Kwa wale walioondoka mapema kwenye show ya Fiesta usiku wa kuamkia
Jumapili baada tu ya Rick Ross kumaliza performance yake, walikosa
kujionea kituko kilichofanywa na Diamond Platnumz. Ama wengine wamekuja
tu kuona picha zilizosambaa kwenye internet.
Akiwa stage na madancer
wake wakati show imepamba moto, Diamond aliamua kuvua na kuonesha boxer
yake nyeupe kama ishara kuwa yeye na madansa wake ni ‘wasafi’ kiasi cha
kutoogopa kuionesha hadharani.
Bahati mbaya watanzania wamemuelewa tofauti. Kitendo hicho kimewakera
wengi.
Kwa mujibu wa maoni tuliyoyapata kupitia ukurasa wetu wa
Facebook baada ya jana kuweka picha hiyo, wengi wameitafsiri picha hiyo
kama ishara ya ‘ushoga’ na huku wengine wakienda mbali zaidi na kuibua
tena mada ya ufreemason. Haya ni baadhi ya maoni.
“Wanaonyesha kuwa na mapepo hao maana walianza na kuvua magoti hadi
mashati wakabakiza suruali , sasa wamebakiza boxer unadhani wakishatoa
boxer watabakiza nini, huo ni ushirikina na muda si mrefu watahumbuka
hao maana naona ule mwisho wao umeshafika; hizo ni akili ama matope…wana
akili ama matahairaaaaa1.”
“Ndio maana wazee wetu hawaupend kuusikiliza huu muzk munaoita bongo
flava. Uchafu kama huu mnafanya mbele za watu au umaarufu unatafutwa kwa
kila njia,basi huyo tanzanite awe john elton wa bongo.”
“Lbd alielewa tofauti,alpockia MUONEKANO MPYA BURUDAN ILEILE ndani ya
fiesta!!nd mana akafanya hcho k2ko lkn pia mayb woz search and luking
fo huzband! nadhan co rdhk nyota uyu.teh teh teh shame upon hiz
unimpressive kboxa.”
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
