Idd Amin Dada.
Mwenyekiti
wa kamati ya Taifa ya Tuzo na Medali nchini Uganda Jenerali Elly
Tumwine ameweka wazi kuwa katika tuzo za heshima zilizotolewa kwa marais
waliowahi kuingoza nchi hiyo pamoja na watu wengine ambao mchango wao
unatambulika..
Aliyewahi kuwa rais nchini humo Hayati Field Marshal Idi
Amin Dada hakupata heshima kwa sababu aliacha urithi wa mfumo mbaya
wakati wa uongozi wake.
Marais
wote wametunukiwa Medali za Miaka 50 ya Uhuru wa Uganda wakati wa
maadhimisho ya sherehe za chama cha NRM kutimiza miaka 27 yaliyofanyika
wilaya Kasese, ambapo rais Yoweri Museveni alipokea medali ya, sambamba
na watu wengine 43.
Jumla
ya watu 3,500 nchini Uganda watapokea tuzo hiyo ambayo inawatambua mtu
mmoja mmoja kwa mchango wake katika kutoa huduma na uzalendo kwa nchi
hiyo tangu ilipopata uhuru.
Jenerali Tumwine amesema Amini hakutambuliwa kwa sababu ya mfumo mbaya alioutumia wakati wa uomgozi wake.
Amini
alikuwa rais wa Uganda kutoka mwaka 1971 hadi 1979 ambapo aliingia
madarakani kwa kupindua serikali ya Milton Obote Januari 1971.
Marais
wengine wote waliopita wakiwemo Sir Edward Mutesa, Obote, Yusuf Lule,
Godfrey Lukongwa Binaisa na Gen. Tito Okello, wametunukiwa medali hizo
za heshima.
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.