Home » , » "NINA MPANGO WA KUWAFUFUA WASANII WALIOPOTEA KATIKA GEMU"..DULLY SYKES

"NINA MPANGO WA KUWAFUFUA WASANII WALIOPOTEA KATIKA GEMU"..DULLY SYKES

tangazo
Dully Sykes ni miongoni mwa wasanii wakongwe wa Bongo Flava waliobahatika kuendelea kubaki juu kiasi cha kufanikiwa kuwa mmiliki wa studio mbili za kurekodi muziki.


Msanii na producer huyo wa Bongo Flava, hivi karibuni ameanza kuwasaidia wasanii wenzake walioanza muziki pamoja ambao kwa sasa wamepotea.

Dully aka Mtoto wa Kariakoo amemchukua Inspekta Haroun ambaye atakuwa chini ya menejimenti yake na studio anayoimiliki ya 4.12. Tayari wasanii hao wameshatoa ngoma ambapo Inspekta amemshirikisha Dully kwenye wimbo uitwao Ashura.

Wasanii wengine ambao hitmaker huyo wa Utamu Utamu amepanga kuwatoa tena ni pamoja na Mack D na kundi la Manzese Crew na pia akiongea na XXL ya Clouds FM jana, staa huyo alisema hivi karibuni ataachia wimbo mpya aliowashirikisha AY na Jokate Mwegelo.

Tupe Maoni yako!

KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DODOSO - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger