
Kuna
wakati wanaume hudhani kwamba, wanawake wanaovaa nusu uchi huwa
wanafanya hivyo kwa sababu ya kutafuta soko kwa wanaume. Inawezekana
kukawa na wale ambao wana sababu hizo, lakini wapo wale ambao wanalipa
fidia kutokana na kuamini kwao kwamba, sura zao zimewaangusha, hivyo
miguu yao mizuri inabidi kuziba pengo au udhaifu huo.
Wakati
mwingine hata wanawake wanaodhani au kudhaniwa kuwa ni wazuri, wamekuwa
wakivaa nguo fupi zinazoonyesha maungo yao. Hawa nao ni lazima wanalipa
fidia ya kasoro fulani waliyo nayo. Inawezekana wameshindwa kulinda
ndoa zao, au inawezekana hawajaolewa na sasa wanataka kuonyesha kwamba,
pamoja...