Kuna
wakati wanaume hudhani kwamba, wanawake wanaovaa nusu uchi huwa
wanafanya hivyo kwa sababu ya kutafuta soko kwa wanaume. Inawezekana
kukawa na wale ambao wana sababu hizo, lakini wapo wale ambao wanalipa
fidia kutokana na kuamini kwao kwamba, sura zao zimewaangusha, hivyo
miguu yao mizuri inabidi kuziba pengo au udhaifu huo.
Wakati
mwingine hata wanawake wanaodhani au kudhaniwa kuwa ni wazuri, wamekuwa
wakivaa nguo fupi zinazoonyesha maungo yao. Hawa nao ni lazima wanalipa
fidia ya kasoro fulani waliyo nayo. Inawezekana wameshindwa kulinda
ndoa zao, au inawezekana hawajaolewa na sasa wanataka kuonyesha kwamba,
pamoja na kutoolewa kwao, bado wao wana sura na miguu au miili mizuri.
Udhaifu
wowote ambao unamkera mwanamke iwe ni wa moja kwa moja au kupitia nyuma
ya ubongo wake, unaweza kuonyeshwa kwa mwanamke huyo kuyatangaza yale
maeneo ya mwili wake ambayo anaamini ni mazuri. Kuyatangaza huko humpa
ahueni kwa kuamini kwamba bado anayo thamani, kwani ataangaliwa sana na
wanaume, kusifiwa na pengine kutongozwa.
Hebu
angalia wanawake ambao wanavaa nguo za kubana huku wakiwa na makalio
makubwa. Hawa mara nyingi wana sura ambazo wao au wengi huamini kwamba
ni mbaya. Huvaa nguo hizi ili kuonyesha kwamba, pamoja na ubaya wa sura
zao, bado wao ni wazuri sana katika maeneo mengine ya mwili ambayo
wanaume na hata wanawake wengi huyapenda au kutamani kuwa nayo.
Wengi hawavai tu nguo hizi za kubana kwa sababu ni fasheni, la hasha, wengi hili ni kimbilio la udhaifu wao.
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.