahamu (pengine ikiwemo yako). Halafu jiulize, huwa unakuta wanandoa hao wakitaniana mara ngapi, kama imeshatokea ukawa karibu nao? Utapata jibu kirahisi sana. Hujawahi, na kama umewahi, basi ni kwa tukio maalumu au tukio la makusudi la wanandoa hao,kukuonesha wewe kwamba, wanandoa hao wako katika amani. 
Ukweli unaendelea kubaki kwamba,kama wanandoa wanajua kuchekeshana, tena kwa makusudi, vurugu ndogondogo huwa zinafutwa kirahisi sana. Ni lazima zifutwe kwa sababu, hatimaye kila jambo huingizwa kwenye mzaha na kuvurugiwa humo.
Wataalamu wanasema, mahali popote ambapo watu wana dhati sana ya mambo (serious), hapo kuna maumivu mengi. Kuna nyumba ambazo kila jambo linajadiliwa na kuzungumzwa kwa sauti kavu na imara ya dhati – hakuna mzaha hata chembe. Mke na mume wako pamoja tangu asubuhi, lakini hakuna hata mmoja ambaye amemfanya mwenzake akacheka. Kama yupo anayejaribu , atakutana na kizuizi cha, ‘si wakati wa mzaha huu.’

Napenda kukushauri kwamba, hebu kuanzia hivi sasa anza kufanya mzaha mdogomdogo kwa mwenzako, lakini wenye nguvu ya kuchekesha. Kama naye alikuwa hajui utamu wa kuchekesha, ataujulia kwako na huenda naye akaanza kufanya mzaha. Lakini mnaweza kwa pamoja kuamua kuanza kuyageuza maumivu mengi kuwa mzaha na vichekesho. Hili linawezekana.

msiba..... mwanaume afariki kwa kuchangiwa na kupigwa na wanawake wawili



Mwanaume mmoja amepatwa na umauti baada ya kuchangiwa na kupigwa na wanawake wawili huko  Madhya Pradesh. mwanamke huyo ambaye alishirikiana na mkwe wake aliyeolewa na mwanawe kumpiga mumewe tena nnje ya mahakama, alifanikiwa kumuua,kisa ni ugomviwa ardhi, wameshikiliwa na polisi kwa uchunguzi zaidi.

SWALI.....JAMANI HUYU MWANAUME ANAYEPENDA KUPIGA WANAWAKE ANGEKUWA TANZANIA ANGEKUWA KABILA GANI?


JE,,,,KWANINI WANAWAKE WENGI KWENYE NDOA HUPIGWA NA WAUME ZAO NA WENGINE HUPIGWA HADI KUFA..../////

 
Tunajua wote kwamba, hutokea wanawake wakateswa sana kwenye uhusiano wao wa kindoa au kimapenzi na bado wakaendelea kukaa tu kwenye uhusiano huo. Inafikia hadi mtu anakufa huku akiona kabisa. Watu wengine huiita hali hii kuwa ni ujinga na wengine huita kulogwa au huelezea hali hii kwa njia ambayo haiwapi haki wanawake hao. Zipo sababu nyingi ambazo zinawafanya wanawake kuendelea kukaa kwenye ndoa ngumu, bila hata kufikiria kuondoka. Sababu nyingine zinaweza kuonekana kama kituko, lakini ndizo zinazowafanya wafie kwenye ndoa.

Kuna ile sababu kwamba, hawajui ukubwa wa kiwango cha mateso. Hii hutokana na kwamba, baada ya kuzoea mateso, mwanamke hufikia kuamini kwamba, hayo siyo mateso, bali ndivyo ndoa inavyotakiwa iwe. Kuna sababu ya kukosa marafiki, ndugu au jamaa wa karibu. Na kwa sababu hana watu wa aina hiyo, inakuwa vigumu kwake kuwa na mahali pa kukimbilia ili aweze kupata nafasi ya kujiandaa kuanza upya maisha. 


Kuna wanaoendelea kukaa kwa sababu dini zao zinawaambia, hawana budi kukaa, kwani wameshakuwa mwili mmoja na waume zao na hivyo hawawezi kuondoka. Wanafikiria iwapo wataamua kutoroka, viongozi wao wa dini watawaona vipi na waumini wenzao watachukuliaje jambo hilo. Kwa hiyo, wanaishi kwenye ndoa hizo kwa sababu ya dini, siyo kwa sababu yao binafsi. Halafu kuna suala la kupenda. Utegemezi wa kihisia huwa unaitwa kupenda. Kwa hiyo mwanamke anasema anampenda fulani kiasi kwamba, hawezi kumwacha, wakati ukweli ni kwamba, anamtegemea mwanaume huyo kihisia.Wanawake wanaoteswa kwenye ndoa, huwa wanajidanganya kwamba, watamudu siku moja kubadili tabia hiyo a waume zao kuwafuja. Wanajiambia kwamba, kutukanwa, kupigwa, kudhalilishwa, na matendo mengine, siyo hiari ya hao waume wao. 


