Home » , , » "BONGO FLEVA IMEFULIA"....MAD ICE

"BONGO FLEVA IMEFULIA"....MAD ICE

tangazo

Msanii wa kimataifa kutoka Tanzania aishiye nchini Finland, Mad Ice amesema ladha ya Bongo Flava imebadilika kwa kiasi kikubwa kutokana na wasanii kutaka kucopy style za wasanii wa nchi zingine husasan Nigeria na Afrika Kusini.


“Jana nilikuwa na mtu mmoja anaitwa Man Razor tulikuwa kwenye interview radio, Dj Tass alipiga kwanja za nyuma ile miaka yetu tunaanza 2002/03 akapiga track zile zote, nikasema kweli muziki umebadilika sana, ladha imepotea, ile ladha ya Bongo Flava ya mwanzo ile, na nikajiuliza ni kwanini. 

Jamaa akaniambia ‘sikiliza vizuri kazi zinazofuata’, kuna flava ya kinaijeria, sijui South Africa sijui wapi, akaniambia ‘unajua tatizo ni kwamba vijana wakisikia wamehit P-Square naye anakambilia anakwenda kwa producer nitengenezee track kama ile,” Mad Ice

Amesema tatizo hilo linachangiwa pia na mashabiki ambao huzipenda nyimbo za wasanii wa Nigeria na hivyo kuwafanya wasanii wengi hasa wanaotegemea muziki kuiga style hizo ili kupata shows zaidi.

“Ni wachache walio na msimamo kwamba mimi natengeteza kazi mimi kama mimi, I don’t care mtu mwingine anafanya kitu gani.”

Mad Ice yupo nchini kwa siku kadhaa sasa na Jumamosi anatarajiwa kuwa na show visiwani Zanzibar.

Tupe Maoni yako!

KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DODOSO - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger