Mrembo, mtangazaji na mjasiriamali wa nchi Tanzania Jokate Mwegelo leo
ameizundua rasmi kampuni yake ya Kidoti Loving katika hafla iliyofanyika
Serena Hotel jijini Dar es Salaam.
Bidhaa za kwanza za Kidoti zilizoingia sokoni ni Nywele (weaving)
ambazo amesema tayari zinapatikana katika soko la Kariakoo na maeneo
mengine jijini Dar es Salaam ambapo baada ya muda mfupi zitaanza
kupatikana mikoani.
Amesema kwa kuanzia kampuni yake imeanza kwa kutengeneza nywele za
aina nane ambazo zinapatikama kwa bei ya kawaida ili kuwawezesha
watanzania wengi kupendeza kwa gharama nafuu.
“Hizi nywele mabibi na mabwana zimefanyiwa utafiti kwa takriban mwaka mzima,” alisema Jokate.
“Ni nywele safi zenye ubora wa hali ya juu, hazifungamani, zipo
katika mawimbi, rangi na style za kisasa, ni nyepesi, rahisi kusukia,
laini, zinadumu kwa muda mrefu na muhimu kuliko yote zipatikana kwa bei
nafuu sana.”
“Ni bidhaa ambazo naweza kusema confidently zinamfaa mwanamke wa kisasa.”
Jokate amesema utengenezaji wa nywele hizo ameusimamia mwenyewe na kwa msaada wa timu yake ya Kidoti.
Hizi ni baadhi ya picha za tukio hilo.
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.