Hivyo wanaamini kwamba, kuna siku watamudu kuwasaidia watoke kwenye tabia hizo. Lakini wakati mwingine wanaume hawa watesaji, huwa wanajidai kusema kwamba, wanafanya mambo hayo bila kujua sababu na kuna wakati wanasema wamelogwa.Hujawahi kuwaona wanawake wanaokwenda kwa waganga kutafuta dawa ili waume zao wasiwapige, ati kwa sababu vipigo vyao vinatokana na kuchananywa na uchawi wanaofanyiwa na wanawake zao wa nje? Mwanamke anaamini kabisa kwamba, mumewe hamjali na anamdhalilisha kwa sababu ya kulogwa!Mwanamke anaweza kujiambia kwamba, kwa sababu mume wake kuna wakati anamtendea wema, hata kama ni moja, basi anampenda na hayo mengine mabaya, yatakwisha au ni bahati mbaya. 


Mwanamke pia anaweza kufikiri kwamba, akijitahidi sana kumfurahisha mumewe, mume huyo atabadilka na kuwa na tabia nzuri. Hivyo hujipendekeza na mwanaume habadiliki na mateso yanaongezeka. Kuna wanaomudu kuishi kwenye uhusiano huu wa sababu, wamemudu kukandamiza, kupunguza ukubwa wa maumivu. Wanajiambia kwamba, wanavyotendewa siyo vibaya sana. Mwanamke anaweza kujiambia, ‘alinipiga kidogo tu, tena mara mbili kwa mwezi, kuna wanaopigwa kila siku.’ Huyu amehalalisha kipigo na mateso, hawezi kuondoka.


Kuna wanawake wanaoamini kwamba, ndoa inajengwa na kuimarishwa na mwanamke au kuvunjwa na mwanamke pia. Kuna andiko moja katika Biblia hutumiwa sana kuwatisha, linalosema, ‘Mwanamke m.p.u.m.b.a.v.u huivunja ndoa yake kwa mikono yake mwenyewe.’ Kwa hiyo wanapofikiria kuondoka, hufikiria kwamba, watu watajua na kumzonga au kumdharau kwa sababu ameshindwa kulinda ndoa. Wengine ni woga tu, kwamba, wakiondoka waume zao watawalipizia visasi au watawasumbua. kuna wakati waume wenyewe ndiyo wanaokuwa wamewatisha kwa kiwango hicho.

maajabu....../////// picha za kwanza za mtu aliyeliwa sura yake akiwa hai.....

Madactari nchini Marekani wametoa picha za mwanzo za mwanaume ambaye sura yake pamoja na pua yake ililiwa na mtu aliyekuwa amepagawa na madawa mapya ya kulevya yanayomfanya mtu awe na hasira kali na mwenye kutaka kujiua.

 Baada ya mei 26 mwaka huu, Ronald Poppo mwenye umri wa miaka 65, Mzee aliyekuwa hana makazi maalumu akilala mitaani, kushambuliwa na kuliwa sura yake alipokuwa amelala pembeni ya stesheni, madaktari wa hospitali ya Miami nchini Marekani wametoa picha na video za Poppo wakisema kuwa anaendelea vizuri na matibabu.

Katika tukio hilo, Rudy Eugene, aliyekuwa na umri wa miaka 31, akiwa uchi wa mnyama huku ikisemekana akiwa amepagawa na madawa mapya ya kulevya yanayoitwa "Bath Salts" au "Ivory Wave", "Purple Wave" au "Vanilla Sky", alimshambulia Poppo ambaye naye alikuwa uchi wakati wa tukio.

Eugene aliutafuna uso wa Poppo na aliendelea kuutafuna pamoja na kupigwa risasi na polisi ili kumfanya asiendelee na shambulio hilo. Polisi walilazimika kumpiga risasi 12 Eugene ndipo alipofariki na shambulio hilo ndipo lilipofikia kikomo.

Lakini hadi shambulio hilo linaisha, asilimia 80 ya sura ya Poppo ilikuwa imeishaliwa. Alikuwa ameishaliwa pua yake yote, jicho lake moja huku jicho jingine likiwa limeharibiwa vibaya sana. Madaktari wanahofia Poppo huenda akapoteza jicho hilo lililobaki akawa kipofu.

Sura yake iliharibiwa vibaya sana kiasi cha kuwafanya madaktari wamfanyie operesheni kadhaa za kurekebisha sura yake.

Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa Eugene ambaye hakuwa na historia ya uhalifu, alikuwa amelewa madawa hayo mapya ya kulevya ambayo humfanya mtu awe mwenye hasira kali, mwenye kutamani kujiua na mwenye kufikiria vitu vya ajabu ajabu.

Madawa hayo ya kulevya ambayo hutengenezwa mitaani kutokana na mchanganyiko wa kemikali yanasemekana pia kumfanya mtu awe anatamani kula nyama za watu. Hivi karibuni babu mmoja wa nchini Marekani aliyetumia madawa hayo ya kulevya alitiwa mbaroni baada ya kutishia kuwatafuna maafisa wa polisi.

Wiki tatu baada ya tukio hilo, madaktari wametoa picha na video ya Poppo wakisema anaendelea vizuri na matibabu.

