picha za mwili wa marehemu baba wema sepetu alipoagwa jijini dar, es salaam


BABA mzazi wa staa wa sinema za Kibongo ambaye pia ni Miss Tanzania 2006/2007 Wema Sepetu, Balozi Abraham Isaac Sepetu ameagwa jana  jioni  nyumbani kwake Sinza - Mori jijini Dar es Salaam.
 
Tukio hilo lilihudhuria na viongozi mbalimbali wa kiserikali akiwemo Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Warioba, Getrude Mongela pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Benard Membe na wengine wengi waliofika kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu aliyefariki dunia Jumapili ya wiki iliyopita.
 
Waziri Membe kwa niaba ya serikali ametoa salamu za rambirambi na kuchangia kiasi cha shilingi milioni  1, “Kwa niaba ya serikali tumechangia kiasi cha shilingi milioni 1. Hata mimi pia nilimfahamu marehemu kwa muda mrefu na alikuwa kiongozi makini, Mungu alilaze roho ya marehemu mahali pema peponi amen,” alisema Waziri Membe.
 
Mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa leo asubuhi kuelekea Zanzibar tayari kwa mazishi.
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 

HAYA TENA...... UCHOVU KITANDANI WAMFANYA MSANII HUYU WA KIKE WA BONGO MOVIE KUWACHUKIA WANAUME WA KIBONGO

Msanii  wa kike wa filamu bongo  maarufu kwa jina  la Husna Chobis ‘Avana’ amedai kuwa yeye hataki kuwa  na mwanaume wa kibongo kwa sababu wengi  wao ni waongo  na  hawayajui  mapenzi...
 
Akiongea  na  mwandishi  wetu, mrembo  huyo  alidai  kuwa  umaarufu  wake  humpa  wakati  mgumu  sana  wa  kumtambua  mwanaume  mkweli  maana  wengi  humtamani  kimapenzi  kutokana  na  jina  lake ( ustaa  wake )

  “Sitaki kuzalishwa   wala  kuwa  na  uhusiano wa  kudumu  na mwanaume  toka  Tanzania  maana  wengi  wao ni tapeli  na  hata  ukiwakubali   huwa hawajui  kitu . ALIFUNGUKA.....
 
"Bora kwa nchi za wenzetu kuna  ndoa za mikataba  kiasi  kwamba  mtu  unakuwa  unajua kabisa nitakuwa na huyu   kaka  kwa muda fulani , ntazaa  naye au ni wa raha tu.
 
"Hiyo  inasaidia  sana  kwa  sababu   kama huyo  kaka  ni   MSHAMBA inakuwa  ni  rahisi  kwako  kumpiga  chini  na  kuangalia  ustaarabu  mwingine”..alisema Avana

MTOTO WA DARASA LA SITA ACHAPWA NA MWALIMU WAKE HADI KUPOOZA MIGUU.... KISA ALIKUNYWA MAJI YA SHULE BILA RUHUSA...

MWANAFUNZI wa darasa la sita, Ismail Godfrey (13) anayesoma katika Shule ya Msingi Maendeleo  Sinuka iliyopo mkoani Kigoma amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya kudai  kutandikwa viboko  na Mwalimu Muige Joseph na kupooza miguu.

 Mtoto huyo ambaye kwa sasa anapata matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar baada ya kukosa matibabu ya kina mkoani Kigoma alipokutana na mwandishi wetu alikuwa na haya ya kusema:  
“Awali sikuwa na matatizo yoyote ya kiafya hususan katika viungo vya mwili, isipokuwa haya yalinipata baada ya kuchapwa fimbo na mwalimu wangu ndipo nikapooza ghafla.
Miguu ya mtoto Ismail iliyopooza.
 
“Tukio hili lilitokea mwezi wa tano nilipokuwa shuleni, nilipofika nilifungua bomba nikawa nakunywa maji kwa kuwa nilikuwa na kiu, ghafla mwalimu huyo alikuja na kuniambia kwa nini nachezea boma,  ndipo akaanza kunitandika viboko. 
 
 “Hapo hapo nikahisi viungo vyote vya mwili vimepoa na miguu ikapata ganzi, nikaanguka chini baada ya kukosa nguvu,” alisema Ismail.
 
Kutokana na tukio hilo baba wa mtoto huyo,  Godfrey Lucas aliitwa  na baada ya kuona Ismail yupo katika  hali hiyo ya kupooza miguu aliamua kumpeleka katika Hospitali ya Mkoa, Maweni, kupatiwa matibabu, huku akifanya juhudi za kumtafuta mtuhumiwa ambaye alikuwa amekimbia makazi  yake.

Ismail Godfrey.
 
Hata hivyo , kutokana na juhudi za kumtafuta kwa kushirikiana na wananchi walifanikiwa kumkamata mwalimu huyo katikati ya mji wa Kigoma na kumfikisha polisi ambapo alifunguliwa kesi kwa jalada namba  KIGO/RB/2269/013 17/3/2013 SHAMBULIO LA MWILI.
 
“Mtoto alianza kutokwa na vidonda miguuni ndipo nikaamua tuje hapa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na tukapokelewa na mtoto amelazwa wodi ya wagonjwa ya Kibasila,” alisema. 
 
 Hata hivyo, amesikitika kuachiwa mtuhumiwa kwa dhamana wakati  mwanaye bado kalazwa na anakosa masomo kwa sababu yake.

AJABU......KIGANJA CHA MKONO WA BINADAMU CHAKUTWA KWA MGANGA AKIMUUZIA MTEJA WAKE KWA KIASI CHA MILIONI 100 JIJINI MWANZA


Mtu mmoja jijini Mwanza anadaiwa kukamatwa na kiganja cha mtu akiwa anajiandaa kumuuzia mteja kwa sh million 100.

Washukiwa walikamatwa  jana  karibia na uwanja wa ndege wa Mwanza  wakifanya  biashara  hiyo  haramu....
 

 Baada  ya  upekuzi  wa  kina, mteja  alikuwa  ana  milioni  100  na mganga alikutwa  na   kiganja cha  binadamu  ambacho kilikuwa  kibichi kikitoa damu.

Kiganja  hicho  kilikuwa  kimevishwa  tunguri  na nywele za binadamu.

MAMBO YA LADY GAGA JUKWAANI LAIV BILA NGUO.....AKITUMBUIZA



         
       
Huyu  ni  msanii Lady Gaga  aliyeamua  kutoa  burudani   akiwa  uchi  wa  mnyama  katika show ya G-A-Y huko London, Uingereza Ijumaa iliyopita.

Gaga (27) alipanda jukwaani akiwa amevalia vazi linalomfunika hadi miguu lakini wakati akiendelea kuperform ghafla alianza kusaula taratibu kutokea juu hatimaye kulishusha vazi lote na kubaki uchi..

DAH... NGUMI ZAPIGWA KATI YA WADADA BARABARANI ETI KISA BWANA WANAEMGOMBANIA


Wadada wawili Warembo wa Mitaa ya kawe waliamua kuzichapa kavu kavu bila maglovsi mbele za watu kwa eti mmoja akimtuhumu mwenzie kuwa anatoka na Boyfriend wake...Inasemekana hawa madada ni marafiki sana lakini leo yamewashinda baada ya kuchangia bwana mmoja ...

UKATILI.. PANGA NA RUNGU VYATUMIWA NA BABA MZAZI WA MTOTO KUMWADHIBU KWA KOSA LA KUTOKWENDA SHULE HUKO MKOANI MBEYA

 
        
Victoria Mukama (10) baada ya matibabu
 
       Kabla ya matibabu
 
      
Mwalimu wa zamu wa Shule ya Msingi Airport, Damali Obadia alisema tukio hilo la ajabu lilitokea  majira ya saa mbili na nusu asubuhi ambapo akiwa ofisini alimuona mzazi huyo akiwa na mtoto huku akiendelea kumpiga wakielekea ofisini.
 
 
 
 Mama mzazi wa binti huyo Teodora Paulo alisema yeye na mume wake hawakuwepo nyumbani ambapo baada ya kurejea kutoka Msibani majira ya asubuhi walimkuta binti yao hajaenda shule na walivyomuuliza sababu ya kutoenda shule alijibu alikuwa havioni viatu vyake.
 
 
 
 majirani wa mtuhumiwa huyo walidai kuwa tabia ya Mwanaume huyo kufanya unyanyasaji inafichwa na mkewe ambaye anaonekana kuwa muoga wa kupigwa na mumewe na kuongeza kuwa anatabia ya kuandika makosa anayotendewa na mkewe
 
 
KATIKA hali isiyokuwa ya Kawaida, Baba mmoja aliyejulikana kwa jina la Oscar Mukama  mkazi wa Isengo Airport Jijini Mbeya amemjeruhi vibaya binti yake Victoria Mukama (10) kwa kumpiga sehemu mbali mbali za mwili wake akitumia vifaa vyake vya ulinzi likiwemo Lungu.

Kwa mujibu wa Mwalimu wa zamu wa Shule ya Msingi Airport, Damali Obadia alisema tukio hilo la ajabu lilitokea  majira ya saa mbili na nusu asubuhi ambapo akiwa ofisini alimuona mzazi huyo akiwa na mtoto huku akiendelea kumpiga wakielekea ofisini.

Alisema mzazi huyo baada ya kufika walimu walimpokea na kumuuliza kwa nini anampiga kiasi hicho mtoto wake alijibu mtoto ni wa kwake mwenyewe na alizaa kwa manufaa yake hivyo haoni sababu ya kuulizwa kuhusu kipigo kwa mwanaye.

Aliongeza kuwa baada ya walimu kumweleza kuwa kitendo alichokifanya ni cha kinyama na hakipaswi kutendeka Mzazi huyo alitoa kisu na kuwatishia walimu ikiwa ni pamoja na kutoa matusi makali dhidi yao ambapo walimu walifanikiwa kumtuliza na kumuomba amwache mtoto ili walimu wamwadhibu.

Alisema baada ya mzee huyo kuondoka na kumwacha mtoto walimpigia simu mama wa mtoto ambaye baada ya kufika shule alizimia kutokana na hali aliyomkuta nayo mtoto wake ambapo Walimu walitoa taarifa kwa Mwenyekiti wa Mtaa kasha kwenda Polisi kuchukua Fomu namba tatu (PF3) kwa ajili ya matibabu.

Mama mzazi wa binti huyo Teodora Paulo alisema yeye na mume wake hawakuwepo nyumbani ambapo baada ya kurejea kutoka Msibani majira ya asubuhi walimkuta binti yao hajaenda shule na walivyomuuliza sababu ya kutoenda shule alijibu alikuwa havioni viatu vyake.

Alisema baada ya kumsaidia kutafuta na kutofanikiwa kuviona baba yake ambaye nayeb alikuwa amejiandaa kwa ajili ya kwenda kazini kwake anakofanya kazi ya Ulinzi alimwamuru mwanaye kuvaa sare za shule na kwenda naye hivyo hivyo kwa kile alichodai anampeleka shule.

Alisema alishikwa na butwaa hadi kupoteza fahamu baada ya kumkuta mtoto amejeruhiwa huku akiwa amepigiwa simu na mumewe kwamba aende shule kumchukua mtoto wake lakini hakujua kama amepigwa kiasi cha kumjeruhi mtoto sehemu mbali mbali za mwili wake.

Akizungumzia kisa cha kupigwa kwake baada ya kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya katika Chumba cha dharula, Victoria Mukama (10) ambaye ni mwanafunzi wa darasa la nne katika Shule ya Msingi Airport alisema wakiwa njiani kuelekea shuleni alishangaa akianza kupigwa bila kuelezwa sababu ni nini.

Alisema alianza kupigwa tangu wanatoka nyumbani hadi wanafika shule iliyoumbali wa Mita 250 kutoka Nyumbani hadi Shuleni akitumia Virungu na fimbo huku akiwa ameshika kisu mkononi kwa ajili ya kuwatishia wanataka kumuokoa.

Kutokana na tukio hilo Jeshi la Polisi linaendelea kumtafuta Mtuhumiwa huyo wa unyanyasaji wa watoto baada ya kufunguliwa kwa jarada lenye namba MB/IR/9563/2013 katika kituo cha kati cha Polisi Mbeya.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa wa Pambogo Esia Edward ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa kamati ya Shule hiyo alisema kitendo kilichofanywa na mtuhumiwa huyo hitendo hakipaswi kufumbiwa macho hivyo ni lazima sheria ichukue mkondo wake kwa kuhakikisha vitendo hivyo vinakomeshwa ndani ya jamii.

Aliongeza kuwa hajawahi kusikia mtuhumiwa huyo kama amewahi kujihusisha na ukatili wa namna hiyo na kuongeza kuwa huwa anatoa ushirikiano vizuri katika ngazi ya mtaa na kuhudhuria vikao mbali mbali vinavyoitishwa pamoja na kuchangia mada.

Nao majirani wa mtuhumiwa huyo walidai kuwa tabia ya Mwanaume huyo kufanya unyanyasaji inafichwa na mkewe ambaye anaonekana kuwa muoga wa kupigwa na mumewe na kuongeza kuwa anatabia ya kuandika makosa anayotendewa na mkewe.

Walisema awali amewahi kuoa mke na kuzaa nae watoto watatu lakini mkewe huyo alikimbia baada ya kuona tabia ya unyanyasaji imezidi kutoka kwa Mwanaume huyo aliyetajwa kuwa ni jamii ya watu wa Mosoma Mkoani Mara ambako tabia kandamizi dhidi ya wanawake na watoto bado zinafanyika.

AJABU....MWIZI WA KUKU AVULIWA NGUO BAADA YA KUKAMATWA......AFUNGIWA NDANI YA TENGA NA WANANCHI TAYARI KWA KUCHOMWA MOTO



Huyu  ni  mkenya   aliyekuwa  ameiba  kuku.Wananchi  walipomnasa walimpa  kichapo  kikali  na  kisha  kumfungia  ndani  ya  tenga  la  kuku  kwa  ajili  ya  kumchoma  moto….

Wangali  katika  maandalizi  ya  kutafuta  petrol, polisi  waliwasili  eneo  la  tukio  na  kumuokoa  kwa  kumpeleka  kituoni

LESENI ZA MAFUTA NA GESI ZAPINGWA NA MNYIKA


WAZIRI Kivuli wa Nishati na Madini, John Mnyika, amemtaka Rais Jakaya Kikwete kusitisha mzunguko wa nne wa utoaji wa leseni za utafutaji wa gesi asili na mafuta hadi sera na sheria ya gesi asili zikamilike, na marekebisho ya sera ya nishati na sheria za mafuta yafanyike. 

Mnyika ambaye pia ni mbunge wa Ubungo (CHADEMA), alisema hatua hiyo ni kurejea maoni na mapendekezo aliyoyawasilisha bungeni kwa niaba ya Kambi Rasmi ya Upinzani Mei 22 mwaka huu.
 
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, alisema rais anapaswa kuchukua hatua hiyo kwa kuzingatia kwamba Mei 25 mwaka huu, badala ya kushughulikia mapendekezo hayo, Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo alitoa majibu ya uongo na upotoshaji bungeni kuhusu masuala mbalimbali.
 
“Aidha Ikulu inapaswa kueleza iwapo Baraza la Mawaziri chini ya Rais Kikwete ndilo lililofanya uamuzi wa kuendelea na mchakato wa kutoa leseni za vitalu vya utafutaji wa gesi asili bila ya kuwepo kwa sera ya gesi asili na sheria ya gesi asili, na sera ya nishati na sheria zinazohusu mafuta au ni maamuzi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) na Wizara ya Nishati na Madini,” alisema.
 
