Home » , , » STEVEN NYERERE AANDAA TAMASHA LA KUMUENZI BABA WA TAIFA

STEVEN NYERERE AANDAA TAMASHA LA KUMUENZI BABA WA TAIFA

tangazo


Jumapili ijayo ya tarehe 14, October ni ‘Nyerere Day’ ambayo hutumika kumuenzi hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Kutokana na siku hiyi msanii wa filamu na mchekeshaji nchini, Steve Nyerere amesema ataitumia kuandaa tamasha la kumuenzi baba wa taifa.


“Nyerere Day ni tarehe 14 itaangukia siku ya Jumapili mimi kama mimi nimeamua kutengeneza kitu ambacho kitakuwa kina mkumbuka mwalimu Nyerere kitu hicho kitaonyesha filamu yangu ya mwalimu Nyerere pale Sunrise Kigamboni,” Steve ameiambia Movie leo ya Clouds FM.

“ Nitaalika watu na watu wengine ambao watapenda kujumuika na familia watoto wa bibi na mabwana basi wanakaribishwa Sunrise kuja pale Sunrise Kigamboni na vilevile jioni nitaonyesha filamu ya Mwalimu Nyerere, kutakuwa kuna viongozi mbali mbali tutaalika, kuna viongozi wa kidini tutawaalika na vilevile nitapeleka hata kwenye viongozi wa Serikali kwasababu Nyerere day kwa sasa hivi kitaifa ina fanyikia Shinyanga, sasa kwa Dar es salam hapa tupo tunamwenzi lakini kumwenzi zaidi Steve kama Steve ndiyo maana nimeamua kuifanya huko Sunrise na wananchi wa Kigamboni nao wameomba kweli lazima kuwe na kitu fulani.”

“Kwahiyo Sunrise wameamua kunipa support na mimi sikuweza kuikataa hiyo support nitakuwa na baadhi ya wasanii wa filamu ambao wamecheza hii filamu ya mwalimu Nyerere kwahiyo nao nita kuwanao katika kufanya usiku huwo ya tarehe 14 kwa kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kwasherehe zaidi,”aliongeza.

“Kwa wale ambao nitakuwa nimewapa kadi kuna kadi ambao nitawapa za free kadi ambazo zitatoka kama 50, na zingine tutachangia pale kama 5,000 hivi.”

Tupe Maoni yako!

KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DODOSO - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger