Mwanaume mmoja wa Jiaxing, China amejikuta akichukua uamuzi mgumu wa
kujikata uume wake baada ya nyota yake ya bahati katika mapenzi
kushindwa kung’aa katika anga la maisha yake, kiasi cha kumfanya akate
tamaa na kuamua kuchukua uamuzi huo.
Baada ya kujikata kiungo hicho muhimu katika mwili wa mwanaume,
mchina huyo Yang Hu mwenye miaka 26 aligundua kwamba haikuwa ndoto ni
kweli ameukataa uume wake, ndipo alipochukua baiskeli yake na kukimbia
hospitali kwa matarajio ya kwenda kuunganishiwa kiungo chake
alichokikata mwenyewe.
Sipati picha aliwezaje kunyonga ‘pedal’ za baiskeli yake mpaka
hospitali ilihali maumivu makali aliyokuwa nayo, lakini mbaya zaidi
kutokana na kuchanganyikiwa kwa alichokifanya, baada ya kufika hospitali
ndipo ndoto zake zikazidi kufifia baada ya madakrati kumueleza kuwa
amesahau kuja na kiungo hicho ili kirudishiwe sehemu yake.
Hu alinyonga baiskeli yake tena kwa haraka kurudi nyumbani kuuchukua
uume wake aliousahau na kurejea tena hospitali, lakini madaktari wakampa
taarifa mbaya kuwa kutokana na kiungo hicho kutenganishwa na mwili na
kukaa muda mrefu bila kuwa na damu haitawezekana tena kukiunganisha na
mwili.
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.