Ngoja leo niyadadavue makosa yanayofanywa na wanawake wengi pale wanapoamua ni nani wa kuoana naye:
1. Kosa la kwanza,
unaolewa na mtu ambaye unajua kabisa ni dhaifu na mkorofi, ukitarajia
kwamba ataondoa kasoro zake akiwa ndani ya ndoa. Hili ni kosa kubwa.
Kama huna furaha sasa na mtu kabla hujaoana naye, usikubali kuingia huo
mkenge. Huwezi kutegemea mtu kuadilika aiwa ndani ya ndoa.
2. Kosa la pili,
unaolewa na mtu asiye sahihi kwa sababu ya msisimko wa mwili kimapenzi
lakini si kwa sababu ya tabia zake. Kuwa mwangalifu na neno “Nakupenda”
neno hili mara nyingi maana yake ni “Nina uchu nawe.” Ndiyo amevutiwa
nawekimaumbile, lakini undani wa tabia yake unaujua? Hapa kuna mambo
manne… Kwanza, Je anapenda kutomfanyia binadamu mwenzie mabaya kama
mabavyo yeye hataki kufanyiwa? Pili, anaishi vipi na watu wengine?
Anaishi vipi na watu ambao ana uadui nao, Anawasamehe au analipiza
visasi? Je anatoa misaada kwa masikini? Tatu, je ni mkweli, anachokisema
ndicho anachokifanya? Je anaaminika? Majukumu anayoahidi kuyafanya
anayatimiza? Nne, je anajipenda? Je ni mtu ambaye yuko imara kimapenzi
au ni mtu wa kuyumbayumba na asiye na msimamo? Sio mtu akishauriwa na
marafiki zake au ndugu zake huko, anakuja na maamuzi yasiyo na kichwa
wala miguu
3. Kosa la tatu,
unaolewa na mtu ambaye hamna malengo na vipaumbele vya aina moja vya
maisha. Je mna utashi wa aina moja? Kwa mfano ni vyema mwanamuziki
akaolewa na mwanamuziki mwenzie kwa kuwa anajua mzingira ya kazi ya
mwenzie ili kupunguza wivu wa kupindukia usio wa lazima
4. Kosa la nne,
unaolewa na mtu asiye sahihi kwa sababu mnakutana kimwili mapema mno.
Kukutana kimwili kabla ya ndoa kunaweza kuleta matatizo makubwa mno.
Tendo la ndoa kabla ya ndoa hufunika uwezo wa mtu kufikiri. Mtu anabaki
kufaidi na kubaki kujali mapenzi ya kimwili na kusahau kukuna ubongo juu
ya mambo mengine. Ni lazima mwanamke akune ubongo ili kujua kama huyo
mpenzi anakidhi vigezo vyote vya mume mtarajiwa.
5. Kosa la tano,
unaolewa na mtu ambaye huna msisimko wa kimwili umwonapo. Kuna
uwezekano mkubwa mwanamke akavutiwa na mwanaume kwa sababu ya aina ya
gari analomiliki. Hapa hakuna msisimko wa kimwili bali mwanamke kavutwa
na gari au rasilimali alizo nazo mwanaume huyo.
6. Kosa la sita,
unaolewa na mwanaume anayependa kudhibiti. kuwa na tabia ya kudhibiti
wenzako ni ya dalili za mtu jeuri na mwenye kujisikia na mfujaji. Naomba
kutofautisha kati ya “kudhibiti” na “kutoa mawazo.” Mtu anayekupa
mawazo ni kwa faida yako, lakini anayekudhibiti ni kwa faida yake.
7. Kosa la saba,
unaolewa na mtu asiye sahihi kwa sababu unakimbia matatizo uliyo nayo.
Unaweza kuwa hujaolewa na huna raha wala amani na ukataka kuolewa. Ndo
haiwezi kukutatulia matatizo yako binafsi ya kisaikolojia nay a
kimapenzi. Badala a kuyapunguza matatizo hayo, ndoa itayaoneza. Kama
huna amani na huyafuahii maisha, chukua jukumu la kurekebisha matatizo
hayo sasa kabla hujaolewa. Itakuwa ni faida kwako na kwa mmeo mtarajiwa.
8. Kosa la nane,
unaolewa na mtu asiya sahihi kwa kuwa yuko ndani ya pembe tatu. Mtu
ambaye anaishi na wazazi wake ni moja ya mfano wa mtu anayeishi katika
pembe tatu. Watu wengine wanaoweza wakawa wanaishi ndani ya pembe tatu
ni kama wanaofanya kazi saa 24! Huyu mtu halali? Watu wengine walio
katika pembe tatu ni watu wanaotumia madawa ya kulevya, mtu
anayetawaliwa na “hobbie” zake, anapenda sana michezo (Mpira), kuperuzi
mitandao ya kijamii na anapenda sana fedha. Hakikisha kwamba wewe na
mpenzi wako , nyote hamtawaliwi na pembe tatu. Mtu ambaye anatawaliwa na
pembe tatu hawezi kumtimizia mpenzi wake haja ya upendo atakapokuwa
anahitaji. Kama mpenzi wako anatawaliwa na pembe tatu kwa kiasi kikubwa,
wewe huwezi kuwa kipaumbele chake.
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.