Msanii wa filamu na muziki wa kizazi kipya bongo Baby Madaha, yupo katika huzuni kubwa baada ya kumpoteza mama yake mazazi jana usiku baada ya kuumwa kwa muda mrefu.
Mwili wa marehemu unasafirishwa leo
kupelekwa Musoma nyumbani kwao ambapo mipango yote na taratibu za kuzika
zitajulikana huko.
Mwandishi wa mtandao huu alizungumza na Madaha ingawa hakuweza kuzungumza sana zaidi ya kutokwa machozi huku akisema kuwa amempoteza mama yake kipenzi ambaye alikuwa akimsapoti kwenye vitu vingi ndani ya maisha yake.
“Naumia sana lakini najua yote ni mipango ya Mungu kwani kila kitu kimepangwa, hivyo tunamuombea mama yetu aweze kwenda salama mbele za haki kwani sote hiyo ndiyo njia yetu,” alisema kwa maskitiko makubwa sana.

KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.