Mwanamke: Dalili zitakazomfanya mpenzi mpya akuone wewe ni king’ang’anizi…!
Hizi
ni miongoni mwa sababu ambazo wanaume wengi huchomoa mapema kwa wapenzi
wao wapya kabla uhusiano haujashika kasi. Kuna wakati wanawake hukosea
na kuvuka mipaka mwanzoni tu mwa uhusiano. Anamganda mwanaume haraka
sana au anaonesha dalili zote za kujipendekeza kupita kiasi. Lakini
jambo ambalo wanawake wengi hawalijui ni kwamba, wanaume wako makini
sana kuwakwepa wanawake ving’ang’anizi……..
Nitadadavua baadhi ya vijitabia vya wanawake vinavyowafanya wanaume wawaone kama ni ving’ang’anizi…..
1. Unataka kuwa naye muda mwingi kuliko kawaida… Ni
vizuri kwa wapenzi wapya kupata fursa ya kuwa pamoja peke yao, lakini
kama unakataa kuwa na mtoko, kuhudhuria sherehe au kukutana na marafiki
na kulazimisha kuwa pamoja peke yenu mahali fulani pa faragha, basi hapo
ni lazima mwanaume atadhani kwamba unataka akupe umuhimu wa pekee muda
wote. Unaweza kukuta mwanamke anakuwa king’ang’anizi kiasi kwamba hana
muda na marafiki zake au watu wengine isipokuwa mpenzi wake. Anakuwa
kama mzigo, muda wote yuko nyuma ya mwanaume kila anapokwenda…. Hapa ni
lazima mwanaume atatemana na wewe kungali mapema. Hakuna mwanaume
anayeweza kujenga mahusiano na mwanamke wa aina hii, watakukimbia kila
siku.
2. Unampangia mwanaume kila kitu… Unampangia aina ya mavazi ya kuvaa, unaanza kuboresha mazingira ya nyumbani kwake haraka sana kwa kununua vitu mbalimbali vya nyumbani kwake bila kushauriana naye. Hiyo ni dalili kwamba una matarajio makubwa kwake, jambo ambalo kwake yeye bado halijamuingia akilini. Hapa mwanaume ambaye huyachukulia mambo kwa tahadhari, hukuona kuwa wewe ni king’ang’anizi na unataka kukita mizizi kwake wakati bado anachunguza uhusiano wenu ili kujua iwapo utakuwa kama vile anavyotarajia yeye… Kumbuka kwamba kila mtu ana sifa azitakazo pale anapochagua mwenza, na ni vigumu kumjua mtu kwa muda mfupi. Kunahitajika muda wa kutosha mtu kumjua mwenzake vizuri linapokuja swala la mahusianao.
3. Unatumia muda mwingi zaidi kukaa kwake…. Unalala
kwa mpenzi wako, na asubuhi mwanaume huyo anaondoka kwenda kwenye
shughuli zake, na wewe unabaki labda ukidai unamsaidia usafi kidogo.
Lakini anaporudi jioni anakukuta bado uko hapo nyumbani kwake ukiwa
umejipumzisha. Inawezekana ukawa umeandaa chakula cha usiku tayari na
pia huenda ukawa umebeba nguo za kubadilisha kwenye mkoba wako pamoja na
vipodozi ukiwa umejiandaa kulala tena hapo kwake. Huonyeshi dalili za
kuondoka hapo kwake zaidi ya kwenda kwako au kwenu na kubadilisha nguo
na kuchukua viti vichache utakavyovihitaji utakapokuwa hapo kwake,
lakini unapanga hayo yote bila kumshirikisha zaidi ya kukuona tu
ukimganda kama luba. Huonyeshi kuwa na maisha yako kama wewe, zaidi ya
kujipachika kwake……
4. Unajenga urafiki na mama yake haraka sana…… Baada
ya kukutambulisha kwa mama yake na kubadilishana namba za simu au labda
na email, unaanza kujenga ukaribu na mama yake kupita kiasi. Wanawake
wengi hudhani kwamba, iwapo watajenga urafiki na mama wakwe watarajiwa,
basi itakuwa rahisi kwao kumnasa mwanaume huyo, maana huamini kwamba
watoto wa kiume hawawezi kwenda kinyume na mama zao linapokuja swala la
kuchagua mwenza. Kwa kawaida wanaume humuona mwanamke anayejipendekeza
kwa mama yake kama vile anataka kulazimisha uhusiano au ndoa, hivyo
humchukulia kama ni king’ang’anizi.
5. Unampigia simu na kumuuliza kama yuko wapi….. Unapompigia simu badala ya kumjulia hali unakuwa na maswali ya kipolisi.. ‘Uko wapi?’ ‘Unafanya nini? Maswali
ya aina hiyo mwanaume huyachukulia kama ya kimtego na hawafurahishwi
nayo. Wanawake wengi huamini kwamba wanaume huwa hawasemi ukweli kuhusu
mahali walipo pale wanapoulizwa na wenzi wao. Jambo hilo linaweza kuwa
kweli au lisiwe kweli. Inawezekana kuwa kweli kwa sababu labda ya
wanaume kukwepa maswali mengi. Mara nyingi wanawake hawaridhiki na jibu
moja. Mfano ni jioni ndio ametoka kazini, lakini nakapitia mahali fulani
kukutana na rafiki yake, inawezekana ikawa ni kwenye mghahawa au kwenye
baa. Kama mwanamke akipiga simu na mwanaume akamwambai yuko kwenye baa
na rafiki yake, yatafuata maswali lukuki. Hakuna mwanaume anayependa
kuulizwa maswali mengi kama vile anatuhumiwa. Na ndio sababu wanaume
wengi wanakwepe kusema mahali walipo. Kwa hiyo ili kuepuka maswali
anaweza kujibu kwa kifupi tu kwamba yuko kwenye kikao kazini na hatakuwa
hewani, ili apate nafasi ya kuzima simu japo kwa muda. Mwanaume humuona
mwanamke mwenye udadisi wa aina hiyo kama king’ang’anizi.
6. Unakuwa na chuki na wanawake wenzako… Pale
ambapo mwenzi wako anapomtaja mwanamke fulani, inaweza kuwa ni
mfanyakazi mwenzake, mke wa kaka yake au mtu wanayeshirikiana
kibiashara, unaonyesha kisirani cha waziwazi kwamba unakerwa na ukaribu
wake na wanawake wengine. Tabia hii inaashiria kwamba wewe unapenda
kumiliki na wanaume wengi huwa hawapendi wanawake wenye vijitabia vya
kupenda kumiliki. Hapo ni lazima utaonekana kuwa wewe ni king’ang’anizi
na uhusiano wenu utavunjika mapema…..
7. Unakubali kila analosema au kila anachokifanya….Kuna kitu kinaitwa ‘uhusiano wa kinyonga.’ Hapa
mwanamke anajibadili kupita kiasi ili afanane na mwenzi wake. Unakuta
mwanamke anakubali kila kitu anachokiamini mwenzi wake bila kuhoji.
Anapoteza utambulisho wake na kujipachika utambulisho wa mwenzi wake.
Mwanaume akikuona uko hivyo, atakukimbia, atajua wewe ni king’ang’anizi
8. Unawazungumzia mabwana ulioachana nao kila wakati…Kama
una kawaida ya kumzungumzia mwanaume uliyeachana naye mara kwa mara
uwapo na mpenzi wako mpya, ina maana kwamba bado hujaachana na jakamoyo
la kuachwa. Hakuna mwanaume anayependa kusikia kuhusu mahusiano yako ya
nyuma, kwa sababu hayamuhusu. Kama ukiwa unapenda kumzungumzia mpenzi
wako wa zamani kila uwapo na mpenzi wako mpya, jua kwamba na yeye pia
utampoteza kwa sababu atakuona kuwa wewe ni dhaifu na king’ang’anizi na
ndio maana umeshindwa kusimama kama wewe, na badala yake unawaza kuhusu
mtu uliyeachana naye pamoja na kwamba uko naye. Sio kwamba ni vibaya
kumzungumzia mpenzi mliyeachana, lakini ni vyema kama utamzungumzia pale
ambapo kuna ulazima sana wa kufanya hivyo, labda kuna jambo ambalo
limamhusu ambalo mnajadili, na ikakulazimu kumtaja…..
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.