Mnyika aliongeza kuwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda anapaswa kueleza iwapo kauli ya kejeli, dharau na uongo ya hivi karibuni iliyotolewa na Waziri Muhongo, kwamba uwezo wa wafanyabiashara wa Tanzania ni kuwekeza kwenye soda na juisi, si kwenye sekta ya gesi, ni msimamo wa serikali au maoni ya waziri binafsi.
 
“Izingatiwe kwamba Wizara ya Nishati na Madini, kupitia Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC), imetangaza mzunguko wa nne wa utoaji leseni za utafiti wa gesi asili na mafuta katika vitalu nane ndani na nje ya maji ya Ziwa Tanganyika vyenye ukubwa wa kilomita za mraba elfu tatu kila kimoja utakaofanyika Oktoba 2013.
  
“Serikali pia imetenga mipaka ya vitalu viwili kwenye bahari kuu, na kuingia ubia wa utafiti na kampuni inayoitwa mbia wa kimkakati (Strategic Partner) ambae serikali haijamtaja,” alisema.
 
Alisema mchakato huu unafanyika wakati taifa likiwa halina sera (mchakato wa kuiandika bado unaendelea) na hatimaye yaanze maandalizi ya kupata sheria mahususi za kusimamia sekta ndogo ya gesi, hatua ambayo inapaswa kuambatana na marekebisho ya kisera na kisheria ya sekta.
 
Aliongeza kuwa tayari Tanzania imeshafanya ugunduzi wa futi za ujazo zaidi ya trilioni 32 za gesi katika maeneo kadhaa nchini, hivyo kuifanya kuwa kati ya nchi vinara wa gesi nyingi Afrika na duniani.
 
“Utajiri huu wa gesi hadi sasa hauna sera wala sheria zinazotoa mwongozo wa usimamizi na udhibiti wake, ili kuhakikisha unawanufaisha Watanzania, kuepuka makosa yaliyofanyika katika uwekezaji mwingine wa gesi asili na rasilimali nyingine uliofanyika bila mifumo thabiti,” alisema.

MKE WA MTU ANASWA AKIJIUZA HUKO BUGURUNI

 
Mchumba huyo wa mtu aliyejitambulisha kwa jina moja la Diva alitoa kali ya mwaka baada ya kuzimia ghafla huku akitokwa na mapovu kinywani baada ya kunaswa  akijiuza.
  
Tukio hilo lilitokea wiki iliyopita maeneo ya Kimboka, Buguruni, Dar ambapo msichana huyo pamoja na ‘madadapoa’ wenzake walikuwa wakifanya biashara hiyo haramu bila kificho.
 
Mara baada ya kuona wenzake wakiwa mikononi mwa nguvu za dola katika kamatakamata ya polisi, mrembo huyo ambaye baadaye alijitambulisha kama mchumba wa mtu, alianguka ghafla na kuzimia kiasi cha kuzua hofu miongoni mwa machangu wenzake walioangua kilio wakidhani mwenzao amekata ringi (kufa).
 
Baada ya muda msichana huyo alirejewa na fahamu akiwa mikononi mwa polisi na kuanza kuangua kilio akiomba asikamatwe kwa kuwa yeye ni mchumba wa mtu na atakuwa kwenye wakati mgumu kama mchumba’ke atajua anajiuza.


“Naomba msinikamate. Mimi ni mchumba wa mtu afande. Mtaniweka kwenye wakati mgumu kama akijua nilikuwa nikijiuza. Jamani nitamkosa mchumba wangu Luka,” alisema mrembo huyo huku akiomba maji ya kunywa.
 
Hata hivyo, kilio chake hakikuwazuia  waandishi  kufanya kazi yake ndani ya Kituo cha Polisi
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DODOSO - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger