Hiki kinaweza kuwa kituko cha mwaka kwenye muziki wa Bongo Flava. Mrembo aliyeigiza kwenye video ya Linex Aifola, ameamua kumfungulia RB msanii huyo baada ya kumpiga kibao cha kweli kwenye video hiyo.
Katika video hiyo Linex anaonekana akiwa amekaa kwenye kochi na kuanza kukagua simu ya mchumba wake Aifola ambaye humo ameigiza Janeth Bundala na ndipo alipogundua kuna meseji za kimapenzi anazotumiwa na mwanaume mwingine kiasi cha kuchukia na kumpiga kofi kali la shavuni.
“hahhahahahhahaha frm no where eti janeti aka aifola kanipigia leo kaniambia kanichukulia R B kwa kofi nililompiga wakati tunaigiza hahah kama kachelewa hv,” aliandika Linex jana kupitia Facebook.
“Sijajua alikua anatania but ndo kitu alichoniambia muda si mrefu
nimekia nacheka tu. Nimemsikia live radion anataka kulipwa aseeee kumbe
anamaanisha. Nimeshaongea nae na kesho ndo nakutana nae rasmi ntajua
anatakaje na ntamalizana nae.”
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.