Wafanyakazi wa mamlaka ya Usalama wa baharini nchini Afrika Kusini wakiwa katika harakati za kusogeza mzoga wa Nyangumi nchi kavu kwa ajili ya kwenda kuzika.
Sehemu
kubwa ya pwani ya Afrika Kusini imefungwa kufuatia mzoga wa nyangumi
mwenye ukubwa wa mita 30 kusukumwa na maji pembezoni mwa fukwe na kuanza
kushambuliwa na jamii ya papa weupe.
Mzoga
wa nyangumi huyo umelazimika kuondolewa haraka ufukweni ulikokuwa
ukielea, kwa kuwa ulikuwa ukifukuziwa na papa weupe kadhaa walio ugeuza
kitoweo na kuhatarisha maisha ya watu.
Mamlaka
husika zimechukua hatua ya kuuondoa mzoga huo lakini pia imefunga
mtandao wa fukwe hizo kuanzia Muizenberg hadi Monwabisi kwa tahadhari.
Mzoga wa Nyangumi ukipimwa urefu.
Mashine Maalum ya kubebea vitu vizito kama Makontena ikifanya kazi ya kusomba mzoga huo.
Jitihada za kumbeba Nyangumi huyo kwa kutumia mashine maalum za kubebea makontena zikiendelea.
Nyangumi akiwa tayari amepakiwa kwenye Lori.
Safari imeanza ya kumsafirisha Nyangumi huyo sehemu kunakohusika.
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.