UKATILI JAMANIII......Mume amuua mkewe na mwili wa marehemu kukutwa katika stoo ya nyumba...

 
Habari zinadai kuwa siku moja Hamida akiwa kwao, Tabata, mume alitishia kujiua na kumfanya marehemu kwenda kutoa taarifa Kituo cha Polisi Tabata na kufunguliwa kumbukumbu ya jalada namba RB TBT/ RB/ 1583/ 2013 TAARIFA.
Pia Hamida alikwenda kutoa taarifa kwenye Baraza Kuu la Kiislamu Tanzania (BAKWATA) ili aweze kupewa talaka yake.
 
 Hamida Issa siku alipohitimu kidato cha sita akiwa na mumewe Yahya pembeni
“Mumewe aliandikiwa barua ya wito na Bakwata lakini hakwenda.
 
“Siku moja mwanaume huyo alimpigia simu mkewe na kumwambia anataka kuhamia Sinza kwa hiyo aende nyumbani kwao vingine wagawane. “Mama yetu (Zaria Munge)alimzuia Hamida kuvifuata vitu hivyo lakini marehemu alilazimisha kwa madai kuwa mumewe akihamia sehemu nyingine itakuwa vigumu kuvipata vyombo vyake,” alisema Rehema.
 
Inadaiwa kwamba mwanaume huyo alikwenda nyumbani kwa wakwe zake ili akamchukue mkewe wakagawane hivyo vyombo. Kutokana na shaka, marehemu aliamua kumchukua mdo go wake ili wawe wawili.
 
Habari zinadai Hamida na mumewe walitembea sanjari huku mdogo mtu huyo akitangulia na kwenda kufikia kwa jirani wakati akiwasubiri.
 
Wawili hao walipofika, mdogo mtu huyo aliwafuata kwa lengo la kuungana nao katika zoezi la kukusanya vyombo lakini sh- emeji yake alikataa na kumtaka abaki nje kisha akafunga mlango kwa ndani.
 
“Nilipoona shemeji amekataa nisiingie na akafunga mlango niliamua kurudi kwa yule jirani. Mara shemeji akanipigia simu kwa namba ya dada ikisema nirudi nyumbani kwani wao bado wana shughuli maalum,”
baye jina halikupatikana mara moja
.
 
Akiwa njiani, alipigiwa tena simu na shemeji yake huyo akimwambia kuwa muda si mrefu simu zote zitazima chaji lakini asiwe na wasiwasi wowote.
 
Habari zinasema kuanzia wakati huo hadi saa sita usiku Hamida hakuwa amerudi kwa mama yake, lakini mara Yahya alimpigia simu mdogo huyo wa marehemu akimuulizia kama dada yake ameshafika nyum bani hapo!
 
“Nikashangaa sana, inakuwaje shemeji aniulize hivyo wakati niliwaacha pamoja baada ya kunizuia kuingia ndani? Kuanzia hapo nikaingiwa na wasiwasi,” alisema.
 
Asubuhi ya siku ya pili, ndugu wa Hamida walikwenda Mbagala na kutoa taarifa polisi ya kupotelewa na ndugu yao huyo katika mazingira ya kutatanisha, polisi walikataa kutoa ushirikiano ikiwemo kuvunja mlango wa nyumba hiyo ili kujiridhisha ndipo waliondoka huku mioyo yao ikiwa imegu bikwa na wasiwasi.
 
Jumanne iliyopita mama mzazi alipokea simu kutoka kwa mjumbe wa eneo la Kwamjerumani (ilipo nyumba ya Yahya) na kumtaarifu kuwa kuna harufu kali sana kutokea kwenye nyumba ya Yahya hivyo wafike mara moja kwa ajili ya ukaguzi.
 
“Simu hiyo ilinishtua sana, nikawataarifu ndugu akiwemo dada wa marehemu, tukaenda,” alisema mama mzazi.
Akaendelea kusema kuwa baada ya kufika mahali hapo, walichukua uamuzi wa kuvunja mlango kwa kupewa ruhusa na mjumbe ambapo chumbani waliukuta mwili wa Hamida ukiwa kitandani.
 
Marehemu alikuwa ameshindiliwa nguo kinywani na kufungwa kitambaa shingoni huku mwili wake ukiwa ndani ya nailoni ikionekana kuwa unyon-gaji umefanyika.
 
Baada ya taratibu zote ku fanyika mwili wa marehemu ulipelekwa katika Hospitali ya Temeke kwa uchunguzi zaidi.
Marehemu Hamida alizikwa Jumatano iliyopita katika Kijiji cha Mzenga, Bagamoyo, Pwani. Ameacha mtoto wa kike aitwaye Tayana. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali panaposta- hiki. Amina.

Sababu sita kuu na za msingi zinazojibu swali la kwanini siku hizi wanaume wengi hawapendi kuoa?,,,,,,

 
Kumekuwa na maswali yasiyo na majibu miongoni mwa jamii kwamba imekuaje vijana wa kiume wamekuwa ni waongo sana hasa linapokuja swala la kuoa? Kwa kadiri siku zinavyozidi kwenda ndivyo ambavyo idadi ya wanaume wanaoogopa kuoa inazidi kuongezeka. Utakuta wapenzi wanaambiana kwamba wanapendana na kuahidiana kuwa wataoana, lakini kitakachotokea baada ya hapo ni mwanaume kuanza kupiga chenga kwa visingizio lukuki.

Kwa nini hali hiyo hutokea?

Ukweli ni kwamba hakuna jibu la moja kwa moja juu ya tatizo hilo, lakini yapo mambo ambayo yanaweza kutupa angalau tafakuri. Nitajaribu kudadavua baadhi ya sababu zinazowafanya wanaume siku hizi kukwepa kuingia katika taasisi ya ndoa:

Ukosefu wa mtu wa kumchukulia kama mfano: Hapa nawazungumzia wale watoto wa kiume waliolelewa malezi ya upande mmoja yaani walilelewa na mama peke yao. Sina maana ya kudharau au kutweza malezi ya mama, la hasha, lakini ni vyema mkafahamu kwamba kuwa na baba asiye na malezi mazuri si sawa na kutokuwa na baba. Na ndio maana nikasema ukosefu wa mtu wa kumchukulia kama mfano. Achilia mbali aina ya malezi atakayoyapata kwa familia yawe mazuri au mabaya lakini lazima kutakuwa na tabia za kiume zitakazoakisi malezi ya mtoto wa kiume katika familia husika. Watoto waliolelewa na mama peke yao kuna kitu huwa wanakosa, kwani wanakuwa hawana mtu wa kumchukulia kama mfano kwa upande wa jinsia ya kiume na hapo ndipo hujikuta wakijifunza wenyewe namna ya kuongea na kutenda kama wanaume kwa sababu katika makuzi yao hawakupata fursa ya kuwa karibu na baba zao. Kwa kuwa siku hizi kuna kundi kubwa la kina mama ambao wamejikuta wakiachiwa mzigo wa malezi ya watoto, baada ya aidha kuachwa na waume zao au kuzalishwa na kutelekezwa (Single mothers), na hapo ndipo tunaposhuhudia mtoto wa kiume anapokua kwa umri na kimo huku akiwa hana mtu wa kumuangalia kama mfano wa mume anavyotakiwa kuwa katika familia zaidi ya kujifunza mambo hayo kupitia katika TV, senema au miziki. Wanaume waliopitia malezi ya aina hii huchelewa sana kuoa kwani huyaangalia maisha ya ndoa kwa namna ya kujaribu na ndipo hapo wengi huishia kuishi kinyumba na wanawake kwa ajili ya kutaka kujifunza namna ya maisha ya ndoa yanavyotakiwa kuwa na ndio sababu huchukua muda mrefu kufanya maamuzi. Na mara nyingi huishia kubadilisha wanawake kutokana na kutokuwa na uhakika wa kile wanachokitafuta.

Mgogoro wa kiuchumi: Kuna kundi kubwa la vijana siku hizi hawana ajira au hawana uhakika na kipato. Ukweli ni kwamba hakuna mwanaume atakayependa kujiingiza kwenye ndoa wakati hana kazi au hana uhakika na kipato chake. Na hiyo ni kutokana na wanawake wengi siku hizi kuonekana kujali zaidi wanaume wenye uhakika na kipato. Hii misemo ya wanawake ya kebehi dhidi ya wanaume wasio na ajira au kipato, kama vile “mwanaume suruale” ina mchango mkubwa sana katika kuwafanya wanaume kukwepa kuoa iwapo hawana ajira au hawana uhakika na kipato chao.


Wanawake wengi kuwa na kiwango cha elimu ya juu: Siku hizi wanawake wengi wameibuka katika kutafuta elimu ya juu kwa juhudi kubwa. Idadi ya wanawake wanaojiunga na vyuo vikuu ni wengi tofauti na ilivyokuwa zamani. Na hiyo ni kutokana na wazazi wengi kubadili mtazamo wao juu ya mtoto wa kike. Zamani mtoto wa kike alichukuliwa kama kitega uchumi. Kwa maeneo ya vijijini na katika familia masikini, watoto wa kike walikuwa wanatazamwa kama, ‘biashara ya kesho’ ambapo watauzwa kwa njia ya mahari. Kwa hiyo thamani yao ilikuwa ni kuolewa, ni ile ya kibidhaa na sio kibinadamu. Lakini tofauti na zamani siku hizi hata kule vijijini kumekuwa na mwamko mkubwa sana wa kumsomesha mtoto wa kike hadi elimu ya juu. Kutokana na mwamko huo wanawake wengi wamejikuta wakiona elimu kama kimbilio pekee la kuepukana na mfumo dume. Mwanamke gani atakubali kunyanyaswa na mwanaume akiwa na elimu yake na labda pia akiwa na kazi yake yenye mshahara na marupurupu ya kutosha, naamini watakuwa ni wachache sana ambao hawajiamini au waliathiriwa na malezi. Kwa upande wa wanaume nao, wamejikuta wakiwaogopa wanawake hawa wenye elimu ya juu kwa hofu ya kuzidiwa kipato na labda kukosa sauti kama mwanaume na hiyo inatokana na ego tu. 

Wanaume huwaona wanawake kama tishio wanapokuwa na mafanikio makubwa kifedha: Inaweza kutokea mwanaume anaweza kuwa na uhusiano na mwanamke ambaye labda tu nisema ni mbangaizaji. Wakati huo anaweza kuahidi kufunga ndoa na mwanamke huyo, lakini iwapo itatokea mwanamke huyo akapata mafanikio kibiashara na kuinuka kifedha. Kama mwanamke asipokuwa makini anaweza kusababisha mwanaume huyo akaingia mitini. Sababu kubwa hapo inaweza kuwa ni hofu ya kuogopa kuongozwa na mwanamke. Kumbuka kwamba mfumo dume bado umetawala vichwani mwa wanaume wengi kutokana na malezi. Mwanaume asiyejiamini ni vigumu sana kwake kuoa mwanamke aliyemzidi kipato. Kwa sababu akifanyiwa jambo dogo tu, inakuwa kama ametoneshwa. Atahisi kutaka kutawaliwa na mwanamke huyo. Jambo ambalo wanawake wanatakiwa kulifahamu ni kwamba kila mwanaume anataka kutambuliwa na kuheshimiwa kama shujaa kabla ya kumfuata msichana. Iwapo utakuwa umesimama iwe ni kifedha au kielimu pale unapotafuta kupata mwenza, inabidi ujishushe sana la sivyo utadoda.


Wanaume wengi siku hizi wana hofu ya majukumu, hasa ya kulea watoto: Kutokana na malezi yao au kile wanachokijua kuhusu watoto, baadhi ya vijana huamini kwamba, kulea watoto ni jambo gumu sana. Lakini wengine wanaamini kwamba, hata mke anapaswa kulelewa kama ilivyo kwa mtoto. Hivyo wanaamua kutafuta kwanza uwezo ambao haupatikani kiurahisi. Kuna wengine, ambao wamefundishwa au kuelekezwa na mila na desturi zao kwamba, kabla hawajaoa, ni lazima wawe na nyumba kwanza, tena kwao. Kwa hiyo, hawa hadi waje wapate uwezo wa fedha wanakuwa wameshachelewa.

Kuna baadhi ya wanaume, maisha bila ya ndoa wanayaona kuwa ndiyo bora kuliko yale ya ndoa: Kuna baadhi ya wanawake hujirahisisha sana kwa wanaume. Siku hizi ni jambo la kawaida sana kukuta mwanaume anaishi na mwanamke bila ndoa, wenyewe wanaita Trial Marriage. Na hapo ndipo unapokuta wanaume hawaoni tena umuhimu wa kuoa. Sasa kama mwanamke anaweza tu kuishi na mwanaume bila ya ndoa na mwanaume huyo akapata huduma zote kutoka kwa mwanamke huyo, unadhani ni kitu gani kitamvuta kufunga ndoa. Jambo lingine ni ile dhana kwamba maana ya ndoa ni tendo la ndoa. Siku hizi wanaume wengi wamejikuta wakiwa hawahitaji tena kuoa kwa sababu tendo hilo linapatikana kiurahisi tofauti na zamani. Siku hizi inawezekana kabisa kumtongoza binti leo na kupata tendo siku hiyo hiyo….. Na hapa siwazungumzii makahaba. Nawazungumzia mabinti zetu ambao wengine ukiwaona ni watu wa kuheshimiwa ukiwaangalia kwa nje lakini kwa ndani hawana lolote, vijana wa siku hizi wenyewe huwaita maharage ya Mbeya.

Kuna sababu nyingi zinazotajwa kusababisha wanaume siku hizi kujivuta sana katika kufanya maamuzi ya kutafuta mwenza. Lakini hizo chache nilizozitaja zina mchango mkubwa.

EWE MWANAMKE UJUE UKWELI LEO....... SIO KILA DALILI YA MWANAMKE KUPENDA NI YA KWELI

 

Siyo kila dalili ya mwanaume kupenda ni ya kweli…!


Kuna wakati ambapo, wanawake wanajikuta wakikabiliwa na swali la, je, mwanaume huyu ananipenda kweli? Hii hutokea pale anapokutana na mwanaume ambaye, huenda amevutiwa naye. Pengine mwanaume naye anaweza kuonesha kuvutiwa na mwanamke huyo.

Kwa hiyo, mwanamke hujiuliza kama akubali ombi la mwanaume huyo na kukubali kuzungumza naye au kuanzisha naye uhusiano, kama mwanaume atakuwa amezungumza naye kuhusu jambo hilo. ni kweli kwamba, kuna ugumu kwa mwanamke kujua hasa ni kwa namna gani anaweza kujua kwamba, huyo mwanaume amempenda kweli au hapana.

Kuna vitu vingi ambavyo vinaweza kuwa ni dalili ya kumpenda mwanamke, lakini wakati huo huo vinaweza visiwe.

1. Hebu tuchukulie kwamba, mwanaume ameonesha kuwa na tabia tunazoziita nzuri. Labda amekumbuka kirahisi jina la mwanamke, ameonesha kuwa msikilizaji mzuri, ameonesha kuwa anajali kuhusu kinachosemwa na mwanamke, na amekuwa anamuuliza maswali kwa dhati na utulivu. Hapa mwanamke anaweza kuamini kwamba, huyu mwanaume anampenda. Lakini ukweli huenda ukawa ni kinyume chake. Inawezekana huyo mwanaume ni muungwana tu, na anaonesha tabia hizo kutokana na uungwana wake na siyo kutokana na kumpenda kimapenzi mwanamke.

2. Kuna watu ambao wana upendo, wamekomaa kihisia na wanajua kuhusiana vizuri na watu. Hii haina maana kwamba, kumwonesha mtu tabia hizo, kuna maana ya kumpenda au kumpenda sana mwanamke. Dalili hizi ni nzuri na inawezekana zikawa zinaonesha mwanaume kumpenda mwanamke, lakini mwanamke asilichukulie jambo hilo kwa namna hiyo.

3. Mwanaume anaweza kuonesha kuwa na udadisi kuhusu mwanamke kwa maana kwamba, kutaka kujua mambo yake, kumfuatilia au kuulizauliza kuhusu habari za mwanamke. Hii haina maana kwamba mwanaume amempenda kimapenzi. Inawezekana mwanaume akawa amevutiwa kimapenzi na mwanamke ndiyo maana akaonesha tabia hizo, lakini siyo lazima iwe hivyo. Kumbuka kwamba, mwanaume anaweza kuvutiwa na mazungumzo ya mwanamke, akavutiwa hata na namna alivyo usoni, hivyo akapenda kuzungumza naye lakini siyo kwa sababu anampenda.

4. Kuna wanaume ambao wana wake au wapenzi, lakini wanajisikia vizuri kusikiliza wanawake wengine au kujua tu habari za wanawake wengine, bila kuwa na haja ya kuanzisha uhusiano nao. Mwanaume anapompa mwanamke ‘ofa’ hasa ya chakula cha mchana au usiku, ni dalili ya wazi ya kuvutiwa naye. Hapa kuna uhakika mkubwa zaidi, labda tu kama mazungumzo yanayotajwa kufanywa wakati huo wa chakula yanafahamika, na ni ya shughuli maalum. Kwa hiyo ‘ofa’ ya chakula ni dalili nzuri na yenye uhakika. Lakini kuna jambo ambalo ni muhimu kwa mwanamke kulifahamu katika hali kama hii. Kuna wakati mwanaume kumpa ‘ofa’ mwanamke kwa chakula cha mchana au jioni, kunaweza kusiwe na maana ya moja kwa moja kwamba, uhusiano utaundwa. Inawezekana katika kutoka outing huko, mwanaume akaghairi. Kwa wengine huchukua muda hadi kuamua kuhusu kuunda uhusiano au hapana.

5. Hata mwanaume kuamua kumpeleka mwanamke kwa familia yao na kumtambulisha kama rafiki yake, ni hatua yenye kuonesha kwamba, mwanaume ameamua kumpenda mwanamke huyo. Lakini wakati mwingine hii inaweza ikawa ni janja yake kutaka tu kumthibitishia mwanamke ili amhadae vizuri, na wala hakuna maana ya uhusiano wa kudumu.

6. Kuzungumza kwa pamoja kuhusu masuala ya baadaye ya kiuhusiano, kama vile, idadi ya watoto na mambo mengine ambayo mara nyingi huzungumzwa na watu ambao tayari wako kwenye uhusiano ni dalili ya mwanaume kuvutiwa mwanamke. Lakini tatizo la jambo hili ni kwamba, kuzungumza masuala ya baadaye inaweza kuwa ni njia ya mwanaume kutaka kujisikia au kujua jinsi inavyokuwa katika mambo hayo. Inaweza kuwa pia ni njia yake ya kutaka kupima wanawake wanavyosema kuhusu masuala hayo. Lakini inaweza ikawa mwanaume huyo anatafuta kujua misimamo ya mwanamke huyo ili hatimaye afanye uamuzi. Kwa hiyo, bado haioneshi kuwa amevutiwa na kuamua tayari.

Mara nyingi wanawake hudanganywa na dalili fulani zinazooneshwa na wanaume wakati wanapoanza kuzoeana nao. Dalili hizi huwafanya kuamini kwamba, wanaume hao wamewapenda tayari, wakati siyo kweli. Kwa kuangalia baadhi ya dalili hizo kama nilivyozitaja, mwanamke anaweza kuwa makini wakati anapoanzisha uhusiano, ili asikurupuke na kujikuta amedanganyika. Ni kweli, kuna wakati ni dalili zinasema kweli, lakini kuna wakai zinadanganya kuhusu kupenda au kupendwa.

TANGAZO LA KIFO BUNGENI DODOMA

Marehemu Anselm L. Mrema enzi za uhai wake.
Katibu wa Bunge, anasikitika kuwataarifu wananchi kuhusu kifo cha mtumishi wa Ofisi ya Bunge katika idara ya shughuli za Bunge, Mkurugenzi Msaidizi Ndg. Anselm L. Mrema kilichotokea jana usiku tarehe 10.11.2013 katika Hospitali ya Mkoa, Dodoma.
Ofisi inaendelea na taratibu za mazishi kwa kushirikiana na familia ya marehemu, tutaendelea kuwapa taarifa zaidi kutokana na msiba huo. Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe. Amen!
 Chanzo: Michuzi…

Msaniii wa taarabu Nyawana Fundikira afariki dunia.

Msanii wa taarab nchini anayejulikana kwa jina la Nyawana Fundikira aliyetamba na wimbo wa 'Nipo Kamili Nimejipanga', amefariki dunia mchana huu kwa ugonjwa wa malaria.
Nyawana amefariki akiwa kwake maeneo ya Mwananyamala B na mwili wake sasa umepelekwa kuhifadhiwa Hospitali ya Mwananyamala, Dar.

daaah..... MAUTI IPO NJIANI INAMVIZIA MTU HUYU..... KWA MUJIBU WA DACTARI


Doctor Amesema kijana Huyu Atafariki Baada Ya 

muda mfupi Kwa Sababu damu imevujia ndani ya 

Ubongo Wake Na Amesema Hawana Uwakika Kama 

Wataweza Kumnusuru.


Lakini Mungu Pekee ndio anauwezo Wa Kuongea 


Juu Ya Huyu kijana Na Anaweza Kumponyesha, 

Eeeh Mungu Twaomba Umponyeshe Huyu kijana 

Na 

 Uweze Kushinda Maneno Ya Doctor. 
 

 Kama Unaamini Mungu Anaweza Kumponyesha 
 
Huyu kijana Comment "Amen" Kwa Huyu kijana 

james Na "Share" Kwa Maombi Zaidi ya watanzania 

wenzake

HAYA SASAAA,,, VIASHIRIA VINAVYOMUONYESHA MPENZI MPYA KUWA WEWE NI KIN'GAN'GANIZA KWAKE....

Mwanamke: Dalili zitakazomfanya mpenzi mpya akuone wewe ni king’ang’anizi…!

Hizi ni miongoni mwa sababu ambazo wanaume wengi huchomoa mapema kwa wapenzi wao wapya kabla uhusiano haujashika kasi. Kuna wakati wanawake hukosea na kuvuka mipaka mwanzoni tu mwa uhusiano. Anamganda mwanaume haraka sana au anaonesha dalili zote za kujipendekeza kupita kiasi. Lakini jambo ambalo wanawake wengi hawalijui ni kwamba, wanaume wako makini sana kuwakwepa wanawake ving’ang’anizi……..

Nitadadavua baadhi ya vijitabia vya wanawake vinavyowafanya wanaume wawaone kama ni ving’ang’anizi…..
1. Unataka kuwa naye muda mwingi kuliko kawaida… Ni vizuri kwa wapenzi wapya kupata fursa ya kuwa pamoja peke yao, lakini kama unakataa kuwa na mtoko, kuhudhuria sherehe au kukutana na marafiki na kulazimisha kuwa pamoja peke yenu mahali fulani pa faragha, basi hapo ni lazima mwanaume atadhani kwamba unataka akupe umuhimu wa pekee muda wote. Unaweza kukuta mwanamke anakuwa king’ang’anizi kiasi kwamba hana muda na marafiki zake au watu wengine isipokuwa mpenzi wake. Anakuwa kama mzigo, muda wote yuko nyuma ya mwanaume kila anapokwenda…. Hapa ni lazima mwanaume atatemana na wewe kungali mapema. Hakuna mwanaume anayeweza kujenga mahusiano na mwanamke wa aina hii, watakukimbia kila siku.

2. Unampangia mwanaume kila kitu… Unampangia aina ya mavazi ya kuvaa, unaanza kuboresha mazingira ya nyumbani kwake haraka sana kwa kununua vitu mbalimbali vya nyumbani kwake bila kushauriana naye. Hiyo ni dalili kwamba una matarajio makubwa kwake, jambo ambalo kwake yeye bado halijamuingia akilini. Hapa mwanaume ambaye huyachukulia mambo kwa tahadhari, hukuona kuwa wewe ni king’ang’anizi na unataka kukita mizizi kwake wakati bado anachunguza uhusiano wenu ili kujua iwapo utakuwa kama vile anavyotarajia yeye… Kumbuka kwamba kila mtu ana sifa azitakazo pale anapochagua mwenza, na ni vigumu kumjua mtu kwa muda mfupi. Kunahitajika muda wa kutosha mtu kumjua mwenzake vizuri linapokuja swala la mahusianao. 


3. Unatumia muda mwingi zaidi kukaa kwake…. Unalala kwa mpenzi wako, na asubuhi mwanaume huyo anaondoka kwenda kwenye shughuli zake, na wewe unabaki labda ukidai unamsaidia usafi kidogo. Lakini anaporudi jioni anakukuta bado uko hapo nyumbani kwake ukiwa umejipumzisha. Inawezekana ukawa umeandaa chakula cha usiku tayari na pia huenda ukawa umebeba nguo za kubadilisha kwenye mkoba wako pamoja na vipodozi ukiwa umejiandaa kulala tena hapo kwake. Huonyeshi dalili za kuondoka hapo kwake zaidi ya kwenda kwako au kwenu na kubadilisha nguo na kuchukua viti vichache utakavyovihitaji utakapokuwa hapo kwake, lakini unapanga hayo yote bila kumshirikisha zaidi ya kukuona tu ukimganda kama luba. Huonyeshi kuwa na maisha yako kama wewe, zaidi ya kujipachika kwake……


4. Unajenga urafiki na mama yake haraka sana…… Baada ya kukutambulisha kwa mama yake na kubadilishana namba za simu au labda na email, unaanza kujenga ukaribu na mama yake kupita kiasi. Wanawake wengi hudhani kwamba, iwapo watajenga urafiki na mama wakwe watarajiwa, basi itakuwa rahisi kwao kumnasa mwanaume huyo, maana huamini kwamba watoto wa kiume hawawezi kwenda kinyume na mama zao linapokuja swala la kuchagua mwenza. Kwa kawaida wanaume humuona mwanamke anayejipendekeza kwa mama yake kama vile anataka kulazimisha uhusiano au ndoa, hivyo humchukulia kama ni king’ang’anizi.




5. Unampigia simu na kumuuliza kama yuko wapi….. Unapompigia simu badala ya kumjulia hali unakuwa na maswali ya kipolisi.. ‘Uko wapi?’ ‘Unafanya nini? Maswali ya aina hiyo mwanaume huyachukulia kama ya kimtego na hawafurahishwi nayo. Wanawake wengi huamini kwamba wanaume huwa hawasemi ukweli kuhusu mahali walipo pale wanapoulizwa na wenzi wao. Jambo hilo linaweza kuwa kweli au lisiwe kweli. Inawezekana kuwa kweli kwa sababu labda ya wanaume kukwepa maswali mengi. Mara nyingi wanawake hawaridhiki na jibu moja. Mfano ni jioni ndio ametoka kazini, lakini nakapitia mahali fulani kukutana na rafiki yake, inawezekana ikawa ni kwenye mghahawa au kwenye baa. Kama mwanamke akipiga simu na mwanaume akamwambai yuko kwenye baa na rafiki yake, yatafuata maswali lukuki. Hakuna mwanaume anayependa kuulizwa maswali mengi kama vile anatuhumiwa. Na ndio sababu wanaume wengi wanakwepe kusema mahali walipo. Kwa hiyo ili kuepuka maswali anaweza kujibu kwa kifupi tu kwamba yuko kwenye kikao kazini na hatakuwa hewani, ili apate nafasi ya kuzima simu japo kwa muda. Mwanaume humuona mwanamke mwenye udadisi wa aina hiyo kama king’ang’anizi. 


6. Unakuwa na chuki na wanawake wenzako… Pale ambapo mwenzi wako anapomtaja mwanamke fulani, inaweza kuwa ni mfanyakazi mwenzake, mke wa kaka yake au mtu wanayeshirikiana kibiashara, unaonyesha kisirani cha waziwazi kwamba unakerwa na ukaribu wake na wanawake wengine. Tabia hii inaashiria kwamba wewe unapenda kumiliki na wanaume wengi huwa hawapendi wanawake wenye vijitabia vya kupenda kumiliki. Hapo ni lazima utaonekana kuwa wewe ni king’ang’anizi na uhusiano wenu utavunjika mapema…..

7. Unakubali kila analosema au kila anachokifanya….Kuna kitu kinaitwa ‘uhusiano wa kinyonga.’ Hapa mwanamke anajibadili kupita kiasi ili afanane na mwenzi wake. Unakuta mwanamke anakubali kila kitu anachokiamini mwenzi wake bila kuhoji. Anapoteza utambulisho wake na kujipachika utambulisho wa mwenzi wake. Mwanaume akikuona uko hivyo, atakukimbia, atajua wewe ni king’ang’anizi
8. Unawazungumzia mabwana ulioachana nao kila wakati…Kama una kawaida ya kumzungumzia mwanaume uliyeachana naye mara kwa mara uwapo na mpenzi wako mpya, ina maana kwamba bado hujaachana na jakamoyo la kuachwa. Hakuna mwanaume anayependa kusikia kuhusu mahusiano yako ya nyuma, kwa sababu hayamuhusu. Kama ukiwa unapenda kumzungumzia mpenzi wako wa zamani kila uwapo na mpenzi wako mpya, jua kwamba na yeye pia utampoteza kwa sababu atakuona kuwa wewe ni dhaifu na king’ang’anizi na ndio maana umeshindwa kusimama kama wewe, na badala yake unawaza kuhusu mtu uliyeachana naye pamoja na kwamba uko naye. Sio kwamba ni vibaya kumzungumzia mpenzi mliyeachana, lakini ni vyema kama utamzungumzia pale ambapo kuna ulazima sana wa kufanya hivyo, labda kuna jambo ambalo limamhusu ambalo mnajadili, na ikakulazimu kumtaja…..
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DODOSO - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger