BABA mzazi wa staa wa sinema za Kibongo ambaye pia ni Miss Tanzania 2006/2007 Wema Sepetu, Balozi Abraham Isaac Sepetu ameagwa jana jioni nyumbani kwake Sinza - Mori jijini Dar es Salaam.
Tukio hilo lilihudhuria na viongozi
mbalimbali wa kiserikali akiwemo Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph
Warioba, Getrude Mongela pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Kimataifa Benard Membe na wengine wengi waliofika kutoa heshima za
mwisho kwa mwili wa marehemu aliyefariki dunia Jumapili ya wiki
iliyopita.
Waziri Membe kwa niaba ya serikali ametoa
salamu za rambirambi na kuchangia kiasi cha shilingi milioni 1, “Kwa
niaba ya serikali tumechangia kiasi cha shilingi milioni 1. Hata mimi
pia nilimfahamu marehemu kwa muda mrefu na alikuwa kiongozi makini,
Mungu alilaze roho ya marehemu mahali pema peponi amen,” alisema Waziri
Membe.
Mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa leo asubuhi kuelekea Zanzibar tayari kwa mazishi.
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.